Wachumi Mtusaidie ni Kwa nini Biashara Nchini imedorora kama sio kupumulia mashine.Miaka hii ya kuanzia 2016

Kwa ujumla mengi ya matatizo ambayo wadau wameyaongelea hapo juu, yamekuwepo tangu awamu zilizopita. Hivyo sio sababu ya Msingi ya kudorora kwa Uchumi wetu. Ukisoma WB report to Africa, maarufu kama African Pulse, ya tarehe 10 April 2019, utaona kuwa mdororo huu upo Dunia nzima na utaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu. Don't take it personal.

Ukija hapa Nchini, kumefanyika kitu fulani ambacho huwezi kukithibitisha kirahisi. Kitu hicho ni Monetary contraction. Ambayo imetokana na mambo kama mawili. La kwanza ni kubana black market nyingi ambazo zilikuwa zina Leak fedha na kuinject fedha kwenye mzunguko kwa namna ambayo haidhibitiki na Serikali.

Pili, ni Serikali kutaka ikae na fedha zote BOT, na zitolewe tu pale inapobidi. Nadhani hii Walifanya makusudi but with evil intentions. Kwa mfano, wamechukua fedha zote na kuzipeleka kwenye miradi mikubwa ambayo production yake iko kwenye longrun (SG, Aghakan bridge&SGR, ATCL n.k). Fedha zote hizi zinaenda nje ya Nchi, ambako kama mjuavyo forex siyo favorable kwetu. Hii imeathiri sana private au household consumption.

Na Kwa sababu hii ni kama agenda maalum kwa awamu ya 5,nadhani tutaendelea kuugulia maumivu. Na kwa mwenendo huu, kama Serikali ikichapisha noti zaidi na kuziingiza Sokoni, basi uchumi wetu ndio bye bye.

Kwa mtazamo wangu, baada ya hizi project kukamilika na kama tutakuwa na uongozi mzuri mbeleni, basi uchumi wetu utaimarika maradufu. Pamoja na mawazo mengi ya wadau huko juu, Naomba kuwasilisha.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yooote ni
Fisiem ni fisiem tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom