Wachumi tusaidieni hapa

Kuna mtu amegusia kidogo masuala ya currency. Naomba kusaidiwa kitu; Japan ambayo ni moja ya nchi tunazoamini zina nguvu kiuchumi, currency yake wameifanya isiwe kivile? Naomba kuelimishwa

Mkuu kwanza nikusahihishe: Japan kama Tz wanatumia flexible exchange rate regime au floating exchange rate kwa maana kwamba wanaacha soko lipandishe au kushusha thamani ya sarafu yao. Sio kwamba wajapani wamethamanisha fedha yao kwa amri (fixed exchange rate regime).

Lakini sarafu ya Japan ndio sarafu ya tatu duniani kutumika katika biashara za kimataifa. Hii manake ni kwamba nchi kubwa duniani zina akiba ya fedha za Japan kutokana na umuhimu wake katika export. Hata hivyo Japan itapoteza endapo sarafu yake itathaminishwa zaidi na nguvu za soko la dunia, na wanachoweza kufanya wajapani ili likitokea ni kununua dola au sarafu nyingine kwa wingi kutoka kwa nchi kubwa ambazo Japan inaziuzia bidhaa zake, kingine itajaribu kuteremsha interest rate ili sarafu yake iwe nyingi kwenye mzunguko na hivyo kuifanya isipande sana na kuteremka sana kufuatana na soko.
 
Back
Top Bottom