Wachungaji/mapadre hamwogopi mungu kufungisha ndoa zikiwa na mimba makanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachungaji/mapadre hamwogopi mungu kufungisha ndoa zikiwa na mimba makanisani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Oct 4, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Hili naona sasa limekuwa ni ukosefu wa adabu ama maadili katika jamii..jamani zamani mimi nijuavyo ni mafuruku kufungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake...nakumbuka kuna siku mchunganji mmoja wa lutherano mwaka jana alikataa kufungisha ndoa ya mtoto wa aliekuwa askofu mkuu mmoja moshi uko akisema kama mtaniruhusu kubariki nitabariki ndoa yenu lakini hivi mkiwa na mimba sifungishi ndoa...hakika kuliwaka moto lakini jambo ambalo sikuamini ile ndoa ilichelewa na akaja mchungaji mmoja akafungish na yeye akiwa anaona aibu akaamua kupasua adharani kama si heshima ya askofu babako kwa kweli tuingefungisha hii ndoa

  sasa hivi jambo hili limekuwa ni aibu kila makanisa sasa yamekuwa yakifungisha ndoa zikiwa na mimba ndani yake....majuzi nilihudhuria harusi moja pale st joseph kati ya harusi tano tatu wanawake walikuwa wamevimba matumbo yao kama wako theartre wanasubiri kupasuliwa ilikuwa jambo la aibu sana lakini hatimae ilifungishwa huku mapadre wakipiga makelel ya kutorudia tena watu wengine...bado najiuliza hawa watu huwa wanahonga ndoa kufungishwa hivi ama wanawafanya upofu hawa watumishi wa MUNGU....nafikiri makanisa yanaitaji kuwa mstari wa mbele kukemea na kutaa hali hizi.....wazazi imefika wakati wa kuheshimu ndoa takatifu msiwaruhusu vijana zenu kujazana matumbo na kuwatia aibu mbele ya madhabahu....imagine majana nimeenda shuguli moja nikakuta jamaa anaonyesha zile picha za mwanamke za zamani he gafla anamwonyesha yule mwanamke akiwa na bwanaharusi mtarajiwa wamekumbatiana wanalishana sasa nkajiuliza kama mmeshamaliza kila kitu tumeiwa kufanaynini???/

  Kazi kwenu mnaotarajia kuoa kuna starehe ukiwa na mtoto ndani ya ndoa...
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe unaonekana huelewi the central doctrine of Christianity, redemption.

  Kanisani si sehemu ya watu wasio na "dhambi", bali kwa mujibu wa Ukristo, ni sehemu ya wakosefu kukimbilia.Kama unataka kufungisha ndoa watu wasio mawaa basi huwezi kufungisha ndoa hata moja, kwa sababu biblia yenu yenyewe imesema wote tumekosea. Nionyeshe mtu anayesema hajakosea na mimi nitakuonyesha muongo.

  Unanikumbusha mafarisayo walivyopewa na Yesu parable ya mchungaji kumuokoa kondoo katika sabato.

  Unanikumbusha parable ya mwana mpotevu aliyefurahiwa na baba yake kurudi nyumbani baada ya kupotea kwa miaka mingi.

  Central theme ya post yako imejaa ufarisayo.

  Hivi unawezaje kujua kama ndoa inayofungishwa kwa mwanamke asiye na mimba haijakiuka misingi ya kutojuana kimwili kabla ya ndoa?

  Na kama huwezi kujua hili kwa nini u assume kwa sababu mwanamke ana mimba basi wawili hawa wamekiuka misingi hii?

  Vipi kama mimba ya mtu mwingine? Vipi kama mama kapata immaculate conception? Wakristo si mnaamini hili?

  Kwa misingi hii hata Josefu angetaka kumuoa Maria asingeweza.
   
  Last edited: Oct 4, 2009
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Hivi unawezaje kujua kama ndoa inayofungishwa kwa mwanamke asiye na mimba haijakiuka misingi ya kutojuana kimwili kabla ya ndoa?

  ENENDENI ULIMWENGUNI MKAZAE NA KUNGEZEKA...UNAJUA MAANA YA HAYA MANENO..???
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  And your point is?
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Mbona anaeleweka dhambi kufunga ndoa mkiwa na mimba bado aieleweki ama tuidhinishe hili
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo unataka wenye dhambi wasifungishwe ndoa?

  Hivi umeelewa post yangu ya hapo juu inayo underline doctrine ya redemption.
   
 7. s

  shabanimzungu Senior Member

  #7
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHRISTIANITY CORRUPTED RELIGION! GAYS...FORNICATORS.....PAEDOPHILES...What ahve you...........They have commecialized the religion and this is what you get..not to mention jews in the west who are also turning chrisianity to what it is now!!!!!!!!!!!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hebu nikuulize ndugu, mwanamme mtu mzima anayefanya ngono na binti wa miaka 8 ni pedofile au sio pedofile.

  NB: Twende taratibu usikimbie.
   
 9. s

  shabanimzungu Senior Member

  #9
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sema bwana najua una fikia wapi! endelea........hebu.
   
 10. b

  bnhai JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hii ni kiashiria kuwa uzinzi umekithiri. Aidha mtu ana tumbo au hana, bila kufuata misingi watu waliojiwekea kwa kweli ni tatizo. Hili lafaa liangaliwe kwa upana. Ni kwanini watu wanafika hapo? Maadili! au kuna mengine??
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka wenye dhambi wasifungishwe ndoa?

  ahaaaaaa
  si wenye dhambi kaka;waliozaa nje ya ndoa hawafungishwi ndoa
  wanabariki ndoa.tofautisha kati ya kufunga ndoa na kubariki ndoa....
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Jibu swali, si ulijifanya kidume?
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kubariki ndoa na kufungishwa ndoa??? Mh hapa pia kuna kazi. Ukisema mie nimeoa, utaeleweka umebariki au umefunga ndoa.
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kibaya kama kuhimiza uzinzi.....
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Ukisema mie nimeoa, utaeleweka umebariki au umefunga ndoa.


  ukisema nina mtoto;si lazima awe wako hata uliemkuta na mkeo
   
 16. b

  bnhai JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Pdidy kasema mtu alifungishwa ndoa kwa heshima ya baba yake. Wale amabo baba zao si influencial inakuwaje? Hakuna sheria kusimamia hilo??? Inamaana hakuna fair ground? Hili ni tatizo pia kuanzia kwenye siasa hadi nyumba za ibada
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Msingi wa kibiblia wa hili uko wapi? Au ni manjonjo ya maaskofu tu?
   
 18. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli hata mie jambo hili linanikera sana utakuta ndoa inafungwa b. arusi tumbo hilo.
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huu ni ufarisayo tu, asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe.

  Fuata mfano wa Yesu na yule mwanamke mchafu pale kisimani.

  Again, central theme ya ukristo si judgement, ni redemption. Usipoelewa hili tu ndiyo utakuja na huu upuuzi ulio judgemental.
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Huu ni ufarisayo tu, asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe.

  HILI LISIWE MKAZO WA KUHIMIZA UZINZI NDUGU YANGU.....,KAMA DHAMBI NI DHAMBI TU HATA HUYO UNAEMSEMEA SIKU YA MWISHO ALIAMBIWA AMEFANYA DHAMBI KAMA UMESOMA VIZURI.....
   
Loading...