Wachungaji: Magufuli si mwanasiasa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
KUWEPO kwa malalamiko kutoka pande nne za nchi kuhusu namna Rais John Magufuli anavyoongoza nchi, kumeliibua kanisa kutoa ombi maalumu kwa viongozi wengine wa dini kumsaidia rais huyo, anaandika Dany Tibason.

Godlisten Daniel, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Nzuguni, Dodoma amewataka viongozi wa dini kumshauri Rais Magufuli ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi na kada zingine.

Hata hivyo amesema, sababu kubwa ya kuwepo kwa malalamiko ni kutokana na yeye (Rais Magufuli) kutokuwa mwanasiasa kwa asilimia 100.

Pia Mchungaji Daniel amesema, katika utawala ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi yake kwa kuzingatia haki na wajibu na asiwepo mtu wa kuonewa.
Akizungumzia utawala wa Rais Magufuli amesema, kwa kipindi kifupi ambacho Magufuli amekuwa rais, kuna mambo ambayo yamezua na sintofahamu hususani katika kisiasa.
Amesema, inaonesha wazi kuwa Rais Magufuli siyo mwanasiasa kwa asilimia kubwa na badala yake ni mtendaji zaidi.

“Kutokana na hali hiyo, watu wengi watashindwa kumuelewa kutokana na misimamo yake lakini wakati huo wanasiasa wengi wanatumia siasa kuficha maovu yao wakiamini kuwa chama kitawakingia kifua.

“Tumeshuhudia utawala uliopita, watu wengi walikimbilia katika siasa kwa lengo la kuficha madhambi yao na sasa imefika hatua kuwa Rais Magufuli kaja na mbinu nyingine, ya kuifanya siasa kutokuwa kichaka cha kujificha na kuficha maovu yao”amesema Mchungaji.

Kuhusu mfumo wa kiutawala amesema, ili nchi iweze kutulia na kila mmoja afurahie matunda ya nchi yake, ni lazima kubadilisha mfumo.

“Mfumo mbovu umesababisha kuwepo kwa watu wengi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na wakati mwingine kila jambo kufanyika kisiasa hata pale isipotakiwa.

“Kila eneo siasa imekuwa ikitawala imefikia hatua ya kuingizwa makanisani na hiyo yote ni kutafuta kichaka cha kuficha maovu,sasa umefika wakati wa kila rahia kujua haki yake na kutimiza wajibu wake,” amesema.
Kuhusu ulipaji wa kodi amesema, ni wajibu wa kila Mtanzania kulipa kodi na ni vyema watanzania wakajenga desturi ya kudai risti pale wanapofanya manunuzi.
 
A

Achana na propaganda za wachungaji ambao wanatumia dini kupiga pesa. Siwaamini wachungaji tena. Magufuli ni kiongozi bora barani Afrika. Anaangalia masilahi ya wengi. Hizo ni porojo tu.
 
Soma vzr ndugu mchungaji anang'ata na kupuliza huyoo
 
Mimi naomba labda nipewe ufunuo mpya.Hivi Siasa ni nini hasa?Nini tafisiri mujarabu ya neno siasa?Je,kuwa mwanasiasa ni kuwa ndumila kuwili?Je ni kuuma na kupuliza?Je ni kuongea hata usiyoyaamini ili kufurahisha watu?Je mwanasiasa ni yule legelege kwenye kusimamamia taratibu na sheria za nchi? Je kuna mifano anuai duniani za watu waliokuwa hawana tabia fulani wakaombewa wakajikuta wanaishi kwa tabia fulani?Je,leo mtu asiye kwa mfano na tabia ya upole anaweza kuombewa akajikuta ni mkali?Hivi njia pekee anayotumia Mungu na anayoisikia ni maombi tu?Je kwa nini njia zingine za kubadilisha tabia au mazingira yetu mbona hazitumiki sana sana leo badala yake tunang'ang'ana na maombi tu. Yesu alishaweka namna ya kukabiliana na mazingira yetu. Research/elimu("...tafuteni mtapata...") au tumieni nguvu("...bisheni mlango mtafunguliwa...")
 
Ni mchungaji kama gwajima, au sadaka zimepungua ndio anaisoma namba
Sadaka ni dili ila kama kuna kamradi ka ujenzi wa barabara ya kwenda hapo kanisani hiyo inaweza kuwa dili zaidi. Wacha mchungaji asikike bana, anaweza akapata bingo!!
 
Mchungaji, wanasiasa ndo walitufikisha hapa. Mungu amesikia kilio chetu, tumempata mtu sahihi kwa wakati sahihi, wacha atupeleke kikwatakwata, nchi inyooke. Au mtumishi ulikuwa unafurahia matoleo mbalimbali yaliyotokana na mzunguko wa fedha chafu - mishahara hewa, madawa ya kulevya, ukwepaji wa kodi nk? Sidhani, wanasiasa hawawezi ondoa haya. Asiye m/siasa 100pc ndo anaweza, na huyo ni rais JPM. HAKUNA MWINGINE.
 
Back
Top Bottom