Wachomwa na zanzibar kusajili meli za mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachomwa na zanzibar kusajili meli za mafuta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTANGANYIKA ORIGINAL, Jul 1, 2012.

 1. M

  MTANGANYIKA ORIGINAL Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

  Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:
  Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-
  (a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships; and
  (b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.
  (2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship is registered under this part.
  Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.

  Meli za mafuta Zilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:
  Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka
  1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta
  2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus
  3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta
  4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta
  5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus
  6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta
  7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta
  8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta
  9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus
  10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus
  11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus
  Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons

  Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration)

  Kulingana na “United Nations Convention Law of the Sea”, Article 91, na za “Geneva convection of Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza usajili huo.

  Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo. Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Isijeikawa hivyo vyombo vinavyosajiliwa Zenj ni vile ambavyo vilishapoteza ssifa za ki-maritime kokote duniani!, hatutaki ya spice yajirudie. Wasalaam.
   
Loading...