Wachungaji 10 matajiri duniani, wengi ni kutoka Afrika: tunajifunza nini?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
1:TD Jakes anautajiri wa $150.2Mil
bishop-jakes-joy-105.jpg



2:wanafungana wawili wote wanautajiri wa $150Mil

Bishop David odeyepo
3280057_davidoyedepo_jpeg75de619f148d60f3385f1c03c62e4827

Huyu ni mwanzilishi wa winner chapel, anamakanisa hadi bongoland. Anamiliki ndege (private Jets) nne, anamajumba ulaya na Marekani sio mtu wa mchezo mchezo, ana makanisa hadi ulaya ingawa yeye ni raia wa Nigeria.

Shepherd Bushiri
Prophet-Shepherd-Bushiri-during-a-humanitarian-service-in-Malawi-in-2016-700x490.jpg

Huyu ni kijana sio wa kawaida, mzaliwa wa Malawi na ana makanisa kusini mwa Africa. ana maelfu ya wafuasi nchi nyingi kusini mwa afrika ikiwemo na Bongoland. Pesa hapati kwenye Zaka na sadaka tu, anamiliki kampuni ya kielectronic, kampuni la mawasiliano, anamiliki mashamba, anachuo kikuu Sudan kusini Bushiri University of agriculture. Anaweza kuwafunika wote siku za usoni, uzi unaobamba wa Forex huko niko kawekeza Kuna hbr zake.

3:Enoch Adeboye utajiri wa dola 55mils
Capture.JPG

Huyu ni moja ya watu wenye nguvu Afrika, amewahi kutoka kweny list ya watu 50 vipanga na wenye Uwezo mkubwa (elites) duniani list ambayo iliwataja pia Obama na Rais mstaafu wa ufaransa. Ni raia wa Nigeria

4:Benny Hinn utajiri dola milioni 52
benny-hinn.jpg

Kama huwa unafungua TV lazima umewahi kukutana na huyu mtu maarufu mwenye Asili ya Israel.
Ni maarufu kwa kufanya mikutano mikubwa na miujiza pia huduma zake hurushwa dunia nzima kwenye matelevision.

5:Chris Oyakhilome utajiri dola mil 50
3161135_30431_jpega31360d48cb04b9f3abc855e2e1cdbfb

Ni mtu mnyenyekevu na mwenye ushawishi mkubwa Sana Afrika na duniani. Amewahi kukumbwa na kashfa ya utakatishaji fedha kama dola mil 35.ni mnaijeria. Anazaidi ya waumini elfu arobaini wengi wao wakiwa ni wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa. Ndio mwafrika wa kwanza katika wakristo ambaye anatv inayobroadcast masaa ishirini na nne kutokea Afrika na kusambaa dunia yote...

6:Creflor dollar utajiri dola million 27
creflo-dollar-private-jet600.jpg

Huyu ni marekani, ni muhubiri na Mwalimu wa neno
Anahudumu huko Georgia us

7: Kenneth Copeland utajiri mil 26.5 dola
Gloria-Kenneth-Copeland.JPG

Huyu ni moja ya watu wenye ushawishi mkubwa katika dunia ya wapentekoste. Aliwahi kuongea na papa franscis kwa Skype mbele ya kanisa siku mjumbe wa papa alipotembelea mkutano wa waprotestant huko US katika harakati za kurekebisha tofauti zao na Catholic church.
Pia amewahi kuchunguzwa kwa mienendo yake kipesa miaka kama mitatu mfululizo.
Huko marekani kanisa Lake lipo kwenye eneo la hekari 1500 humo Kuna Kila kitu hadi uwanja wa ndege na anajet ya $ 17Millions

8:Bill Graham - dola milioni 25
billy_graham.jpg

Huyu ni mtu wa kihistoria, amefanya mikutano mikubwa sana miaka ya zamani. Na wachungaji wengi na makanisa mengi ya kipendwa ni matunda ya kazi yake...

9:Mathew Ashimolowo
pastor-matthew.png

Huyu mnaijeria.
Makao makuu ya kanisa lake ni Maryland marekani. Alikuwa mtumishi wa kanisa moja Nigeria four square gospel church, alipotumwa atembelee Uingereza kufungua kanisa huko, Huyu jamaa alijiongeza na akajitenga hakurudi tena na akaanzisha Lake ambalo ndio limemfanya umeona hapa. Anamiliki kanisa kubwa la kipentekoste kuliko yote Uingereza. Vyanzo vyake vingine vya mapato ni kutoka kwenye uwekezaji wa hisa na machapisho yake.

10:Bishop TB Joshua - utajiri dola million 15.
10300270_627534654033981_6850412232080554025_n.jpg

Huyu sasa ndio mwisho wa maneno na maarufu sana duniani kuliko wenda wote hapo juu. Maarufu kwa kubashiri matukio kabla hayajatokea. Alianza huduma yake 1987.Ni mtu ambaye bado ni controversial kwenye masikio na macho ya wengi kwa uwezo alio nao wa kusadikika kuponya Kila gonjwa ikiwemo na kufufua. Kwa waumini na watu wanaohusudu miujiza kwenye ibada kwa huyu jamaa ndio penyewe. Anamakanisa(wafuasi) Afrika nzima, ugiriki, Asia na kote huko anajipatia mapato kwa njia ya sadaka na kumfanya awe milionea.




Haya na wakwetu Gwajima, Mwingila, mzee wa upako, mh rwakatale, Malisa, bulldozer, kakobe etc
Mjitahidi mtutoe na sisi kimasomaso tuingie tuwachomoe hao wamarekani na wanaijeria.

Nawaacha na swali kwa nini wengi ni Waafrika tukizingatia Afrika ni Bara masikini sana....
 
Hahahahahaha..! Hawa jamaa ni wapiga pesa saafi kabisa..! Yaani pesa zao hazipigwi hata kodi! Maana sadaka haikatwi kodi ati.! Daaah natamani na nami niingie kwenye biashara hii ambayo capital yake ni domo lako likichanganywa na communication skills iliyotukuka..!
 
Hahahahahaha..! Hawa jamaa ni wapiga pesa saafi kabisa..! Yaani pesa zao hazipigwi hata kodi! Maana sadaka haikatwi kodi ati.! Daaah natamani na nami niingie kwenye biashara hii ambayo capital yake ni domo lako likichanganywa na communication skills iliyotukuka..!
FANYA HARAKA HUJACHELEWA
 
Tulingia utajiri au tunatakiwa kulingia kukua kwa imani?kweli ukristo umeingiliwa yesu alituusia tuutafute ufalme wa mbinguni na si wa duniani.
Kuringia sio kulingia..
 
Tulingia utajiri au tunatakiwa kulingia kukua kwa imani?kweli ukristo umeingiliwa yesu alituusia tuutafute ufalme wa mbinguni na si wa duniani.
Utajiri sio dhambi, ndio maana mbinguni watu wataisha zaidi ya matajiri hawa tunaowaona, miji ya mbinguni kwa mujibu wa ufunup ni mizuri kuliko hata sebule ya Bill gate mkuu
 
Hahahahahaha..! Hawa jamaa ni wapiga pesa saafi kabisa..! Yaani pesa zao hazipigwi hata kodi! Maana sadaka haikatwi kodi ati.! Daaah natamani na nami niingie kwenye biashara hii ambayo capital yake ni domo lako likichanganywa na communication skills iliyotukuka..!
inahitaji uwe na extraordinary kipaji,
Ukiona watu kumi wanafanikiwa kuingia humo top ten, ujue kuna maelfu kama sio malaki ambao wako benchi na wanavipaji lakini hawafanikiwi. Hawa jamaa wanastahili pongezi. Mungu awazidishie maana sio kazi rahisi ...
 
Nafikiri unatakiwa kujua mifumo ya makanisa na huduma ulizozitaja, established churches kama vile RC, Lutheran nk ni matajiri wakubwa isipokuwa utajiri wao unatajwa kama ni kitaasisi. Hawa wengine wanaotajwa kuwa ni matajiri wakubwa ukweli utajiri wao bado sio wakwao bali ni wa makanisa au huduma zao. Mfumo unawapa nguvu juu ya hizo mali japo sio kwa ajili yao. Fikiri huduma za kijamii anayofanya TB Joshua mfano, ni kubwa kuliko hata zinazofanywa na established churches. Kuna kiwango cha mafanikio ambacho mtu akifikia huwa anachoweza anachomiliki sio kwa ajili yake tena. Self esteemed person
 
Back
Top Bottom