Wachina wampiga dereva, Mkuu wa kituo asema utaratibu wa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina wampiga dereva, Mkuu wa kituo asema utaratibu wa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwanaharakatihuru, Aug 15, 2012.

 1. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kuendelea kuwanyanyasa wazawa wachina watatu wa kampuni ya CHICO wamemfanyia unthinkable mfanyakazi alietaka kuwapa msaada watoto sabini baada ya kutaka kuwapa msaada wa kuvuta basi lao.

  Dereva Yassin Twaha alichofanyiwa na maelezo ya kamanda Bundala yanatia kinyaa wazalendo wa nchi hii sasa tusimame tujilinde wenyewe.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Aisee sie tunawapapatikia sana hawa ngozi nyeupe!! Ndio maana nao wanatunyanyasa wakiwa kwao na hata huku kwetu!! Ndio maana mie simfagilii mzungu kabisa!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,008
  Trophy Points: 280
  Hivi wachina wako wangapi nchini hadi watutawale!???????
  Tuwarudi hawa hata kwa manati. Wamesha jua bei ya mahakimu, huko hamna haki kwa mzawa
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanaharakati huru imekuwaje?Tuhabarishe ni wapi hayo yametokea?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wachina wanapata kiburi kwa ajili ya rushwa wanazotoa kwa Polisi.
   
 6. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mkiwaudhi watampiga BAN baba yenu asiende kwao!
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kila kazi ina kanuzi zake, msaada upi? walikuwa hatarini kupoteza maisha? au walikuwa wameharibikiwa tu na gari? unaweza kuona unatoa msaada kumbe unahatarisha zaidi usalama wao. mfano kuwavuta na wao wamo ndani ya gari linalovutwa, kama kafanya hivyo anastahiki kichapo, kwani alikuwa anahatarisha maisha ya hao wanafuzni zaidi ya kuwasaidia.

  Huyo dereva ni punguani avute basi na kuna wanafunzi ndani? huyo alistahiki kulimbokwa.
   
 8. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jiulize ilikuwaje askari wachache tu waliweza kuswaga watumwa kibao toka Kigoma mpaka Bagamoyo .... wakipita sehemu nyingi tu zenye wazawa wengi (mfano Tabora, Dodoma, Morogoro etc.) .... hakuna mtu alithubutu kusaidia kuwatoa utumwani ndugu zetu! .... Inasikitisha, lakini Waafrika Ndivyo Tulivyo.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nyie manotetea mnaona huy dereva alikuwa anafanya la maana kuvuta basi liliharibika lenye wanafunzi ndani? amma kweli Watanzania bado tupo nyuma sana kuhusu mambo ya usalama.
   
 10. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama unaijua hiyo barabara huyo dereva alifanya kitendo cha uungwana kikubwa ila polisi wetu are for sale
   
 11. M

  Marketer JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kijana kabla ya kwenda kufanya kazi kwa wahindi/wachina/waarabu inabidi uchukue training ya self defence au judo lasiivo yatakayo kukuta sauri yako! ohooo! Unless uwe umeaga kwenu na kwenu kwenyewe sumbawanga/tanga/pemba/ukingani hapo mchina akikupiga mkono unanasa mpaka akuombe msamaha mwenyewe. chezea african technology!!!!
   
 12. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali dhaifu huongozwa na watu dhaifu.......
   
 13. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zomba nilishakuambia huo upolisi wako utakucost wewe kuwa shushu tu lakini you are in the wrong move mkuu. Jamaa amedhalilishwa kwa ajili ya kuwaondoa watoto wale waliokuwa wanaenda kwenye umitashumta ili wasivamiwa na majambazi ile barabara nadhani unawajua. Lakini kwa kumvunja mkono na kumtengua nyonga sio ubinadamu we will fight chico company and we will build chinese phobia kitaeleweka tu
   
 14. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una gari wewe au unategemea PT
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Inahusu nini?

  Huyo dereva alikuwa punguani na wachina wamempa fundisho safi kabisa. Harudii tena na nna uhakika na kazi hana kwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi. Msitake kutetea ujinga.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hata wawe wanakwenda wapi. Huwezi kuvuta gari lenye aboiria ndani, ni makosa makubwa sana. Huyo dereva kichapo halali yake. Usitete ujinga.

  Kama unajuwa kuwa haya mabasi ya siku hizi, breki, usukani, gear hufanya kazi kwa kutegemea injini usingesema yote hayo. Gari ikizima ikawa inavutwa hata ndogo haitakiwi ipakie abiria, hata kuivuta na dereva ndani ni makosa. Ikiharibika inatakiwa ije breakdown kuivuta au kuipakia iiondoe ilipo ili isisababishe madhara zaidi.

  Huyo dereva kulimbokwa ni sawa kabisa. Atarudia?
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Asante kwa taarifa.

  Ningependa kurudia tena, tunapoweka mada hapa tuwe tunajaribu kutoa picha kamili, lakini kama ulivyoleta mada kama mipasho kana kwamba tunakijua unachozungumzia ujumbe wako haujakamilika, nikama katika english structure unapoletewa sentence isiyobeba subject and predicate, na hivyo kuwekwa katika kundi la "flag."

  Kwa hiyo naweza kusema ujumbe ulioleta sijauelewa, ni flag, samahani kwa hillo. Unapoleta ujumbe jaribu kujibu maswali yale muhimu matano, hata kama yote huna walao matatu yanaweza kusaidia wasomaji kuelewa, lakini ilivyo hapa nashindwa nichangie nini kwani sijuia undani wa habari hiyo kwa vile imeelea hewani tu.
   
 18. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ala! Kumbe kosa la dereva!
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha barabara wala njia, Kafanya makosa kuvuta gari yenye wanafunzi ndani. Usitetete ujinga, madhara yake yangeweza kuwa makubwa zaidi. ya kuwawacha hapo na kwenda kuwaombea msaada unaostahili. Tanzania hii huwezi kwenda Kilomita 20 bila kukutana na kijiji kama hakuna hifadhi ya serikali. Angekwena hata kambini kwao kuwaombea usafiri mwngine badala ya kujidai uhodari wa kuwavuta.

  Sijui aliviona videmu vya seko ndio vikamzuzuwa. maana ushasema Umitashumta lazima vilikuwepo vyenye T shirt zinazoonyesha ramani ya nido, akazuzuka.
   
 20. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa taarifa yako CCK wakichukua nchI usajili wakada zote unaanza upya matoyoyo kama nyie mnao walinda wawekezaji tunafukuza
   
Loading...