Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Leo kwa kuwa siyo siku ya kazi nilijihimu kwenda soko la Ilala kujipatia mahitaji yangu.
Nilipoteremka stand ya Ilala sokoni (kutokea maeneo ya Buguruni) niliona watu wengi, hasa vijana wameshika T shirt na kofia za CCM (hawajazivaa). Nikakumbuka pale pana ofisi ya CCM ya mkoa karibu na Kobis petrol station. Walikuwa wanazigawa bure Takukuru mko wapi?
Lakini kuna kitu kimoja kilinitia moyo sana na naweza kusema bila kujiuma mdomo kwamba Watanzania wanataka mabadiliko pamoja na hizo hongo za bure za CCM.
Nilipoingia kwenye mvurugano wa watu wanaouza mboga na matunda, nilisikia vijana (wabeba mizigo etc) wakiambizana: Nendeni mkachukue nguo za bure lakini mabadiliko lazima.
Mwingine akijibu: Umenena taabu hii tuliyo nayo hadi lini?
Jamaa mmoja mtu mzima aliyekuwa karibu ananunua majani ya maboga akasema Mabadiliko lazima mwaka huu tumechoka kula majani kama mbuzi kwani nyama haikamatiki.
Mwingine alimjibu huyo kwa kicheko: Si alisema yule waziri fisadi kwamba hata ikibidi tule majani, ndege ya rais ni lazima inunuliwe? Mmesahau? Si mnaona majani yalivyotanda hapa? (akionyesha mboga za majani za kila aina zilivyojaa sokoni pale.
Mwingine mzee mmoja akasema: Aliyesema si yule waziri mwenye kesi aliyenadiwa na Kikwete kwamba mtu safi?
Nikaendelea na shughuli zangu huku nikajawa na mawazo makubwa nikiwaza mabadiliko yaja iwapo watu wengi wanazo fikra za namna hiyo.