Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,800
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limewakamata raia watano kutoka China wanaomiliki mgodi wa Zem Tanzania Limeted katika kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama, wakitorosha mchanga wenye madini mbalimbali maarufu kama makinikia.
Raia hao wa China wamekamatwa wakiwa katika harakati za kusafirisha mchanga huo kwenda Jijini Dar es Salaam kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Japhary Mohamed, amesema walipata taarifa kuhusu wawekezaji hao kuandaa mpango wa kutorosha mchanga huo wa madini na ndipo Jeshi la Polisi lilipolazimika kuweka mtego ambao umewezesha kukamatwa.
Anasema kuwa walifanikiwa kukamata magari mawili katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma yakiwa na masanduku 14 yenye mchanga huo wenye madini ya aina mbalimbali.