Wachunguzi: Jamhuri ni nani tunayesalimu kwa jina lake?

kudamademede

Member
Jan 1, 2020
62
241
Tanzania ni Nchi inayoongozwa na wanadamu ambao wameumbwa na Mungu na wanapata nguvu ya kuongoza na kutawala kutoka kwa mwenyezi Mungu aliyewaumba. Hii bila ubishi wala majivuno wala matambo.

Mkuu wa nchi ana nafasi kubwa sana ya kuwafanya wananchi wake wamtegemee Mungu au wasimtegee Mungu bali wazitegemee akili zako. Tunaweza kukubaliana kama tulivyokubaliana tangu zamani kuwa serikali haina dini lakini hatuwezi kamwe kukubaliana kwamba Serikali haina Mungu.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu baada tu ya Kuapishwa kuongoza nchi yetu baada ya Hayati Magufuli kufariki ameibuka na salamu mpya kabisa ambayo anaitumia kuwasalimia wananchi na viongozi wa serikali yake nanukuu “NAWASALIMU KATIKA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA”

Hii sio salamu ni dhihaka kubwa sana ambayo kama haitasitishwa basi kuna siku Mungu ataikinai na wananchi wataichoka na hapo itabidi tuegeshe jahazi kama sio kubadilisha nahodha.

Wachunguzi wa mambo tunahoji; Huyu Jamhuri ya Muungano ambaye rais anatumia jina lake kutusalimia ni nani? Wakiristo wamezoea kusalimiana katika jina la Yesu huku wakiitikia AMINA na Waislamu wakitumia As-salamu alaykum huku wao wakiitikia Wa alaykumu s-salam. Je, huyu Jamhuri ya muungano ni sawa na Yesu wa wakristo au Allah wa waislamu?

Je, tunaweza naye kumwamini kwamba atatuvusha katika matatizo na shida tulizonazo kama wakristo wanavyofanya kwa Yesu au waislamu wanavyofanya kwa Allah? Je, huyu Jamhuri ameanza lini hii kazi na kabla ya hapo alikuwa wapi maana hatukuwahi kumsikia akitajwa kwa utukufu namna hii?

Tangu salamu hii imeanza kuna baadhi ya mambo yameanza kutokea na hapa tumeona tuchunguze machache yake:

Jamhuri amekuja na barakoa na social distancing ambazo kwenye awamu ya sita tulizitupilia mbali na kumwamini Mungu na kweli alitusaidia na dunia ilistaajabu jambo hilo.

Jamhuri amekuja na ujambazi na uporaji wa kiwango cha juu sana vitu ambavyo tulikuwa tumesahau kabisa kama huwa vipo.

Jamhuri anataka kutuletea chanjo, tudungwe vitu tusivyovijua kisha tuitikie kazi iendelee. Tulijua alikuwa anamsadia hayati Magufuli kulinda na kutetea wananchi wa Tanzania lakini dalili za kutaka wananchi wapewe chanjo zinafanya tuhoji kama kweli salamu hii yenye jina la Jamhuri inafaa kweli kwetu.

Wachunguzi wa mambo tunahoji ripoti ya uchunguzi wa chanjo ya Corona kama inafaa kutoa mwelekeo wa serikali katika kuwaamulia wananchi wetu.

Ni tafiti zipi alizotumia Rais Mwinyi wa Zanzibar kuhalalisha chanjo kwa wananchi wa Zanzibar? Je, Rais amekutuma uanze wewe kisha apime upepo ukoje kabla ya kuwadunga wananchi wa bara? Je, mmejiandaa na matokeo baada ya kuwachoma watu hivyo vyuma mwilini? Je, mko tayari kujibu mbele ya aliyewaumba sababu zilizowapelekea kufanya hivyo?

Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni. Bila shaka mmetumia mbinu hii kwa kujificha kwenye salamu ya jamhuri ambayo kwa hakika mnajua haina Mungu ndani yake. Mmeona mtumie jina la Jamhuri kuleta chanjo kwa watu ambao walitumia jina la Mungu na wakashinda.

Bado kuna ya kujirekebisha kwenye mambo mnayotaka kufanya kwa watu wa Mungu; hakuna faida yoyote mtakayopata kwa kuwauza wananchi na kuwakumbatia watu ambao tangu asili hawana nia njema na sisi.

HATUTAACHA KUHOJI NA KUCHUNGUZA MAMBO.

NISAIDIENI SANA KUMTUMIA UJUMBE HUU RAIS WA TANZANIA, MH SAMIA SULUHU HASSAN. TUNAMPENDA NA HIVYO ARUDI KWENYE MSATARI HARAKA SANA.

