Wachina wazuiwa kuingia Kenya wakitokea Tanzania

Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
49,580
2,000
Kenya. Watu 16 walizuiwa kuingia nchini Kenya kupitia mpaka wa Lunga Lunga katika mji wa Kwale wakitokea Tanzania
Kati ya watu hao, 13 ni raia wa China.

Raia hao wa China ni Xiao Zhanquan, Xu Shaul, Xu Duo, Lyu Xiaohua, Zhou Changyong, Jiang Chunyang, Xiao Zhanquan, Lyu Xiaohua, Wang Xiaoba, Shang Deyuan, Huang Honghui, Yang Yubiao na Cao Bingwang.

Watu hao walisindikizwa na madereva watatu wa Tanzania ambao ni Saidi Seif Mapunda, Hassan Mohammed Makolo na Wema Ramadhani Muambeya.

Ripoti ya Polisi iliyoonwa na kituo cha runinga cha Citizen Kenya inaonyesha watu hao waliwaambia wakaguzi katika eneo hilo kuwa walikuwa wanaelekea mjini Mombasa kwa ajili ya kazi maalumu katika kampuni ya Bamburi Cement Ltd.

Hata hivyo, baada ya mahojiano zaidi ilitakambulika kuwa tangu walipowasili nchini Tanzania kati ya Machi 4- 16, 2020 hawakutimiza siku 14 za kujitenga katika karantini zilizowekwa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.

Wote 16 walizuiwa kuingia Kenya kutokana na kutokidhi maagizo ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na walirudishwa mpakani.

Mwananchi
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
49,580
2,000
Ukisoma hii article usipolia wewe sio Mtanzania.

Yani hawa viongozi wa Tanzanian wanawaruhusu tu wachina kuingia nchini bila kufanya lolote.
Imagine hao wachina wn Corona je. Wameambukiza wabongo wangapi?
Uzuri hili korona litaanza kuwapata hao tuliowapa Mamlaka na wanaleta mzaha.

Au labda ni tatizo la elimu?
Elimu ya pale UDSM inatakiwa ifanyiwe marekebisho makubwa.

Udsm itaua nchi yetu.

Kwa nini products za pale zinataka kuua watanzania?

Kweli kabisa wanashindwa atleast kufunga mipaka au kuwaweka wageni quarantines kwa siku 14?
Wangepungukiwa ni nini?

Hii ni makusudi kabisa.

Ingekuwa chadema hapo tungeona nguvu kubwa sana.

Nawasilisha
 
Mzimu wa Kolelo

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,098
2,000
Safi sana wakenya nawapongeza kwa hilo
hvyo ndivyo mamlaka inatakiwa iwe heko iwe mfano kwa nchi zingine zenye utaratibu wa kishamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,276
2,000
Mnajua Yale makaratasi ya ziada ya kura yanatokaga Wapi? Kwa Nini kura fake zinakamatwa...!

Kuna ushwahiba Hapo....
 
Top Bottom