Wachungaji wa Kike na Wahubiri wengine mnasemaje kuhusu kifungu hiki cha Biblia Takatifu?

92mtl

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
461
308
kama kichwa cha habari kinavo sema napata wakati mgumu niki soma walaka wa kwanza wa 1wakolinto 14:34-35
34: Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
35: Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
36: Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
37: Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

Nawasilisha ili tujadili kwa pamoja heading iskupe shida tufafanuliane tupanuane kiupeo
 
Attachments

  • Wakorintho_14.mp3
    937.7 KB · Views: 338
Bible ipo deep sana......

Yoeli 2:
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
 
Hapo lazima waingie mitini kwa staili ya kusema roho mtakatifu kawatokea!! Shida ni kuwa tunajuaje kama ni roho takatifu au ni ya shetani iliyowatokea?? Jibu rahisi ni kuwa roho yoyote inenayo kinyume na maandiko ni ya shetani!.
Ukweli ni kwamba mwanamke hata kusimama ktk minmbari haruhusiwi, lkn cha ajabu makanisani watu wanacheza kabisa kwa kunengua nyimbo za injiri juu ya jukwaa. Ni haraam! Tena ni haraam!. Kila nikitafakari siku ile, nahuzunika sana maana itakuwa ni siku ngumu sana! Itakuwa ngumu mno! Hii ni siku ya kiama, watu wengi hawaamini lkn kiyama ni kweli kipo.
 
Bible ipo deep sana......

Yoeli 2:
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
Kunahitaji mwongozo wa roho mtakatifu katika kuisoma biblia
 
Hili ni agano la kale ambalo kwa mujibu wa wakristo limefutwa kwa agano jipya. Usifute kifungu cha agano jipya kwa kutumia agano la kale. Angalia usije kuwa mtu wa motoni.
 
Nyaraka za Mtume Paulo ziliandikwa kuwalenga watu fulani. Miongoni mwa Wakorintho, mwanamke hana nafasi ya kuzungumza mbele za kadamnasi.

Paulo aliwaambia Wakorintho yanayowahusu Wakorintho, lakini si kwamba aliwakataa wanawake. Soma Matendo 18:24-26
hivyo maandiko ya paul yote ni kwa ajili ya wakoritho na sio maagizo kwa kanisa?
 
Kunahitaji mwongozo wa roho mtakatifu katika kuisoma biblia
Hapa ndipo wakristo wanaponiachaga hoi wakiona umewabana kwa hoja iliyo dhahiri katika biblia lazima watakimbilia kumsingizia roho mtakatifu. Hapa ndio tunajiuliza roho gani mtakatifu anaenda kinyume na andiko takatifu!!!. Je haiwezi kufikirika kuwa shetani kajifananisha na roho takatifu ili kuwapoteza wajinga??
Anyway Ngoja tuwaachie wenyewe, Mwenyezi MUNGU anajua yale tusiyoyajua. Kwa ujumla watu wengi wametupa maandiko migongoni mwao wameamua kufuata matamanio yao ya kidunia. Siku ile ya Hesabu tuiogope maana ni chungu sana.
 
Nyaraka za Mtume Paulo ziliandikwa kuwalenga watu fulani. Miongoni mwa Wakorintho, mwanamke hana nafasi ya kuzungumza mbele za kadamnasi.

Paulo aliwaambia Wakorintho yanayowahusu Wakorintho, lakini si kwamba aliwakataa wanawake. Soma Matendo 18:24-26
Duu sasa mistari iliyoandikwa kwaajili ya waafrika ipo wapi?? Kwa hiyo kitabu cha biblia hakiwahusu wale ambao hawakuandikiwa; maana maandiko ya paulo karibu yote yaliwalenga watu fulani eg Timotheo n.k
 
Hili ni agano la kale ambalo kwa mujibu wa wakristo limefutwa kwa agano jipya. Usifute kifungu cha agano jipya kwa kutumia agano la kale. Angalia usije kuwa mtu wa motoni.
Agano jipya halijafutwa, wakristo wanaosema hivyo wanatumia roho mtakafujo.
 
Back
Top Bottom