Wadada mkipata kazi muwe na heshima na busara

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,379
Habari wadau,

Huu uzi nauandika huku bado nikiwa na maswali kibao kichwani,

Leo asubuhi nilikuwa na mishe za town mapema sana hata ofisini sijaingia, kuona hivyo nikaona bora nimchukue mke wangu nim-drop ofisini kwake halafu mimi niendelee na mishe zangu. Kufika ofisini kwake akaniambia please tangulia ofisini kwangu nisubiri nakuja naenda kumuona dokta Salma maana anataka change na wewe umeniambia utapitia bank, so ngoja nikamuone nichukue hizo pesa zake nikuletee.

Mimi nikaelekea ofisini kwake, ile nafika tu najiribu kukaa kwenye kochi pale karibu na reception yule mama aliekuwepo pale si akanifurumusha tena kwa maneno yasiyo mazuri. Namnukuu "we kaka we haya vipi? Mbona unakaa hapo? kakae kuleee kwenye viti huku ni ofisini."

Nikamwambia kwani na hivi si pia viti, na nilimkuta mshkaji flani hivi kakaa hapo anachezea simu lakini hakuonekana kuwa staff. Mimi nikaona nisibishane nae nikainuka nikasimama pembeni namsubiri mke wangu, mara mke wangu akaja, kuniona tu akajua nimekasirika. Akanipa pesa za change nikasepa.

Niipo njiani naelekea mishe akapiga, akaniuliza una nini mume wangu? Nikampa kisa chochote cha yule receptionist. Sijui kilichoendelea ila baada ya muda akanitumia SMS " msamehe mume wangu kaniomba msamaha, alikuwa hajakujua wewe ni nani, lakini pia ungemwambia kama wewe mume wangu"

Nikamwambia mke wangu, kwa hiyo angeniheshimu tu kwa kuwa mimi mume wako? Vipi watu wengine ambao wanakuja hapo ofisini kwenu na hawamjui mtu hapo? Ndio mnavyowafanyia hivi? Mke wangu akaniambia usijali nitadeal nae. Kwa hasira nikamwambia mke wangu, mwambie ajirekebishe, asiwe na dharau, au kwa kuwa nilikuwa sijachomekea na kuvaa shati kali na suruali kali? Au kwa vile nilikuja na makobazi? Mwambie kama hajui mshahara wangu ni mara nane ya mshahara wake. Acheni dharau.

Siku moja nipo Tanga natoka site nimechafuka na pikipiki ya mzee jioni nipo mitaa ya mgandini market pale, kikawaida jioni traffick ni kubwa sana mitaa ile, pamoja na congestion basi kuna dada mmoja na kiscudo chake kidogo nimchune, yaani yule dada alishusha kioo akaniangalia kwa dharau halafu akaniambia ungeichuna hii ungenijua mimi ni nani, aiseee nilimuwakia vibaya sana. Alidhani labda ni bodaboda flani tu hivi, na hata ningekuwa ni bodaboda hana haki ya kunionyesha dharau.

Wadada mkiajiriwa mjiangalie, dharau zenu na kujiona mmefika hakutowanufaisha chochote.
 
Back
Top Bottom