Wachumi tusaidieni hapa

nini faida ya strong currency kwenye uchumi ?
nini faida ya strong currency kwenye uchumi wa nchi isiyo na export za kutosha??
nini faida ya strong currency kwa watu wa taifa husika ambao ni masikini na maisha yao ni pangu pakavu??
tukiwa na stong currency maana yake....value for money inaonekana,welfare ya citizens huonekana,prices zinakuwa relative stable,na vilevile export hapo lazima iwe greater than import ili na balance of payments iwe favourable
 
nashukuru sana kwa nondo zako, naona kama naanza kuelewa uchumi hivi...

sasa mkuu inakuwaje sasa nchi kama tanzania inakuwa masikini wakati kuna hizo principles and rules za uchumi ambazo ukizifuata unatoboa?
wachumi wetu ni vi_laza, sio wazalendo, tatizo nini sasa maana maelezo yako yapo very clear hata kama hujasoma uchumi unaeleweka...
je tunauhakika gani na mbinu zetu za uchumi kwa sasa??
 
tatizo linakuja kwenye Government officials ku-corrupt ,emblezzment of public fund,na politicians ku-entervene.....yani hapo tu mkuu ndo tunakwama...siasa yetu nayo ni tatizo kubwa
 
hiyo inatokana na sababu huwezi ku-equate bidhaa na huduma zilizozalishwa at a certain time na volume ya money circulation, sababu kuu ikiwa ni kuwa kunaweza kuwa na surplus ya bidhaa na huduma au deficit ya bidhaa na huduma.wakati money supplly ipo constant au imeongezeka...hata USA na GREAT BRITAIN wana inflation ila kwa rate ndogo
Asante Sana kwa majibu mubashara nimekuelewa sana.
 
mkuu nashukuru kwa ufafanuzi mzuri, swali langu la kwanza hukulielewa,, lakini sio mbaya ngoja nilitengeneze ulielewe..

upatikanaji wa hela unapokuwa mgumu halafu bei za bidhaa kupaa, - nini hatari yake?
upatikanaji wa hela unapokuwa mgumu halafu bei za bidhaa zisishuke wala kupanda ( zikabaki constant kama amabvyo zilikuwa upatikanaji wa hela ulipokuwa nafuu au hela ilipokuwepo) - nini hatari yake?

Ela ikiwa ngumu kuipata manake bei zitalazimika kuteremka, mfano ukishindwa kuuza nyumba yako utalazimika kupunguza bei ili mwenye ela ashawishike kununua. Kwa maana hiyo lazima bank kuu ijaribu kuwianisha uzalishaji na kiasi cha ela kwenye mzunguko.

Hatimaye bei za bidhaa ambazo hazitaki kuteremka kutokana na upungufu wa fedha LAZIMA zitateremka au kuondolewa kutoka soko moja kwenda sehemu nyingine na huku wazalishaji wakiacha kufanya uzalishaji zaidi. Hivyo overtime biashara ambazo mteremko wa bei unaleta hasara zitajifunga au kutoweka. Bidhaa ambazo ni necessities (za lazima/muhimu Kama chakula afya malazi na mavazi) zitachelewa tu kuteremka bei lakini hatimaye zitateremka au uzalishaji wake kupungua.

Ni vizuri kukumbuka/kutambua kwamba kupanda kwa bei haina maana kwamba ela ni nyingi kuliko uzalishaji kila wakati. Mfumuko wa bei waweza kusababishwa na kukua kwa uchumi (crowd out effects), na mfumuko wa aina hii ni kawaida na ni rahisi ku control. Ni mfumuko unaotokana na ajira nyingi ambazo zinasababisha surplus (kiasi cha fedha za ziada) ambayo inatamanisha wazalishaji kupandisha bei hadi surplus iwe zero.

kinachotokea Tz ni mchanyato wa matatizo, kwanza mzunguko wa fedha kwa maana rahisi ya kiasi cha fedha umepungua, pili uzalishaji umepungua, tatu international donors waliokuwa wanakupa budget support wameghairi, matumizi ya serikali ambayo uenda sambamba na matumizi binafsi kwenye savings na investment yamepungua, private investors ambao wange offset kupungua kwa matumizi ya serikali wame shy away katika maamuzi yao, na kibaya zaidi, IMANI ya wawekezaji wa nje na ndani imepotea kutokana na kodi kandamizi na malalamiko ya consumers kutoka kila kona ya nchi.

Kwa tunavyokwenda miezi ya karibuni kutakuwa na kila dalili na kila kishawishi kwa serikali kuchapisha fedha (borrowing/printing) ili kuupa boost uchumi kwa namna ya kuongeza ela kwenye mzunguko. Hili likitokea basi tutakuwa tumetia sahihi kitabu cha laana cha maulana maana uchumi wetu utakuwa fake kupita bidhaa za mchina.

Twakuomba utusikieeeeee!!
 
tatizo linakuja kwenye Government officials ku-corrupt ,emblezzment of public fund,na politicians ku-entervene.....yani hapo tu mkuu ndo tunakwama...siasa yetu nayo ni tatizo kubwa
Yes! Hapa kwetu inakubidi uiruhusu taaluma yako itawaliwe na siasa ukienda kinyume unatumbuliwa.
 
mkuu leo nitakutesa sana kwa maswali, nisamehe bure tu...

mbona kuna shida kidogo mfano TANZANIA hiki kipindi hela ni ngumu kidogo halafu bei ziko palepale na vitu vingine vimepanda bei... mfano cement bei ipo palepale, unga, sukari bei zimepanda, mabati bei zipo palepale... hii kitaalamu tuiteje??

Kumbuka kuna short term, medium term na long term effects ya kila sera au economic policy. Pia kuna bidhaa ambazo ni price sensitive na price insensitive (wachumi wanaita price elasticity)
 
tukiwa na stong currency maana yake....value for money inaonekana,welfare ya citizens huonekana,prices zinakuwa relative stable,na vilevile export hapo lazima iwe greater than import ili na balance of payments iwe favourable

Wala sio hivyo sana kwa nchi masikini kama Tz.

Strong currency without power to influence international market ni sawa na papa kwenda msikitini au imamu kwenda kanisani.

Na ndio maana Bank ya dunia na International Monetary Fund walitushauri tuache kuyathamanisha madafu kupita uhalisia wake. Wala hawakukosea.
 
Yes! Hapa kwetu inakubidi uiruhusu taaluma yako itawaliwe na siasa ukienda kinyume unatumbuliwa.

Ndiyo raha ya shule na maisha ya mtandaoni.Uchumi halisi ni maisha halisi.Wewe unazalisha na kuuza nini(bidha au huduma) je inahitajika.Unaoshindana nao na bidhaa zako kipi bora Zaidi?
.
Unalenga usaidiwe na mama ,baba,dada na wajomba zako kupata fedha za mahitaji yako ila uwe na uhuru wa kuchagua chakula,nguo,gari na kumbi za kustarehe baada ya kukusanya misaada ya ndugu zako.Hiyo ni shule ya nadharia za kiuchumi kwa mtu hafifu.

Hatuhitaji kwenda darasani tu kuujua uchumi halisi.Nenda kwa Wakinga,Wapare na Waha.Mambo yao mengine waachie wenyewe jifunze nadharia zao za uchumi tu, utaelewa tatizo liko wapi.

Kwa wanaoamini ugenini tu kujifunza nenda China.Jifunze nidhamu yao ya kazi,wanavyokula,aina ya vyakula, wanavyovaa,wapi wananunua bidhaa wanazotumia utapata jibu.Tatizo tumeng'ang'ania nadharia za mtawala.

Nimewahi kufuga Ng'ombe nikiwa na vijana wakunisaidia kazi hiyo.Unategemea ningewafundisha nadharia za kupata mifugo yao wenyewe na namna ya kuwatunza vizuri wangeendelea kunitumikia? nauiliza ili nijue.

Sijabobea kwenye uchumi ila kamwanga ka kunionyesha giza na nuru ninako.Wanaofundisha uchumi wanao wanaouita mnyororo usiokoma wa umaskini.Uwekaji akiba hafifu,mtaji hafifu na uwekezaji hafifu.

Tunauliza nchi tukidhani sisi si sehemu ya nchi.Jiulize kwa unachopata unaweka akiba kiasi gani,umekusanya mtaji kiasi gani,umewekeza wapi? Wengi wetu tumewekeza kwenye simu za bei mbaya,magari ghali ya kutembelea,kwenye pombe na warembo tunalalamika uchumi haukui.

Tujifananishe na jirani zetu wa Kenya aina za simu wanazotumia,magari wanayotembelea,kiasi cha fedha wanazowapa Malaya,tunaweza kujua pa kuanzia.

Wangapi kati yetu tumewasifu wezi na kuwaita wajanja na kuwatukana waaminifu na kuwaita wapumbavu hawajui kutumia nafasi zao.Sisi ni sehemu ya tatizo tukijierekebisha nchi itapaa,tuking'ang'ania miujiza tutaendelea kushangaa.

Tatizo namba moja tunakula kuliko tunavyozalisha.
 
Zipo sehemu nakubaliana nawe na zipo sehemu sikubaliani nawe.

Huwezi kuitoa serikali kwenye maendeleo ya watu kama ambavyo huwezi kuwatoa watu wake kwenye maendeleo yao. Kwa nchi masikini kama Tz, serikali ina sehemu kubwa katika kuleta maendeleo kuliko sehemu ya watu wake katika kuleta maendeleo. Hivyo basi tunaposhindwa kuendelea tuna kila sababu ya kuhoji serikali maana kupitia serikali ndio tumeweka social contract zinazo define maendeleo yetu na namna ya kuyafikia.

Mimi nasema kinyume cha ulichosema, kwamba serikali yetu ikifanya kile au yale yanatogemewa nchi itapaa. Serikali ikiwa inasikiliza vipaumbele vya watu wake badala ya watu kuisikiliza serikali nchi itapaa. Nakubali mfano wako wa watu kununua simu ya bei mbaya kuliko kuwekeza, ila ningekuomba uutumie mfano huo huo kutueleza kwanini serikali imenunua ndege na inaendelea kununua ndege badala ya kuwekeza kwenye elimu au ajira! Labda tabia zetu ni mwongozo wa tabia za viongozi wetu ambazo kwa ujumla wake hazina tija kwetu. Kama ndivyo basi viongozi na wawe wakwanza kubadirika.
 
Kuna mtu amegusia kidogo masuala ya currency. Naomba kusaidiwa kitu; Japan ambayo ni moja ya nchi tunazoamini zina nguvu kiuchumi, currency yake wameifanya isiwe kivile? Naomba kuelimishwa
 
tukiwa na stong currency maana yake....value for money inaonekana,welfare ya citizens huonekana,prices zinakuwa relative stable,na vilevile export hapo lazima iwe greater than import ili na balance of payments iwe favourable
Hasa nikizingatia kuwa Japan inaexport kwelikweli
 
Ela ikiwa ngumu kuipata manake bei zitalazimika kuteremka, mfano ukishindwa kuuza nyumba yako utalazimika kupunguza bei ili mwenye ela ashawishike kununua. Kwa maana hiyo lazima bank kuu ijaribu kuwianisha uzalishaji na kiasi cha ela kwenye mzunguko.

Hatimaye bei za bidhaa ambazo hazitaki kuteremka kutokana na upungufu wa fedha LAZIMA zitateremka au kuondolewa kutoka soko moja kwenda sehemu nyingine na huku wazalishaji wakiacha kufanya uzalishaji zaidi. Hivyo overtime biashara ambazo mteremko wa bei unaleta hasara zitajifunga au kutoweka. Bidhaa ambazo ni necessities (za lazima/muhimu Kama chakula afya malazi na mavazi) zitachelewa tu kuteremka bei lakini hatimaye zitateremka au uzalishaji wake kupungua.

Ni vizuri kukumbuka/kutambua kwamba kupanda kwa bei haina maana kwamba ela ni nyingi kuliko uzalishaji kila wakati. Mfumuko wa bei waweza kusababishwa na kukua kwa uchumi (crowd out effects), na mfumuko wa aina hii ni kawaida na ni rahisi ku control. Ni mfumuko unaotokana na ajira nyingi ambazo zinasababisha surplus (kiasi cha fedha za ziada) ambayo inatamanisha wazalishaji kupandisha bei hadi surplus iwe zero.

kinachotokea Tz ni mchanyato wa matatizo, kwanza mzunguko wa fedha kwa maana rahisi ya kiasi cha fedha umepungua, pili uzalishaji umepungua, tatu international donors waliokuwa wanakupa budget support wameghairi, matumizi ya serikali ambayo uenda sambamba na matumizi binafsi kwenye savings na investment yamepungua, private investors ambao wange offset kupungua kwa matumizi ya serikali wame shy away katika maamuzi yao, na kibaya zaidi, IMANI ya wawekezaji wa nje na ndani imepotea kutokana na kodi kandamizi na malalamiko ya consumers kutoka kila kona ya nchi.

Kwa tunavyokwenda miezi ya karibuni kutakuwa na kila dalili na kila kishawishi kwa serikali kuchapisha fedha (borrowing/printing) ili kuupa boost uchumi kwa namna ya kuongeza ela kwenye mzunguko. Hili likitokea basi tutakuwa tumetia sahihi kitabu cha laana cha maulana maana uchumi wetu utakuwa fake kupita bidhaa za mchina.

Twakuomba utusikieeeeee!!
Duuuuh.. Kwa hyo ile hali ya Zimbabwe inainyemelea tz yangu?
 
M
Zipo sehemu nakubaliana nawe na zipo sehemu sikubaliani nawe.

Huwezi kuitoa serikali kwenye maendeleo ya watu kama ambavyo huwezi kuwatoa watu wake kwenye maendeleo yao. Kwa nchi masikini kama Tz, serikali ina sehemu kubwa katika kuleta maendeleo kuliko sehemu ya watu wake katika kuleta maendeleo. Hivyo basi tunaposhindwa kuendelea tuna kila sababu ya kuhoji serikali maana kupitia serikali ndio tumeweka social contract zinazo define maendeleo yetu na namna ya kuyafikia.

Mimi nasema kinyume cha ulichosema, kwamba serikali yetu ikifanya kile au yale yanatogemewa nchi itapaa. Serikali ikiwa inasikiliza vipaumbele vya watu wake badala ya watu kuisikiliza serikali nchi itapaa. Nakubali mfano wako wa watu kununua simu ya bei mbaya kuliko kuwekeza, ila ningekuomba uutumie mfano huo huo kutueleza kwanini serikali imenunua ndege na inaendelea kununua ndege badala ya kuwekeza kwenye elimu au ajira! Labda tabia zetu ni mwongozo wa tabia za viongozi wetu ambazo kwa ujumla wake hazina tija kwetu. Kama ndivyo basi viongozi na wawe wakwanza kubadirika.

Mjadala wenye tija ni hoja kuondolewa kwa hoja,mijadala ya dhihaka hujibiwa kwa dhihaka.Umekuja kwa hoja nitakujibu kwa hoja.Serikali ingenunua ndege za kutembelea viongozi ningeona ni upuuzi.Tunataka kuondoka kwenye ujinga wa kutegemea sigara na pombe kama vyanzo pekee vya mapato kupitia utalii.Ni rahisi kuwavutia watalii kwa kuwahakikishia usalama wao,usafiri wa uhakika,malazi na vivutio vingine.

Unaweza kuwekeza nje ya utalii.Unapaswa kulinganisha kipi kitangulie na kipi kifuate.Kwenye kilimo unahitaji fedha nyingi Zaidi,muda mrefu Zaidi wa kurejesha gharama ulizoekeza,wigo mpana wa wawekezaji na umakini mkubwa Zaidi wa kuwekeza.

Huhitaji kuanzisha vivutio vipya vya utalii bali unahitaji kutunza tu vilivyopo,kuimarisha mapokezi na kutangaza ulivyo navyo.Ndege ni uwekezaji kwa ajili ya kuwaleta watalii tunaowahitaji.

Tuna changamoto za kuzitatua zisizohitaji serikali tu.Nitaitaja moja.Watalii wakija hawahitaji kuona wanyama tu wasiokuwepo kwao.Wanataka kuona tunakula nini,tuna vaa nini,muziki wetu upoje.Tembelea hoteli zetu zinazo wapokea uone aina ya vyakula,lugha zinazotumika,mavazi ya wanaowapokea na muziki tunaowawekea.Vitu hivi vinathibitisha matumizi yetu ya akili. Pima haya kwa kutembelea Mombasa tu kwa jirani zetu.Aibu hii inafichwa kidogo na ndugu zetu wa Zanzibar kupitia staha ya mavazi yao,sema yao,muziki wao ila sina uhakika na chakula wanachowashawishi wageni wale.Tunawapa vitu vilivyowachosha kwao.

Nimeonyesha umuhimu wa ndege na nini sisi kama raia tunaweza kufaidi na kuchangia kukua kwa utalii.Onyesha eneo ambalo unaamini kuwa serikali inaweza kuondoa kasoro zake na kukuza uchumi wa watu wake.

Kuongeza thamani ya mazao ni wajibu wetu raia si Serikali.Serikali tuitake ipunguze kodi kwenye nyenzo za kuongezea thamani mazao yetu,iwatie moyo na kuwasaidia watengenezaji wa bidhaa waliopo hata kama wanatengeneza silaha.Badala ya kuwafunga tuwaunganishe na vyombo vyetu vya ulinzi ili wanachofanya kiwe siri yetu wenyewe badala ya kuwakatisha tamaa na kutegemea silaha zote kutoka ugenini.

Tuitake Serikali yetu kutoingia katika mikataba ya kipuuzi kama mmoja uliopo jamvini kuhusiana na udhibiti wa mbegu ili tu tununue mbegu za wazungu. Kuingia mikataba ya kutaka wakulima wote wanunue mbegu zinazozalishwa na kampuni za kigeni na kuigeuza haramu kisheria usambazaji wa mbegu za kwetu ni utumwa halisi.Haya ni baadhi ya maeneo ya kuyapigia kelele.

Tunapaswa kuzalisha bidhaa wanazozihitaji wazungu na wasizoweza kutupangia bei.Nitataja eneo moja tulilolipuuza kwa upumbavu na si ujinga wetu.Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili. Dunia nzima tunayoiita ya kwanza wanataka mazao yaliyotokana na kilimo hai,kuifanya ngeni na ya kisasa wameipa jina tu la kigeni"organic farming" na kwa kuwa wataalam wetu wengi wao wamefundishwa kukariri na siyo kufikiri huichukulia hii kama njia isiyo lipa.

Hatujiulizi kwa nini ngozi nyeupe haitaki mboga mboga na matunda yaliyozalishwa kwa mbolea zao na viatilifu vyao.Kwa mnaotaka ushahidi fuatilieni na mlete mrejesho kwa nini hoteli kubwa zilizopo Tanzania hununua mboga mboga na matunda nje ya Tanzania.Fuatilieni na mjue kwa bidhaa hizo wanazonunua Tanzania masharti yao ni yapi.

Tunahitaji kufikiri na kuamua cha kufanya na si kulalamika.Tulionywa kuwa tusikubali wengine wafikiri kwa niaba yetu.

Kazi kubwa ya serikali ni kujenga mazingira rafiki kwa shughuli za kiuchumi.Pamoja na mapungufu mengi ya Serikali yapo mambo makubwa mazuri sana yamefanywa.Nikiangalia mtandao wa barabara zetu, na tukafufua reli zetu zote hatutakuwa na haki ya kulalamika.

Kama unaweza kuzalisha bidhaa Mtwara na ukaiuza Tanga,Ukazalisha bidhaa Kigoma na ukaifikisha kirahisi Dar na huna unachozalisha utakuwa umechagua kushindwa na kutegemea serikali ikusaidie kuendelea.
 
bado napata shida sana na uchumi wetu kama hatutaongeza export, tuongeze uzalishaji wa ndani na kuuza sana mazao yetu nje kwa maana ya kuwekeza sana kwenye kilimo kwa kuwezesha wakulima wadogo, wakati na wakubwa, tujitahidi sana kudhibiti dhahabu yetu na madini yetu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wakubwa ikiwezekana mnunuzi awe serikali kwa hawa wachimbaji wadogo na hapo serikali itayakusanya na kuexport na sio kuwaacha wachina, wahindi na wakenya kihorera ...
 
Kuna hii hali kidogo inachanganya sana kwangu na kwa watu wengine bila shaka, WATAALAMU WA UCHUMI TUNAOMBA MTUSAIDIE HAPA TAFADHALI;

1. Hela inapokuwa ngumu halafu bei za vitu zinapanda au kubakia palepale wakati upatikanaji wa hela ukiwa na unafuu - hii inaashiria nini na nini tafsiri yake??.

2. Mzunguko wa hela unapokuwa mdogo - nini athari za kiuchumi kwa wananchi husika??..

3. Kipi kifanyanyike taifa na wananchi wake wawe na uchumi bora na wenye nguvu??

4. Nini msingi wa uchumi wenye nguvu utakaodumu kwa miaka zaidi ya 100??.

Nini madhara ya kujenga ghorofa kwenye mchanga? Ukipata jibu la hilo swali utaelewa uchumi ulikuwaje huko nyuma na nini kinaendelea sasa hivi?
 
Back
Top Bottom