Wachunguzi wa Mambo
 
Kanisa lako unaloabudia ndani yake liko katika hiyo ARDHI YA JAMHURI....

Msikiti wako unaoswalia ndani yake uko katika hiyo ARDHI YA JAMHURI.....

Maslahi ya KIUSALAMA ya maaskofu na wachungaji wako ,yanaangaliwa na hiyo JAMHURI....

Maslahi ya KIUSALAMA ya maustadhi na masheikh wako yanachungwa na hiyo JAMHURI.....

Bidhaa zako unazotumia wewe ,mumeo ,mkeo ,wanao ,wazee wako na nduguzo usalama wake kwenu unaangaliwa na hiyo JAMHURI......

Kwa ufupi kabisa ,JAMHURI iko kwa AJILI YAKO....KWA AJILI YA MAISHA NA USTAWI WAKO....utake usitake!!!!

#KaziIendelee
#NchiKwanzaKablaYaKilaKitu
#SiempreSiempreJMT
#HastaLaVictoriaJMT
 
Holy Crap, umeandika Utumbo

Nyie Mlifikia Hatua ya Kumfananisha Jiwe na Yesu, Mkaenda Mbali kumuamuru Mungu eti amshukuru Jiwe, Mkamchonganisha Jiwe na Mungu maana hakuwakemea waliokuwa wanamfananisha naye, Jiwe hakumrudishia Mungu utukufu wake.

Matendo Ya Mitume 12:21-23

21 Siku ya hao wajumbe kumwona mfalme ilipofika, Herode alivaa mavazi rasmi ya kifalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi akaanza kutoa hotuba.
22 Alipokuwa akihutubu watu walimshangilia, wakapiga kelele wakisema, “Hii ni sauti ya Mungu! Sio sauti ya mwanadamu!”
23 Mara malaika wa Bwana akampiga Herode; akaliwa na funza akafa kwa sababu hakumpa Mungu utukufu.
 
Aibu yako umeandika utumbo mtupu,kama wewe ni baba wa familia sipati picha unavyowalea watoto wako.Nakushauri ebu fanya kazi acha kumpiga majungu mama wa watu...Poor you! and Shame upon you.
 
🤣🤣
 
Dini ni Imani, Imani ni yako Binafsi kama wengine walivyo na Imani zao (Hata mwingine akisema Jamuhuri ndio Mungu wake ni yeye na Imani yake)

Hivyo basi kama wewe ni Mtanzania basi upo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (hautaki, unaweza kubadilisha uraia) Ila sio wote wanaomwamini Mungu (na kutokumwamini Mungu hakuwafanyi wasiwe watanzania) Kwanza kuna mababu zetu walipigana na kufa kwa kupinga hizi Imani zilizokuja na baadae indirectly kutuletea Ukoloni (kwahio wewe hukatazwi ndani kwako unaweza kuendelea kusalimiana kama unavyotaka)
 
Sio bidhaa zote sokoni zinafaa kwa matumizi yote...chukua inayokufaa. Tunaosalimiana kwa jina la aliehai tuendelee wanaosalimiana kwa majina ya visivyo hai waendelee pia ...ili tuchambuane. Assalamualaikum! ....Bwana Yesu asifiwe!.
 
Mkumbushe pia hata akikosa anaweza kushtakiwa na Jamuhuri.
Kanisa lako unaloabudia ndani yake liko katika hiyo ARDHI YA JAMHURI....

Msikiti wako unaoswalia ndani yake uko katika hiyo ARDHI YA JAMHURI.....

Maslahi ya KIUSALAMA ya maaskofu na wachungaji wako ,yanaangaliwa na hiyo JAMHURI....

Maslahi ya KIUSALAMA ya maustadhi na masheikh wako yanachungwa na hiyo JAMHURI.....

Bidhaa zako unazotumia wewe ,mumeo ,mkeo ,wanao ,wazee wako na nduguzo usalama wake kwenu unaangaliwa na hiyo JAMHURI......

Kwa ufupi kabisa ,JAMHURI iko kwa AJILI YAKO....KWA AJILI YA MAISHA NA USTAWI WAKO....utake usitake!!!!

#KaziIendelee
#NchiKwanzaKablaYaKilaKitu
#SiempreSiempreJMT
#HastaLaVictoriaJMT
 
Tanzania ni Nchi inayoongozwa na wanadamu ambao wameumbwa na Mungu na wanapata nguvu ya kuongoza na kutawala kutoka kwa mwenyezi Mungu aliyewaumba. Hii bila ubishi wala majivuno wala matambo.

Mkuu wa nchi ana nafasi kubwa sana ya kuwafanya wananchi wake wamtegemee Mungu au wasimtegee Mungu bali wazitegemee akili zako. Tunaweza kukubaliana kama tulivyokubaliana tangu zamani kuwa serikali haina dini lakini hatuwezi kamwe kukubaliana kwamba serikali haina Mungu.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu baada tu ya Kuapishwa kuongoza nchi yetu baada ya Hayati Magufuli kufariki ameibuka na salamu mpya kabisa ambayo anaitumia kuwasalimia wananchi na viongozi wa serikali yake nanukuu “NAWASALIMU KATIKA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA”

Hii sio salamu ni dhihaka kubwa sana ambayo kama haitasitishwa basi kuna siku Mungu ataikinai na wananchi wataichoka na hapo itabidi tuegeshe jahazi kama sio kubadilisha nahodha.

Wachunguzi wa mambo tunahoji; Huyu Jamhuri ya Muungano ambaye rais anatumia jina lake kutusalimia ni nani? Wakiristo wamezoea kusalimiana katika jina la Yesu huku wakiitikia AMINA na Waislamu wakitumia As-salamu alaykum huku wao wakiitikia Wa alaykumu s-salam. Je, huyu Jamhuri ya muungano ni sawa na Yesu wa wakristo au Allah wa waislamu? Je, tunaweza naye kumwamini kwamba atatuvusha katika matatizo na shida tulizonazo kama wakristo wanavyofanya kwa Yesu au waislamu wanavyofanya kwa Allah? Je, huyu Jamhuri ameanza lini hii kazi na kabla ya hapo alikuwa wapi maana hatukuwahi kumsikia akitajwa kwa utukufu namna hii?

Tangu salamu hii imeanza kuna baadhi ya mambo yameanza kutokea na hapa tumeona tuchunguze machache yake:

Jamhuri amekuja na barakoa na social distancing ambazo kwenye awamu ya sita tulizitupilia mbali na kumwamini Mungu na kweli alitusaidia na dunia ilistaajabu jambo hilo.

Jamhuri amekuja na ujambazi na uporaji wa kiwango cha juu sana vitu ambavyo tulikuwa tumesahau kabisa kama huwa vipo.

Jamhuri anataka kutuletea chanjo, tudungwe vitu tusivyovijua kisha tuitikie kazi iendelee. Tulijua alikuwa anamsadia hayati Magufuli kulinda na kutetea wananchi wa Tanzania lakini dalili za kutaka wananchi wapewe chanjo zinafanya tuhoji kama kweli salamu hii yenye jina la Jamhuri inafaa kweli kwetu.

Wachunguzi wa mambo tunahoji ripoti ya uchunguzi wa chanjo ya Corona kama inafaa kutoa mwelekeo wa serikali katika kuwaamulia wananchi wetu.

Ni tafiti zipi alizotumia Rais Mwinyi wa Zanzibar kuhalalisha chanjo kwa wananchi wa Zanzibar? Je, Rais amekutuma uanze wewe kisha apime upepo ukoje kabla ya kuwadunga wananchi wa bara? Je, mmejiandaa na matokeo baada ya kuwachoma watu hivyo vyuma mwilini? Je, mko tayari kujibu mbele ya aliyewaumba sababu zilizowapelekea kufanya hivyo?

Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni. Bila shaka mmetumia mbinu hii kwa kujificha kwenye salamu ya jamhuri ambayo kwa hakika mnajua haina Mungu ndani yake. Mmeona mtumie jina la Jamhuri kuleta chanjo kwa watu ambao walitumia jina la Mungu na wakashinda.

Bado kuna ya kujirekebisha kwenye mambo mnayotaka kufanya kwa watu wa Mungu; hakuna faida yoyote mtakayopata kwa kuwauza wananchi na kuwakumbatia watu ambao tangu asili hawana nia njema na sisi.

HATUTAACHA KUHOJI NA KUCHUNGUZA MAMBO.

NISAIDIENI SANA KUMTUMIA UJUMBE HUU RAIS WA TANZANIA, MH SAMIA SULUHU HASSAN. TUNAMPENDA NA HIVYO ARUDI KWENYE MSATARI HARAKA SANA.

Wachunguzi wa Mambo
Labda waulize wale jamaa wanaoshitakiwa na jamuhuri watakuwa wanamfahamu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom