Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni Kujamiiana
Nilivyoelewa MIMBA ni MATOKEO TU ya KUJAMIIANA
Wakuu kwani tatizo ni Kujamiiana kabla ya Ndoa au Mimba kabla ya Ndoa?
Deuteronomy 22:20-21 NAB
LAKINI IKIWA NI KWELI NENO HILI..LA KUTOONEKANA KWAKE YULE KIJANA ALAMA ZA UBIKIRA; NA WAMTOE NJE YULE KIJANA MLANGONI PA NYUMBA YA BABAKE WAMPIGE MAWE MPAKA AFE..KWA ALIVYOFANYA UPUMBAFU WAKE...KWA KUFANYA UKAHABA KATIKA NYUMBA YA BABA YAKE......
SO UKIWA UNAZINI UKIWA BADO KWA WAZAZI WAKO HAKUNA SABABU YA WEWE KUTOPIGWA MAWE...MNALIJUA HILI...SO UTAONA MIMBA NI KAMA MATOKEO TU NA DHANA ZAIDI NI KUZINI .....YAANI UZINZI..MMMHHH TOPIC NJEMA
Mtowa maoni inaelekea unasoma Bible iyokwisha pitwa na wakati ambayo hakidhi mahitaji ya wafuwasi wake katika karne hii pia unasahau kuwa Bible imekuwa ik upgrade kwa kudhi maisha ya kile na ndio maana makanisa mengi kwa sasa yamekubali kuwa Gays na Lisbia wanaweza kuwa wachungaji wa makanisa kwani wanachokifanya kanisani ni kumtumikia Mungu wao,pia katika ukatoliki kulikuwahakuna Ngono kabla ya ndowa lakini kwa sasa hilo limepanguswa ,binafsi naliona hilo halina matatizo pia angalau wao wanafunga ndowa wazungu walioleta Hii dini hapa Tz wao sikuhizi hata haya mambo ya ndowa hayana nguvu wewe zalisha tu .
Pdidy sio makanisa yote, makanisa ya kiprotestant ndio yako hivi, nayo hutegemea aina ya pastor wa mahali hapo,
Mimba ni alama ya kuwa hawa watu walikutana kimwili, Bible hairuhusu kukutana kimwili kabla ya ndoa, na hatujui namna ya kujua hawa walikutana kimwili au la, Mimba ni moja ya kithibitisho kuwa hawa watu walikiuka maadili ya biblia, kuruhusu watu kuoana na mimba ni kuhalalisha tendo lifanyike kabla ya ndoa!
Huwa nasema kila siku there is no compromise katika kumfuata Mungu,so as there is no compromise kufuata katiba zetu za organisations, taifa, n.k
Kushindwa kulinda na kusimamia kile kinachopaswa kufuatwa kwa gharama yeyote ni ushahidi tosha wa dini za kuletewa na kurithishwa, NDIO tunatka hapo tunaenda CCM,CHADEMA , kwenye makampuni tunayafisadi hili hali tukijua katiba na miiko!
Hii ni makosa, I am pastor though!
Mhhhhhh hapooooooooooo nnaona NDOA NI CHACHE SANA
HASA UPANDE WA DAR ES SALAAM KARIBU KILA NDOA MAKANISANI KAMA HAWANA MIMBA BASI WANAISHI PAMOJA NA KAMA HAWAISHI PAMOJA BASI WALIKUWA WANAZINI KABLA YA NDOA....
Wakuu kwani tatizo ni Kujamiiana kabla ya Ndoa au Mimba kabla ya Ndoa?
Mama Mia hili swala siku hizi gumu sana, watu wengi siku hizi wanafunga ndoa wameshakutana kimwili, ni asilimia chache sana wanafunga ndoa takatifu.Unajua tatizo tunalolalamikia hapa ni si haki kufungisha ndoa za wenye mimba na wasio na mimba at the same tyme lazima tuwaheshimu hawa wanaokuja kanisani hawajakutana kimwili......ukisoma kwenye biblia
Utawajua tu! mkuu, mimi nimeoa mwaka 2006, sikuwahi kukutana kimwili na mke wangu kabla ya ndoa, wala aina ya tendo lolote linaloweza kutafsirika ni mapenzi! Yet I live in DSM! Ndio nikauliza ni aina ya makanisa gani hayo?? sio wote mkuu, trust me wako wengi, japo hawavumi. ni sawa na walewale kuwa bila nyumba ndogo hakuna maisha, simply kwa sababu yeye ana udhaifu huo!
Tatizo kubwa hapa ndugu ni kujamiiana kabla ya ndoa. Mimba ni matokeo na only indicator kuwa hawa watu walikutana kimwili, kwa hiyo NI KITU AMBACHO wachungaji wana uwezo wa ku-control, kwa maana ya kukemea, ukikubali matokeo maana yake umekubali source(umehalalisha practise). na hata watoto ndani ya nyumba tunawaonya kwa makosa wanayofanya, then tunakuwa tumerekebisha tabia yake,
Majaji wanawahukumu waliopelekwa mahakamani, japo wezi wako wengi, polisi hukamata wanaowaona, japo wezi wako wengi, tunaowaita mafisadi tutawaita tu wezi kwa sababu tumewajua, lakini nyuma ya pazia wako wezi, mafisadi na wakosaji wengi.
Wachungaji wangedeal na haya matokeo, ni rahisi kuzuia chanzo,just imagine watoto wanaopevuka miaka wanaambiwa ngono haina makosa, maana hata ukipata mimba unakaribishwa, otherwise what is religion then??
Tuite spedi spedi, japo ni wazuri kutetea haya mambo, mbona the same makanisa zamani haya yalikuwa hayatokei? na yakitokea wachungaji walikuwa wanakataa? kwa nini imeanza kuanzia miaka ya 1990, na imekithiri miaka ya 2000, miaka 50 ijayo, si tutaenda ngazi nyingine ya immoral?? au zamani hawakuwa na viungo active vya uzazi??
Lazima tujue chanzo cha hili tatizo, tuliseme, tujadili, bila kujitetea hata kama sisi wakosaji! then tujue ikiwa hili LA MIMBA LINATETEWA HIVI JE YA UFISADI?
ARE OUR CHURCHES IS REAL CHURCHES OR JUST A SOCIAL CLUBS?? ARE THEY REAL FOLLOWING WHATS WRITTEN IN THE BIBLE?
Lets go to the basics??
Unajua tatizo tunalolalamikia hapa ni si haki kufungisha ndoa za wenye mimba na wasio na mimba at the same tyme lazima tuwaheshimu hawa wanaokuja kanisani hawajakutana kimwili......ukisoma kwenye biblia
Hivi ndoa nini haswa? Je kama mmefanya mambo yote ya kimila kwa mfano mwanaume amepeleka posa na mahari upande wa mwanamke. Na pande zote za kike na kiume wamejua kwamba watu hawa ni wachumba. Je hapo kama mkiamua kula tunda kuna dhambi au tayari imekuwa halali kwa kuwa ndoa ya kimila imefanyika?
Mkuu wangu Waberoya ( Mhandisi na Mchungaji) wewe ni Mchungaji kama status yako inavyoonyesha!
Jee unataka Wachungaji wa control vipi hii ishu? Kwa Kutaa kufungisha Ndoa zao?
Imagine wamekuja watu with round belled stomach ( Namaanisha wajawazito) kwako wewe Mchungaji, watu hawa walishatubu dhambi yao ya Uzinzi na Mungu aliyesirini amewasamehe. Sasa kama Mungu mwenyewe amewasamehe wewe mchungaji unapata wapi mamlaka ya Kukataa kutumika na Mungu kuwaunganisha Wawili hawa?
Labda ungeeleza ni namna gani wachungaji na Mapadre wanavyoweza kuli control hili jambo pasipo kumkwaza mungu aliyesamehe na kuvitakasa Viumbe hivi!