Wachumi na Wanasiasa Tusaidieni Tanzania Ilifikia Wapi ?

DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
500
Kwa kifupi sana wana Jf kila siku Mtaani kwangu na Kauli kutoka kwa baadhi ya viongozi ninasikia wanasema Nchi ilifikia pabaya ,mara kwa tulipokuwa tumefikia Tulihitaji Mtu kama JPM ,mara Tanzania ilikuwa Shamba la bibi

Swali Wanauchumi tujuzeni sisi tusioelewa Tanzania tulifikia PABAYA au PAZURI ? Maana Toka awamu ya nne iko Madarakani tunaambiwa na Taasisi za kimataifa Uchumi wetu Unakua kwa kasi hata report ya Mwisho Ya IMF ilionyesha uchumi wetu unakua kwa 7.1% na inakadiliwa kuwa nchi itakayokua zaidi kiuchumi ukiacha Ivory coast .

Naombeni Maelezo .wanasiasa mnaposema ilifika pabaya mnamaana gani ?
 
gundogan

Member
Nov 7, 2015
26
45
kwa mawazo yangu naona kuna vitu viwili twaweza changanya. kuna uchumi kukua na uchumi kuendelea, kwa lugha iliyopanda ndege twasema( economic growth na economic development), mwananchi mmoja mmoja ananufaika pale uchumi unapoendelea na sio uchumi kukua. uchumi ili uendelee unaitaji shughuli za wananchi katika kukuza pato la ndan(GDP). ila tunaweza kukuza uchumi kwa kuwa na wawekezaji wakutoka nchi za nje na kuzalisha ndan ya nchi ila nchi ikanufaika kwa asilimia ndogo ukilinganisha na asilimia kubwa wanazopeleka katika nchi zao. serikali inatakiwa iwainue wazawa katika kuwekeza ndan na nje ya nchi ili tuzidishe exportation na sio importation. natumai ntakuwa nmeeleweka. samahan kwa typing error
 
MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,320
2,000
Washabiki wakisiasa watakuambia nchi ilifikia pabaya! Hao hawajui wanachoongea na wala hawana idea ya kukua kwa uchumi na maendeleo ya watu. Uchumi wetu ulikuwa kufikia hizo asilimia na tulikuwa tunashangiliwa kila kona ya dunia. Tatizo tulilokuwa nalo ni tatizo la kila sehemu Africa: Rushwa na kushindwa kwa kukua kwa uchumi wetu kuhakisi maendeleo yetu.

Tunachoshuhudia sasa ni sera za kugawana pato la taifa kuliko kuzalisha. Kodi tunazozitunga kila kukicha na kuwavalia manyanga wafanyabiashara hazilengi katika uzalishaji bali ugawaji wa pato la taifa kwa njia ya huduma na miundombinu. Kwa sera hizi sasa tunaweza kupaaza sauti na kusema zinaumiza uchumi na hivyo maendeleo yetu.

Investment ambayo ndio uzalishaji inapunguzwa kwa kodi kupitia kitu wachumi wanaita marginal propensity to savings (sent kadhaa zinazotengwa kwa investment kwa kila shilingi unayoipata kama mshahara au faida kutoka katika biashara). Nchi za wenzetu kodi kamwe sio ubabe na wala sio kitu kinachotengeneza vita kati ya wafanyabiashara na serikali Kama inavyoashiria sasa Tz. Maana unafuu wa kodi unaongeza investment/uzalishaji na nyongeza ya kodi inaumiza uzalishaji. Hapa swala la kodi kwa maana hii lazima liangaliwe kama panga ikatayo kuwili.

