Wachumi tusaidieni hapa

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Kuna hii hali kidogo inachanganya sana kwangu na kwa watu wengine bila shaka, WATAALAMU WA UCHUMI TUNAOMBA MTUSAIDIE HAPA TAFADHALI;

1. Hela inapokuwa ngumu halafu bei za vitu zinapanda au kubakia palepale wakati upatikanaji wa hela ukiwa na unafuu - hii inaashiria nini na nini tafsiri yake??.

2. Mzunguko wa hela unapokuwa mdogo - nini athari za kiuchumi kwa wananchi husika??..

3. Kipi kifanyanyike taifa na wananchi wake wawe na uchumi bora na wenye nguvu??

4. Nini msingi wa uchumi wenye nguvu utakaodumu kwa miaka zaidi ya 100??.
 
Ukback255

Senior Member
Aug 31, 2016
175
500
Continues rise in price of Goods with no ability of purchasing power of the people no suppy with availability of stock in the industries this cause declaration of industries and unemployment of the people......

Ohhh my God help us.......
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Majibu ya maswali yote ni = SERA MBOVU YA UCHUMI KATIKA NCHI HUSIKA MADHARA YAKE NI MAKUBWA SANA.

Hata siku moja siasa haiwezi kuitawala uchumi na uchumi haiwezi kuitawala siasa they are depends on each other. ILA kwakua wachumi wabobezi wapo busy kuwafungia watu mageti Buguruni Chama na Mwl aliekariri formula za sodium bicarbonate ameshakua mmahiri katika kama Adam Smith kwenye uchumi No body care.
 
MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,309
2,000
Kuna hii hali kidogo inachanganya sana kwangu na kwa watu wengine bila shaka, WATAALAMU WA UCHUMI TUNAOMBA MTUSAIDIE HAPA TAFADHALI;

1. Hela inapokuwa ngumu halafu bei za vitu zinapanda au kubakia palepale wakati upatikanaji wa hela ukiwa na unafuu - hii inaashiria nini na nini tafsiri yake??.

2. Mzunguko wa hela unapokuwa mdogo - nini athari za kiuchumi kwa wananchi husika??..

3. Kipi kifanyanyike taifa na wananchi wake wawe na uchumi bora na wenye nguvu??

4. Nini msingi wa uchumi wenye nguvu utakaodumu kwa miaka zaidi ya 100??.

Mkuu, swali lako # 1 umejichanganya, liandike upya. Kwanza unasema ela imekuwa ngumu na wakati huo huo unasema upatikanaji wake una nafuu! Msingi wa swali lako unakidhana hivyo fafanua.

Swali lako # 2 linajibika kwa ufupi kama ifuatavyo. Mzunguko wa ela (ambao hapa nitarahisisha kwa kuwianisha kiasi cha fedha) unapopungua kunatokea na mambo makubwa mawili kwenye uchumi. Moja, kama uzalishaji hautabadirika sambamba na upungufu wa fedha basi kutakuwa deflation (yaani bei za bizaa zitashuka), baada ya muda wazalishaji nao watapunguza uzalishaji na wanunuzi watalazimika kupunguza manunuzi na matokeo yake kutakuwa na depression au recession (kuanguka kwa uchumi). Kwa maana nyingine ili hili lisitokee kiasi cha ela kwenye mzunguko lazima kiwiane na ongezeko la uzalishaji. Pili, ela ikipungua pasipo kuwiana na uzalishaji riba inaongezeka, hii inasababisha watu wakimbizie ela zao bank na wakopaji kuzikimbia bank zinazokopesha na matokeo yake uzalishaji mpya unapungua, ajira zinapungua, na umasikini unachukuwa nafasi yake. Dawa ni kuwianisha kiasi cha fedha kwenye mzunguko na ongezeko la uzalishaji, hii ni kazi ya BoT.

Swali lako # 3 na # 4 ni maswali yanayohitaji vitabu kwa vitabu kuyajibu hayo. Kuna waandishi wengi wameandika mengi na bado kitendawili cha kuendelea kwa nchi hakijapata ufumbuzi kwa nchi masikini kama Tz. Hata hivyo haina maana kwamba kama nchi hakuna tunachoweza kufanya tukapunguza umasikini, na moja ya tunayoweza kufanya ni kuhakikisha viongozi wetu wanatusikiliza badala ya wao kutaka tuwasikilize.
 
Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Kuna hii hali kidogo inachanganya sana kwangu na kwa watu wengine bila shaka, WATAALAMU WA UCHUMI TUNAOMBA MTUSAIDIE HAPA TAFADHALI;

1. Hela inapokuwa ngumu halafu bei za vitu zinapanda au kubakia palepale wakati upatikanaji wa hela ukiwa na unafuu - hii inaashiria nini na nini tafsiri yake??.

2. Mzunguko wa hela unapokuwa mdogo - nini athari za kiuchumi kwa wananchi husika??..

3. Kipi kifanyanyike taifa na wananchi wake wawe na uchumi bora na wenye nguvu??

4. Nini msingi wa uchumi wenye nguvu utakaodumu kwa miaka zaidi ya 100??.Hii single imechuja baada ya wananchi kuwapuuza na propaganda zenu za mabasi kukosa abiria
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Mkuu, swali lako # 1 umejichanganya, liandike upya. Kwanza unasema ela imekuwa ngumu na wakati huo huo unasema upatikanaji wake una nafuu! Msingi wa swali lako unakidhana hivyo fafanua.

Swali lako # 2 linajibika kwa ufupi kama ifuatavyo. Mzunguko wa ela (ambao hapa nitarahisisha kwa kuwianisha kiasi cha fedha) unapopungua kunatokea na mambo makubwa mawili kwenye uchumi. Moja, kama uzalishaji hautabadirika sambamba na upungufu wa fedha basi kutakuwa deflation (yaani bei za bizaa zitashuka), baada ya muda wazalishaji nao watapunguza uzalishaji na wanunuzi watalazimika kupunguza manunuzi na matokeo yake kutakuwa na depression au recession (kuanguka kwa uchumi). Kwa maana nyingine ili hili lisitokee kiasi cha ela kwenye mzunguko lazima kiwiane na ongezeko la uzalishaji. Pili, ela ikipungua pasipo kuwiana na uzalishaji riba inaongezeka, hii inasababisha watu wakimbizie ela zao bank na wakopaji kuzikimbia bank zinazokopesha na matokeo yake uzalishaji mpya unapungua, ajira zinapungua, na umasikini unachukuwa nafasi yake. Dawa ni kuwianisha kiasi cha fedha kwenye mzunguko na ongezeko la uzalishaji, hii ni kazi ya BoT.

Swali lako # 3 na # 4 ni maswali yanayohitaji vitabu kwa vitabu kuyajibu hayo. Kuna waandishi wengi wameandika mengi na bado kitendawili cha kuendelea kwa nchi hakijapata ufumbuzi kwa nchi masikini kama Tz. Hata hivyo haina maana kwamba kama nchi hakuna tunachoweza kufanya tukapunguza umasikini, na moja ya tunayoweza kufanya ni kuhakikisha viongozi wetu wanatusikiliza badala ya wao kutaka tuwasikilize.
mkuu nashukuru kwa ufafanuzi mzuri, swali langu la kwanza hukulielewa,, lakini sio mbaya ngoja nilitengeneze ulielewe..

upatikanaji wa hela unapokuwa mgumu halafu bei za bidhaa kupaa, - nini hatari yake?
upatikanaji wa hela unapokuwa mgumu halafu bei za bidhaa zisishuke wala kupanda ( zikabaki constant kama amabvyo zilikuwa upatikanaji wa hela ulipokuwa nafuu au hela ilipokuwepo) - nini hatari yake?
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Hii single imechuja baada ya wananchi kuwapuuza na propaganda zenu za mabasi kukosa abiria
usiwaze sana siasa brother ni vizuri ukakuza maarifa kidogo,,..
halafu sio kila anaewaza tofauti na wewe basi atakuwa pia upande tofauti na wewe...

taifa la tanzania ni masikini toka 1961 mpaka leo, ukiwa na akili timamu huwezi kufurahia umasikini huu, jitahidi hata pale unapoweza kushauri basi ukashauri pia kwa manufaa ya TANZANIA sio CDM wala CCM..
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Continues rise in price of Goods with no ability of purchasing power of the people no suppy with availability of stock in the industries this cause declaration of industries and unemployment of the people......

Ohhh my God help us.......
Mkuu sio mbaya ukatafsiri kwa lugha yetu pendwa na Mama aka KISHWAHILI, ili wote wakuelewe . siunajua tena brother hii lugha ya MZUNGU...
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
Majibu ya maswali yote ni = SERA MBOVU YA UCHUMI KATIKA NCHI HUSIKA MADHARA YAKE NI MAKUBWA SANA.

Hata siku moja siasa haiwezi kuitawala uchumi na uchumi haiwezi kuitawala siasa they are depends on each other. ILA kwakua wachumi wabobezi wapo busy kuwafungia watu mageti Buguruni Chama na Mwl aliekariri formula za sodium bicarbonate ameshakua mmahiri katika kama Adam Smith kwenye uchumi No body care.
hiyo nchi husika ifanyeje sasa, ili madhara yasiwe makubwa na mwisho wasiku isiendelee kuwa taifa masikini??
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,528
2,000
kawaida money supply ni lazima iwe sawa na amount ya goods and services in the economy ili currency iwe strong.....ila fedha ikiwa nyingi ktk mzunguko na bidhaa na huduma zikiwa chache lazima kutokee inflation(mfumuko wa bei)....vilevile fedha ikiwa chache ktk mzunguko na huduma na bidhaa zikawa nyingi hutokea deflation(mporomoko wa bei) kwa hyo ni lazima
money supply= amount of goods and services in the economy.....na hakuna nchi yoyote dunian inayoweza ku-balance hyo equation, mfumuko wa bei hutofautiana baina ya nchi na nchi
 
je inakuwaje sasa kama fedha ikiwa chache katika mzunguko halafu huduma na bidhaa zikawa nyingi na kukawa hakuna hiyo deflation ( yaani namaanisha hela hamna halafu bei ziko juu au zinafanana na wakati hela ikiwepo nyingi??)...
 
nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
4,193

Akisoma hii nondo hapa atakuelewa vizuri sana.

Sasa naomba na mimi nipate elimu kidogo, je! Ni kitu gani kinachosababisha hiyo equation hapo juu isiweze kubalance katika nchi husiku wakati uchumi unaendeshwa kwa principle zake?
 
nini faida ya strong currency kwenye uchumi ?
nini faida ya strong currency kwenye uchumi wa nchi isiyo na export za kutosha??
nini faida ya strong currency kwa watu wa taifa husika ambao ni masikini na maisha yao ni pangu pakavu??
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,528
2,000
je inakuwaje sasa kama fedha ikiwa chache katika mzunguko halafu huduma na bidhaa zikawa nyingi na kukawa hakuna hiyo deflation ( yaani namaanisha hela hamna halafu bei ziko juu au zinafanana na wakati hela ikiwepo nyingi??)...
under ceter peribus=everything remain constsnt,hiyo kitu ndiyo ina-apply ......haiwezi kuwa hivyo mkuu....hiyo itakuwa sio economics maana automatically hela zikiwa hamna producers lazima wapunguze price ya bidhaa na huduma....
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,819
2,000
under ceter peribus=everything remain constsnt,hiyo kitu ndiyo ina-apply ......haiwezi kuwa hivyo mkuu....hiyo itakuwa sio economics maana automatically hela zikiwa hamna producers lazima wapunguze price ya bidhaa na huduma....
mkuu leo nitakutesa sana kwa maswali, nisamehe bure tu...

mbona kuna shida kidogo mfano TANZANIA hiki kipindi hela ni ngumu kidogo halafu bei ziko palepale na vitu vingine vimepanda bei... mfano cement bei ipo palepale, unga, sukari bei zimepanda, mabati bei zipo palepale... hii kitaalamu tuiteje??
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,528
2,000
Akisoma hii nondo hapa atakuelewa vizuri sana.

Sasa naomba na mimi nipate elimu kidogo, je! Ni kitu gani kinachosababisha hiyo equation hapo juu isiweze kubalance katika nchi husiku wakati uchumi unaendeshwa kwa principle zake?
hiyo inatokana na sababu huwezi ku-equate bidhaa na huduma zilizozalishwa at a certain time na volume ya money circulation, sababu kuu ikiwa ni kuwa kunaweza kuwa na surplus ya bidhaa na huduma au deficit ya bidhaa na huduma.wakati money supplly ipo constant au imeongezeka...hata USA na GREAT BRITAIN wana inflation ila kwa rate ndogo
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,528
2,000
mkuu leo nitakutesa sana kwa maswali, nisamehe bure tu...

mbona kuna shida kidogo mfano TANZANIA hiki kipindi hela ni ngumu kidogo halafu bei ziko palepale na vitu vingine vimepanda bei... mfano cement bei ipo palepale, unga, sukari bei zimepanda, mabati bei zipo palepale... hii kitaalamu tuiteje??
mkuu leo nitakutesa sana kwa maswali, nisamehe bure tu...

yani hapo kuna measures za ku-control inflation ndo zinatumika wakati huu....ambazo ni (contractionary monetary and physical policies)...hiz monetary zinakuwa-implemented na BOT wakati hizo physical policy serikali ndo wanazisimamia....BOT wanachofanya ni kuzinyima mikopo kwa kuweka rate kubwa kwa benki za kawaida na ,kuongeza kiwango cha reserve requirement,Open market Operation,etc na serikali inapunguza matumizi ambayo ni capita expenditure na recurrent expenditure na kuuza,treasury bills,bonds,etc automatically hela inavopungua kwenye mzunguko na wazalishaji hupunguza gharama za uzalishaji...na gharama za uzalishaji zikipungua moja kwa moja bei ya bidhaa na huduma hupungua...japokuwa PRICE INDICES inatueleza kuwa baada ya muda fulani bei ya huduma na bidhaa huongezeka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom