Wachungaji na Masheikh wa mishahara wanaoshindwa kukemea wanasiasa waovu, ndio wanaofanya watu waidharau dini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
WACHUNGAJI NA MASHEIKHE WA MISHAHARA WANAOSHINDWA KUKEMEA WANASIASA WAOVU, NDIO WANAOFANYA DINI IDHARAULIKE.

Kwa Mkono wa Robert Heriel.

Kazi hudhaulika pale uasi unapotamalaki, hata ile kazi iliyonjema na halali hudharaulika na kuwa ya aibu pale waovu wanaposhika kazi hizo. Zama hizi, kazi karibia zote zimeharibika kutokana na uasi kutamalaki, Uasi ni nini? ni kwenda kinyume na sheria za Mungu, uasi katika kazi hutokana na watu kuwa wabinafsi na kuthamini PESA kuliko UTU. Kuthamini pesa ndio sababu hasa ya kazi nyingi kudharaulika.

Inafahamika kuwa kazi zote zilizohalali ni kazi za Mungu, iwe ni Udereva, Ukulima, ufugaji,Upolisi, uanajeshi, Ualimu, Udaktari, uhunzi, Uanasheria, uhasibu, Uchungaji miongoni mwa kazi zingine. Kila mara naandikaga kuwa kazi uifanyayo ikiwa ni halali basi kaa ukijua kabisa ni kazi ya Mungu. Hivyo nimesema haya ili kuendelea na harakati zangu za kufuta ile kasumba iliyopo ndani ya jamii yetu isemayo; Uchungaji, unabii, uaskofu, ukuhani, Upadri, usheikhe, uimamu, usharifu ndizo kazi za Mungu pekee. Kazi zote ni kazi za Mungu, na kila mtu anamtumikia Mungu kwa kazi yake.

Kila kazi inadhima yake, lakini lengo kuu la kazi zote duniani ni kulinda UTU wa binadamu. Kumfanya mtu aishi maisha ya furaha na amani. Kazi yoyote isiyoendana na lengo kuu la Kulinda UTU wa binadamu huitwa kazi HARAMU, na ndizo hizo hukatazwa na MUNGU. Kazi haramu ni zile kazi zinazotweza, kuharibu na kudhalilisha utu wa binadamu, zinazoathiri na kuleta madhara kwenye maisha ya mwanadamu na viumbe wengine.

Kama nilivyosema, kila kazi ina dhima yake ndani ya jamii. Zipo kazi ambazo zima zake ni Kutoa ELimu ndani ya jamii, kazi hizo ni kama vile Ualimu kwa aina zake, Uchungaji na Ushekhe kwa aina zake. Kazi za Ulinzi na usalama ni Upolisi kwa aina zake, kazi za usafiri ni Udereva kwa aina zake, Kazi za Afya ni utabibu kwa aina zake miongoni mwa kazi na dhima zake zingine.

Katika mada yetu leo ya FANI YA UCHUNGAJI NA USHEIKHE ambayo dhima yake kuu ni kutoa elimu ya kiroho, kwa kufundisha, kukemea,kuonya, kufafanua, kueleza, mazuri na mabaya ambayo ni makosa mbele za Mungu.

Ili kazi ya uchungaji na usheikhe iwe halali lazima izingatie mambo hayo hapo juu, lakini kinyume chake ni kuifanya kazi hiyo kuwa HARAMU kabisa.

Mchungaji au Sheikhe anapotoa elimu pekee ya kidini, kuifafanua, kuielezea, bila kukemea, na kuonya watawala waovu anaingia katika kundi la watumishi haramu katika kazi yake.

Waalimu mashuleni na vyuo moja ya majukumu yao ni kusahihisha na kukosesha(kukosoa) pindi wapimapo wanafunzi wao. Mwalimu anayeweza tuu kumpa sahihi mwanafunzi mahali alipopatia alafu akashindwa kumkosesha mwanafunzi mahali alipokosea huyo atakuwa mwalimu haramu. Ndivyo katika kazi ya Uchungaji na Usheikhe.

Mchungaji na sheikhe ni mwalimu wa jamii katika masuala ya kiroho, hapaswi kuogopa wanafunzi wake licha ya kuwa wapo wanafunzi wa hulka, na hadhi tofauti tofauti.

Siku hizi kazi ya Uchungaji na Usheikhe ni moja ya kazi zinazodharaulika kutokana na Wachungaji na Masheikhe wengi kuwa watu wa mishahara. Wamegeuka watumishi njaa hali inayowaathiri katika utendaji wa kazi yao ya uchungaji au Usheikhe.

Tabia za Wachungaji na Masheikhe wa siku hizi wanaofanya dini zidharaulike na wao kuonekana vioja ni kama ifuatavyo;
1. Wengi wao ni wapenda fedha zaidi kuliko huduma
2. Wengi wao hawana elimu ya kutosha ya dini hasa hasa wachungaji(madhehebu ya ukristo) Mtu akishajua vifungu viwili anaanzisha kanisa. Kidogo Masheikhe wanajitahidi kwani ni ngumu kuwa sheikhe pasipo kujua uislam. Ila kwa Ukristo mtu yeyote hata asiye na uelewa anaweza kuwa Mchungaji na akajiita nabii.

3. Wengi wao ni waoga, hawana uwezo wa kuwakemea watu wenye vyeo vikubwa wakiwemo watawala na matajiri
4. Wengi wao ni wanafiki na hawana uwezo wa kutenda kwa haki kwani sio wachungaji na masheikhe halisi bali ni watu wa mishahara
5. Wengi hupenda kujipendekeza kwaa watu wakubwa hata kama watu hao wanashutuma za kutenda maovu
6. Wengi wao ni watetezi wa watawala hata kama uovu unafanywa na hao watawala.
7. Asilimia 90% hawawezi kukemea maovu yafanywao na watawala wao ni kusifia na kutafuta vifungu mshenzi kutoka katika vitabu.

8. Wengi hujipendekeza na kuona fahari kwenye shughuli za watu wakubwa kama watawala na matajiri kama vile matukio ya misiba na harusi bila kujali matendo mabaya ya wakubwa hao lakini kamwe hawawezi kujipendekeza kwa masikini hata kama angekuwa anamatendo mema.
9. Wengi hutumia sheria za dini kwa watu masikini lakini sheria hizo hazifanyi kazi kwa watu wakubwa yaani watawala na matajiri hata wafanye mabaya yapi.
10. Wengi wao humwogesha shetani na kumpaka manukato mazuri kwa kutumia aya za kwenye vitabu. Mtawala afanyapo mabaya, basi baadhi ya wachungaji na masheikhe huitwa kumuogesha na kumsafisha kisha kumpaka mafuta ili mtawala aonekane hakufanya ubaya wowote.

11. Wengi hutumia lugha za vitisho kuwatishia watu kuhusu adhabu za Mungu badala ya kufanya kazi ya kufundisha, kufafanua, na kuonya. Wengi hutumia vitisho ili kujenga hofu kwa waumini. Wanasahau MUNGU ni baba wa wote.
12. Wengi hupenda zaidi mafundisho ya pesa.

Nilifanya Utafiti mdogo ambao nitauachia hivi karibuni kuwa, ni kwa nini wanawake wengi hawapendi kuolewa na Wachungaji na Masheikhe? Majibu yalishtua, bila shaka nawe yatakushtua. Hata wewe unaweza kuuliza wanawake kumi kama sample ndogo hapo mtaani kuwa je wangependa kuolewa na mchungaji au sheikhe alafu utakuja kubaini kuwa wengi wao yaani 9 kama sio wote wanaweza kukataa. Na hii ni kutokana na wachungaji na masheikhe wengi kuikosea heshima kazi yao.

Niwaombe Wachungaji na Masheikhe mfuate dhima ya kazi yenu, acheni kuogopa wanafunzi wenu wakati ninyi ndio waalimu wa kuwafundisha mambo ya kiroho. Msifanye dini idharaulike na MUNGU kuonekana ni hamnazo, au mshenzi kwaa tabia zenu za hovyo.
Uchungaji sio kubeba mavitabu makubwa ya dini, na kuvaa majoho makubwa huku mkiwa mmevaa makofia vichwani vyenu; Na usheikhe sio kuvaa Kanzu za dubai na vikoti vilivyodariziwa, kichwani mkiwa na barakasheikhe na fimbo mkononi. Sio usimamapo kwenye madhabahu kupiga piga kelele kama vichaa huku mkishindwa kuwakemea watawala waovu.
Hayo Maleba kila mtu anaweza kuyavaa tuu. Uchungaji na Usheikhe ni elimu ya Mungu, miiko na maadili yake kuyatekeleza.

Nawapongeza Wachungaji na Masheikhe wote ambao mmeendelea kusimamia maadili ya kazi yenu bila kuogopa changamoto. Niwape moyo msikate tamaa kwa uchache wenu, chapeni kazi ya MUNGU. Tunajali na kuthamini kazi zenu. Tunajua hamna pesa inayozidi lakini Mungu hawanyimi pesa ya mahitaji ya lazima.

Yohana 10:12
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.

Ni mimi Mwana kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa iringa Mjini
 
Sasa hivi mafundisho ya dini yamegeuzwa biashara na wahuni wachache wasio na hofu ya Mungu, ukitaka kuamini hilo shauri ibada ziongozwe kwa kujitolea kama ilivyo kwa Mashahidi wa Yehova.
 
Sasa hivi mafundisho ya dini yamegeuzwa biashara na wahuni wachache wasio na hofu ya Mungu, ukitaka kuamini hilo shauri ibada ziongozwe kwa kujitolea kama ilivyo kwa Mashahidi wa Yehova
Kwa sasa ni biashara halisi kabisa.

Hakuna cha wito tena
 
Tunasoma Alana za nyakati mwana fasihi. Kama kukosoa Basi ni kistaarabu. Lakini pia, unapoikosoa serikali lazima pia uishauri Cha kufanya. Na ushauri sio amri kwamba ni lazima utekelezwe. Unaweza kushauri lakini anayeshauriwa akagoma kukufuata ushauri wako. Je utamlazimisha kufanya Kama ulivyomshauri?. Kumbuka mfano wa Yohana mbatizaji na Herode kilitokea Nini eee mwana fasihi? Tunatumia maandiko pia kwamba,` aonywaye Mara nyingi akishupaza shingo atavunjika ghafla Wala hatapata dawa';. Baada ya hapo tunarudi kuendelea kupiga magoti madhabahuni kwa Bwana. Kwa uchache, Asante.
 
Napokea maoni yako Mkuu
 
Back
Top Bottom