Ukusanyaji wa kodi kwa uwingi wala sio jambo la kushangiliwa hata siku moja. Wala hakuna uongozi duniani unaopimwa kwa kiwango cha kodi. Very simple, kodi ni kama bima, kadri unapokusanya bima nyingi ndipo unapotakiwa kujiandaa kulipa fidia kubwa maana umechukuwa risk ambayo mlaji wa bima ingemfanya arekebishe tabia na hivyo kujiepusha na madhara tarajiwa. Vivyo hivyo kodi, kadri serikali inapolazimisha watu walipe malimbikizo ya kodi ya awamu iliyopita ndipo inaponyang'anya wafanyabiasha mitaji na ndipo serikali itakapojikuta ikiingia gharama ya kuijenga upya sekta binafsi na ya umma. Wakati hili linafanyika uzalishaji unapungua na uchumi unaangukia pua.

Tatizo, narudia, serikali ya awamu hii imejikita katika kuhakikisha biashara inafuata sheria na kodi inalipwa huku wala rushwa wakidhibitiwa. Haya yote ni mambo mazuri na wazalendo tunatakiwa kuyapongeza na kuunga mkono kila hatua. Tatizo ni kwamba mambo haya yamekuwa substitute ya dhana mzima ya uzalishaji. Tumeacha kuangalia namna ya kuongeza uzalishaji na badala yake tumejikita kwenye income distribution na equalization schemes kana kwamba tunazalisha vyakutosha.

Nilidhani magazeti yangekuwa yanaandika namna tunavyopiga hatua katika kutatua tatizo la ajira. Sera ya viwanda sasa inapotea masikioni mwa umma badala yake mahakama ya mafisadi na vita vya shisha na ushoga vimepamba moto. Vita vya kupambana na rushwa ndio imekuwa ndio habari za asubuhi, mchana, na jioni! Habari za kupungua meli za mizigo bandarini na namna ya kuongeza, habari za watalii kuacha kuja kutokana na kodi, habari za wachimbaji gas kufungasha virago na namna tunavyojipanga kuwarudisha, habari za kusitisha ajira serikalini na mikakati ya kuzirejesha haraka, habari za kupanda kwa bei ya sukari na ukosefu wa nishati ya mafuta, habari ya mabenki kusitisha kutoa mikopo na badala yake kuhakikisha wadeni wake wanalipa haraka nk hazionekani kuwa vipaumbele katika uzalishaji.

Nchi inahitaji kuamka na kuanza kutilia mkazo uzalishaji kwanza kabla ya ugawanaji. Msisitizo wa ulipaji kodi, vita dhdi ya rushwa na ufuatwaji wa sheria lazima visindikize lengo kuu la kuongeza uzalishaji. Sidhani kama tunataka kujenga uchumi usio na wala rushwa, wakwepa kodi, na watiifu wa sheria ambao wamo kwenye nchi yenye kiwango kidogo cha uzalishaji. Sidhani kwamba tupo tayari uzalishaji upungue ili mradi tu sera za uagawanaji na ufuataji sheria zinazingatiwa. Kwasababu, lazima kwanza kuwe na uzalishaji ndipo hayo mengine yawepo na kurekebishwa.

Nchi ilifika pabaya kiuchumi? Jibu hapana! Je sasa iko pabaya? Jibu, tunaelekea kubaya sana, na jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza uzalishaji.
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,774
2,000
Kwa kifupi sana wana Jf kila siku Mtaani kwangu na Kauli kutoka kwa baadhi ya viongozi ninasikia wanasema Nchi ilifikia pabaya ,mara kwa tulipokuwa tumefikia Tulihitaji Mtu kama JPM ,mara Tanzania ilikuwa Shamba la bibi

Swali Wanauchumi tujuzeni sisi tusioelewa Tanzania tulifikia PABAYA au PAZURI ? Maana Toka awamu ya nne iko Madarakani tunaambiwa na Taasisi za kimataifa Uchumi wetu Unakua kwa kasi hata report ya Mwisho Ya IMF ilionyesha uchumi wetu unakua kwa 7.1% na inakadiliwa kuwa nchi itakayokua zaidi kiuchumi ukiacha Ivory coast .

Naombeni Maelezo .wanasiasa mnaposema ilifika pabaya mnamaana gani ?
wengi ni washabiki na chuki tu. wala hawajui chochote. Ukuaji wa uchumi kipindi cha Kikwete hautotofautiana na wa Magufuli. time will tell.
 
Mkwawabongo

Senior Member
Jul 28, 2015
154
225
Mkuu uneongea ukweli Kama mchumi na sidhani Kama level uliochambua ni ya mtu mwenye degree za Tanzania....Watanzania wanashabikia ujinga lakini ikianza kuwachoma inavyotakiwa ndio watatumia akili kufikiria....Kitu Magufuli anafanya ni Uongozi wa mwaka 1967 Kama mentor wake Nyerere...Alafu anatumia ujinga wa watanzania dhidi yao, ukicriticise unaitwa Polisi kuhojiwa ambayo ni ujinga.
Washabiki wakisiasa watakuambia nchi ilifikia pabaya! Hao hawajui wanachoongea na wala hawana idea ya kukua kwa uchumi na maendeleo ya watu. Uchumi wetu ulikuwa kufikia hizo asilimia na tulikuwa tunashangiliwa kila kona ya dunia. Tatizo tulilokuwa nalo ni tatizo la kila sehemu Africa: Rushwa na kushindwa kwa kukua kwa uchumi wetu kuhakisi maendeleo yetu.

Tunachoshuhudia sasa ni sera za kugawana pato la taifa kuliko kuzalisha. Kodi tunazozitunga kila kukicha na kuwavalia manyanga wafanyabiashara hazilengi katika uzalishaji bali ugawaji wa pato la taifa kwa njia ya huduma na miundombinu. Kwa sera hizi sasa tunaweza kupaaza sauti na kusema zinaumiza uchumi na hivyo maendeleo yetu.

Investment ambayo ndio uzalishaji inapunguzwa kwa kodi kupitia kitu wachumi wanaita marginal propensity to savings (sent kadhaa zinazotengwa kwa investment kwa kila shilingi unayoipata kama mshahara au faida kutoka katika biashara). Nchi za wenzetu kodi kamwe sio ubabe na wala sio kitu kinachotengeneza vita kati ya wafanyabiashara na serikali Kama inavyoashiria sasa Tz. Maana unafuu wa kodi unaongeza investment/uzalishaji na nyongeza ya kodi inaumiza uzalishaji. Hapa swala la kodi kwa maana hii lazima liangaliwe kama panga ikatayo kuwili.

Ukusanyaji wa kodi kwa uwingi wala sio jambo la kushangiliwa hata siku moja. Wala hakuna uongozi duniani unaopimwa kwa kiwango cha kodi. Very simple, kodi ni kama bima, kadri unapokusanya bima nyingi ndipo unapotakiwa kujiandaa kulipa fidia kubwa maana umechukuwa risk ambayo mlaji wa bima ingemfanya arekebishe tabia na hivyo kujiepusha na madhara tarajiwa. Vivyo hivyo kodi, kadri serikali inapolazimisha watu walipe malimbikizo ya kodi ya awamu iliyopita ndipo inaponyang'anya wafanyabiasha mitaji na ndipo serikali itakapojikuta ikiingia gharama ya kuijenga upya sekta binafsi na ya umma. Wakati hili linafanyika uzalishaji unapungua na uchumi unaangukia pua.

Tatizo, narudia, serikali ya awamu hii imejikita katika kuhakikisha biashara inafuata sheria na kodi inalipwa huku wala rushwa wakidhibitiwa. Haya yote ni mambo mazuri na wazalendo tunatakiwa kuyapongeza na kuunga mkono kila hatua. Tatizo ni kwamba mambo haya yamekuwa substitute ya dhana mzima ya uzalishaji. Tumeacha kuangalia namna ya kuongeza uzalishaji na badala yake tumejikita kwenye income distribution na equalization schemes kana kwamba tunazalisha vyakutosha.

Nilidhani magazeti yangekuwa yanaandika namna tunavyopiga hatua katika kutatua tatizo la ajira. Sera ya viwanda sasa inapotea masikioni mwa umma badala yake mahakama ya mafisadi na vita vya shisha na ushoga vimepamba moto. Vita vya kupambana na rushwa ndio imekuwa ndio habari za asubuhi, mchana, na jioni! Habari za kupungua meli za mizigo bandarini na namna ya kuongeza, habari za watalii kuacha kuja kutokana na kodi, habari za wachimbaji gas kufungasha virago na namna tunavyojipanga kuwarudisha, habari za kusitisha ajira serikalini na mikakati ya kuzirejesha haraka, habari za kupanda kwa bei ya sukari na ukosefu wa nishati ya mafuta, habari ya mabenki kusitisha kutoa mikopo na badala yake kuhakikisha wadeni wake wanalipa haraka nk hazionekani kuwa vipaumbele katika uzalishaji.

Nchi inahitaji kuamka na kuanza kutilia mkazo uzalishaji kwanza kabla ya ugawanaji. Msisitizo wa ulipaji kodi, vita dhdi ya rushwa na ufuatwaji wa sheria lazima visindikize lengo kuu la kuongeza uzalishaji. Sidhani kama tunataka kujenga uchumi usio na wala rushwa, wakwepa kodi, na watiifu wa sheria ambao wamo kwenye nchi yenye kiwango kidogo cha uzalishaji. Sidhani kwamba tupo tayari uzalishaji upungue ili mradi tu sera za uagawanaji na ufuataji sheria zinazingatiwa. Kwasababu, lazima kwanza kuwe na uzalishaji ndipo hayo mengine yawepo na kurekebishwa.

Nchi ilifika pabaya kiuchumi? Jibu hapana! Je sasa iko pabaya? Jibu, tunaelekea kubaya sana, na jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza uzalishaji.
 
DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
500
Washabiki wakisiasa watakuambia nchi ilifikia pabaya! Hao hawajui wanachoongea na wala hawana idea ya kukua kwa uchumi na maendeleo ya watu. Uchumi wetu ulikuwa kufikia hizo asilimia na tulikuwa tunashangiliwa kila kona ya dunia. Tatizo tulilokuwa nalo ni tatizo la kila sehemu Africa: Rushwa na kushindwa kwa kukua kwa uchumi wetu kuhakisi maendeleo yetu.

Tunachoshuhudia sasa ni sera za kugawana pato la taifa kuliko kuzalisha. Kodi tunazozitunga kila kukicha na kuwavalia manyanga wafanyabiashara hazilengi katika uzalishaji bali ugawaji wa pato la taifa kwa njia ya huduma na miundombinu. Kwa sera hizi sasa tunaweza kupaaza sauti na kusema zinaumiza uchumi na hivyo maendeleo yetu.

Investment ambayo ndio uzalishaji inapunguzwa kwa kodi kupitia kitu wachumi wanaita marginal propensity to savings (sent kadhaa zinazotengwa kwa investment kwa kila shilingi unayoipata kama mshahara au faida kutoka katika biashara). Nchi za wenzetu kodi kamwe sio ubabe na wala sio kitu kinachotengeneza vita kati ya wafanyabiashara na serikali Kama inavyoashiria sasa Tz. Maana unafuu wa kodi unaongeza investment/uzalishaji na nyongeza ya kodi inaumiza uzalishaji. Hapa swala la kodi kwa maana hii lazima liangaliwe kama panga ikatayo kuwili.

Ukusanyaji wa kodi kwa uwingi wala sio jambo la kushangiliwa hata siku moja. Wala hakuna uongozi duniani unaopimwa kwa kiwango cha kodi. Very simple, kodi ni kama bima, kadri unapokusanya bima nyingi ndipo unapotakiwa kujiandaa kulipa fidia kubwa maana umechukuwa risk ambayo mlaji wa bima ingemfanya arekebishe tabia na hivyo kujiepusha na madhara tarajiwa. Vivyo hivyo kodi, kadri serikali inapolazimisha watu walipe malimbikizo ya kodi ya awamu iliyopita ndipo inaponyang'anya wafanyabiasha mitaji na ndipo serikali itakapojikuta ikiingia gharama ya kuijenga upya sekta binafsi na ya umma. Wakati hili linafanyika uzalishaji unapungua na uchumi unaangukia pua.

Tatizo, narudia, serikali ya awamu hii imejikita katika kuhakikisha biashara inafuata sheria na kodi inalipwa huku wala rushwa wakidhibitiwa. Haya yote ni mambo mazuri na wazalendo tunatakiwa kuyapongeza na kuunga mkono kila hatua. Tatizo ni kwamba mambo haya yamekuwa substitute ya dhana mzima ya uzalishaji. Tumeacha kuangalia namna ya kuongeza uzalishaji na badala yake tumejikita kwenye income distribution na equalization schemes kana kwamba tunazalisha vyakutosha.

Nilidhani magazeti yangekuwa yanaandika namna tunavyopiga hatua katika kutatua tatizo la ajira. Sera ya viwanda sasa inapotea masikioni mwa umma badala yake mahakama ya mafisadi na vita vya shisha na ushoga vimepamba moto. Vita vya kupambana na rushwa ndio imekuwa ndio habari za asubuhi, mchana, na jioni! Habari za kupungua meli za mizigo bandarini na namna ya kuongeza, habari za watalii kuacha kuja kutokana na kodi, habari za wachimbaji gas kufungasha virago na namna tunavyojipanga kuwarudisha, habari za kusitisha ajira serikalini na mikakati ya kuzirejesha haraka, habari za kupanda kwa bei ya sukari na ukosefu wa nishati ya mafuta, habari ya mabenki kusitisha kutoa mikopo na badala yake kuhakikisha wadeni wake wanalipa haraka nk hazionekani kuwa vipaumbele katika uzalishaji.

Nchi inahitaji kuamka na kuanza kutilia mkazo uzalishaji kwanza kabla ya ugawanaji. Msisitizo wa ulipaji kodi, vita dhdi ya rushwa na ufuatwaji wa sheria lazima visindikize lengo kuu la kuongeza uzalishaji. Sidhani kama tunataka kujenga uchumi usio na wala rushwa, wakwepa kodi, na watiifu wa sheria ambao wamo kwenye nchi yenye kiwango kidogo cha uzalishaji. Sidhani kwamba tupo tayari uzalishaji upungue ili mradi tu sera za uagawanaji na ufuataji sheria zinazingatiwa. Kwasababu, lazima kwanza kuwe na uzalishaji ndipo hayo mengine yawepo na kurekebishwa.

Nchi ilifika pabaya kiuchumi? Jibu hapana! Je sasa iko pabaya? Jibu, tunaelekea kubaya sana, na jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza uzalishaji.
Nimekuelewa sana mkuu
 
mzalendo15

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
1,367
2,000
Uchumi hauwezi kuendelea kwa kuvutia wawekezaji wenye njaa bila kuboresha uwezo wa ndani.

Focus ya serikali hii ni kukusanya kodi lakini haijaweka mazingira endelevu ya kukusanya kodi.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,445

Hongera sana "Mgonjwa wa Ukimwi" (na pia pole sana maana Ukimwi ni hatari!)
umenena vizuri sana!!
 
MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,320
2,000
Uchumi hauwezi kuendelea kwa kuvutia wawekezaji wenye njaa bila kuboresha uwezo wa ndani.

Focus ya serikali hii ni kukusanya kodi lakini haijaweka mazingira endelevu ya kukusanya kodi.

Upo sahihi Mzalendo15, na niongeze tu kwamba mazingira endelevu ya kukusanya kodi yanatengenezwa tu na mazingira na sera madhubuti ya kuongeza uzalishaji. Ongeza uzalishaji utaongeza kodi (makusanyo + tax base) punguza au puuzia sera za uwekezaji/uzalishaji utapunguza kodi (makusanyo + tax base) na hivyo utapunguza uzalishaji mara dufu.

Kodi kama sera hazitakiwi kuwa katika increasing trends bali zinatakiwa ziwe set kwenye automatic mode kuhakisi uhalisia wa mwenendo wa uchumi kiuzishaji. Serikali ya awamu hii ilitakiwa kwanza kutoa fursa ya ongezeko kubwa la shughuli za uchumi, ingejipa mwaka au miaka 2 kuruhusu hili. Of course hili lingekuja kwa gharama zake kama vile inflation, rushwa, na ukwepaji kodi (hali ya kawaida kokote nchi masikini kwenye ongezeko la shughuli za uchumi). Baada ya ongezeko hili ndipo serikali ingefanya fine tuning ya kodi kwa kuanza mstari mpya tangu kuongezeka kwa uzalishaji. Vyovyote vile, uzalishaji ndio unazalisha kodi na kodi hii ndio inatumika kutoa huduma na miundombinu inayoongeza uzalishaji, tax base na kuendeleza gurudumu la uchumi wa nchi.

Wala hatujachelewa, tujikite kwenye uzalishaji sasa. Kilimo, viwanda, utalii, maliasili, international trade, foreign direct investment nk vinatakiwa vipate msukumo wa haraka, mlundikano wa kodi na red tapes kwenye sekta hizo hausaidii.
 
MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,320
2,000
Hongera sana "Mgonjwa wa Ukimwi" (na pia pole sana maana Ukimwi ni hatari!)
umenena vizuri sana!!

Hahaha wala mimi sio mgonjwa wa gonjwa hili hatari! Hii ID nilifunguliwa na rafiki yangu mzungu niliyekuwa nasoma naye na kuishi kwenye apartment tuliyokuwa tumepanga wote! Mgonjwa ukimwi ndio yakawa maneno yake mawili ya kiswahili aliyokuwa anayamudu kuyasema wakati huo 2005! Tangu hapo nimekua nikitumia hii ID na nimejaribu mara kadhaa kuwaomba mods wanibadirishie bila kupoteza records zangu wameshindwa!

Nadhani ifike wakati JF wafanye kama Facebook, waruhusu members kubadiri majina yao, ukitilia manani wakati umebadirika na popularity ya JF imeongezeka.
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
10,199
2,000
Mgonjwa bado upo vizuri sana mgonjwa wa ukimwi bado c4 zipo vizuri hongera kwa mchango muruwa !
 
mzalendo15

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
1,367
2,000
Upo sahihi Mzalendo15, na niongeze tu kwamba mazingira endelevu ya kukusanya kodi yanatengenezwa tu na mazingira na sera madhubuti ya kuongeza
uzalishaji. Ongeza uzalishaji utaongeza kodi (makusanyo + tax base) punguza au puuzia sera za uwekezaji/uzalishaji utapunguza kodi (makusanyo + tax base) na hivyo utapunguza uzalishaji mara dufu.

Kodi kama sera hazitakiwi kuwa katika increasing trends bali zinatakiwa ziwe set kwenye automatic mode kuhakisi uhalisia wa mwenendo wa uchumi kiuzishaji. Serikali ya awamu hii ilitakiwa kwanza kutoa fursa ya ongezeko kubwa la shughuli za uchumi, ingejipa mwaka au miaka 2 kuruhusu hili. Of course hili lingekuja kwa gharama zake kama vile inflation, rushwa, na ukwepaji kodi (hali ya kawaida kokote nchi masikini kwenye ongezeko la shughuli za uchumi). Baada ya ongezeko hili ndipo serikali ingefanya fine tuning ya kodi kwa kuanza mstari mpya tangu kuongezeka kwa uzalishaji. Vyovyote vile, uzalishaji ndio unazalisha kodi na kodi hii ndio inatumika kutoa huduma na miundombinu inayoongeza uzalishaji, tax base na kuendeleza gurudumu la uchumi wa nchi.

Wala hatujachelewa, tujikite kwenye uzalishaji sasa. Kilimo, viwanda, utalii, maliasili, international trade, foreign direct investment nk vinatakiwa vipate msukumo wa haraka, mlundikano wa kodi na red tapes kwenye sekta hizo hausaidii.

Umeongea vizuri sana.
Bila kujenga misingi na sera madhubuti kuboresha uwezo wa ndani tutakuwa tunajidanganya lazima tutambue kwamba maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe.

Kwamfano katika sera ya viwanda ili kuboresha uwezo wa ndani lazima wangeweka classification ya aina ya viwanda ambavyo wawekezaji wanatakiwa wajekuvianzia.
Viwanda vinavyo tumia teknolojia rahisi ambavyo vipo ndani ya uwezo wetu tungeviendesha sisi wazawa.Kwamfano viwanda vya kusindika mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi kwa kiweka sera madhubuti ambayo itamuwajibisha mzawa kuviendeleza na kuvilinda. Viwanda kama hivi Ndio base ya Uchumi wa nchi. viwanda kama hivi vingetoa ajira kwa watanzania kwa zaidi ya asilimia 60% na kuboresha kipato cha mwananchi mojamoja na hata wale wa hali ya chini hivyo kuboresha dhamani ya sarafu ya nchi na ongezeko la pato la taifa.

Wawekezaji wangekuja kuanzisha viwanda vinavyo tumia teknolojia ya juu.
Lakini tukiachia kila kitu wawekezaji kwa lengo la kupata kodi tutadhoofisha uwezo wa watanzania kujitegemea kwa kiwango cha juu.

Inapaswa tujifunze ujasiri kwa wazungu kama uingereza kwa kuthubutu kusimama wao wenyewe ili kuboresha uwezo wa taifa.
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,445
2,000
Hahaha wala mimi sio mgonjwa wa gonjwa hili hatari! Hii ID nilifunguliwa na rafiki yangu mzungu niliyekuwa nasoma naye na kuishi kwenye apartment tuliyokuwa tumepanga wote! Mgonjwa ukimwi ndio yakawa maneno yake mawili ya kiswahili aliyokuwa anayamudu kuyasema wakati huo 2005! Tangu hapo nimekua nikitumia hii ID na nimejaribu mara kadhaa kuwaomba mods wanibadirishie bila kupoteza records zangu wameshindwa!

Nadhani ifike wakati JF wafanye kama Facebook, waruhusu members kubadiri majina yao, ukitilia manani wakati umebadirika na popularity ya JF imeongezeka.
Aisee! story nzuri sana ya hiyo ID. mimi nadhani kwa uzito huo, acha tu ibaki ilivyo. tayari watu wanakujua kwa jina hilo. unajua watu watakudefine kwa depth na weight ya michango yako, na siyo kwa ID yako. Pia una habari kuna sehemu zinaitwa kwa mfano: TANGI BOVU, wakati wala hakuna tangi bovu? au MBUYUNI wakati mbuyu wenyewe ulishakatwa siku nyingi!
 
DNR

JF-Expert Member
Mar 28, 2013
523
500
Hahaha wala mimi sio mgonjwa wa gonjwa hili hatari! Hii ID nilifunguliwa na rafiki yangu mzungu niliyekuwa nasoma naye na kuishi kwenye apartment tuliyokuwa tumepanga wote! Mgonjwa ukimwi ndio yakawa maneno yake mawili ya kiswahili aliyokuwa anayamudu kuyasema wakati huo 2005! Tangu hapo nimekua nikitumia hii ID na nimejaribu mara kadhaa kuwaomba mods wanibadirishie bila kupoteza records zangu wameshindwa!

Nadhani ifike wakati JF wafanye kama Facebook, waruhusu members kubadiri majina yao, ukitilia manani wakati umebadirika na popularity ya JF imeongezeka.
Mzungu maneno ya kwanza kuyamudu huwa salamu kama ...mambo ,hujambo ...etc
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom