Wachina, Wakorea, Wahindi, Waarabu, wanapata wapi ujasiri wa kufukuza watendaji wa afya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina, Wakorea, Wahindi, Waarabu, wanapata wapi ujasiri wa kufukuza watendaji wa afya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Froida, Jun 3, 2011.

 1. F

  Froida JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Karibu mwezi sasa tunaangalia kwenye vyombo vya watu matapeli wa huduma ya afya,wakorea,wchina,waarabu,wahindi, wakifoka na kuwafukuza wataalamu wetu toka wizara ya Afya,kwa maneno makali,kuwatupia mikono ya dharau,wanadai wajitambulishe kwa barua ,wanawzuia wasikague baadhi ya maeneo,kiujumla hawana heshima kabisa kwa kauli,lugha na matedno kwa wataalamu hawa

  Najiuliza ni vipi wahamiaji haramu wanaweza kutoa huduma ya tiba bila vibali wala ujuzi,tunauhakika gani kama watakuwa hawachomi watanzania sindano yenye viambukizo vya wadudu kama birusi bya ukimwi na hepatatis,

  Inakuwaje wanaendesha hizi hospitali au dispensary bila kijiji,kata,wilaya,mko kuwastukia hivi tuko salama kweli nchi hii,tunaambiwa kuna wageni wanakuja kuchimba madini,wengine wamechukua nyumba hawataki kutoka,wengine wamejimilikisha mashamba,wengine wana viwanda feki vya juice,sabuni je kuna mtu kweli anajali usalama wa wananchi

  Inakuwaje watu wasiozungumza kiswahili wanaweza kuajili,wanunua wapi dawa wanazotibia hawa wagonjwa,nina hasira sana kuona serikali inaweza ikawa legelege kiasi hiki mpaka kila mtu ambaye ni mgeni akaingia nchini nakufanya afanyavyo huku akiwanyonya wananchi na kuharibu afya za watanzania
  Watanzania wenzangu hali ya kuchezea afya za wananchi ni baya sana kuna siku tutakuja kushangaa watu wengi wana kansa,au hawazai,au si rijali au watoto wanazaliwa vilema kutokana na kupatiwa tiba zisizo na usalama wowote
  Nadhani wizara ya afya hili zoezi liwe endelevu
   
 2. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hasira ya kwanza ielekeze kwa watz kwa kuchagua hicho unachoita serikali legelege.
  Hasira ya pili imwage idara ya uhamiaji; hao wageni wameingiaje ndani ya nchi.
  Hasira ya tatu ielekeze kwenye wizara husika, je walifanya ukaguzi wa kina kabla ya kutoa vibari kwa hivyo vituo.
  Mwisho chukua hatua. Hatma ya taifa hili ipo mikononi mwako na mimi, siyo wauza sura. Hawa wababaishaji tunaishi nao mtaani......
   
 3. Saeedgenius

  Saeedgenius Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Serikali ni watu, wewe ukiwa mmoja wao, jiulize umechukua hatua gani? badala ya kukaa kulalamika. Nadhani ukichukua hatua itaweza kutusogeza hatua moja mbele lakini lalamo hazina tija kubwa kwetu.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  katika Maisha yangu naweza kujivuna kwmba kuna mambo mengi mazuri ambayo nimeyafanya ambayo kwa uhakika zaidi nimeweza kutumikia nchi yangu,lakini mambo ya hii serikali legelege inayaoruhusu kila upupu kuingia kwenye nchi yetu nashindwa kuelewa hakika ningekuwa afisa uhamiaji,bwana labour,mto leseni,mtekelezaji wa sera nakadharika,nakadharika nisingethubutu kuiadhili nchi hii nzuri yenye watu wazuri wenye utulivu wa hali ya juu,kuwafanya wanyanyasike kwenye nchi yao,inauma kwamba kuna watu wanaingiza dawa zimeandikwa kichina,kiajemi,kihindi,kiarabu tunzaniona kwenye vituo hivi vya matapeli wa tiba,ebu niambie wewe unayefurahia jambo ovu la aina kuendelea,haya mambo yapo hapa Tanzania tuu
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii ni moja ya fulusa za kikwete muwekezaji kwanza
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  iNASIKITISHA SANA NIMEONA KWENYE HABARI ZA ITV SAA 2 USIKU JINSI WA MISRI WASIO NA VIBALI VYA KUFANYA KAZI ACHA UDAKTARI WANATIBU NDUGU ZETU KULE MUSOMA HALAFU WANAFUKZA WATENDAJI WA SERIKALI BILA NNIDHAMU.
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Hicho ndio kilichonikasirisha sana kile kisichana anathubutu kumwambia daktari eti go go go i dont want to see you halagu anarudhisha mlango kuwasukumia nje hivi wanatuonaje hawa watu wengine kule kwao wamezaliwa kwenye maguta na mitaro ,mbaya sana hii haiwezakani kabisa
   
 8. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Ahsante Saeedgenius,
  Serikali legelege hutokana na watu legelege, watu wasilalamike, wajue kuwa wana uwezo wa kubadili mambo yaende kama wanavyotaka. Kila mmoja asikubali kuwa duni, asikubaliane na mambo yaliyo kinyume na ustawi wa jamii yake, ajue kwamba ni muhimu kupambana na hakika wenye haki watashinda!
   
 9. H

  Haki JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesahau Wazungu?
   
 10. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Thi unajuwa tunavoabudu wadhungu .. tehtehte!
   
 11. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi unafikiri hawa wakaguzi wangekuwa wamefanyiwa hivi kwa weusi wenzao (watz),sasahivi si ingekuwa ni habari nyingine?si ajabu ungekuwa unashuhudia FFU na ma-defender yao wakiwa hawachezi mbali ili yeyote atakaye hoji wawetayari kumkamata hata kumpeleka mahakamani.
  Sasa sioni tatizo la wageni kutunyanyasa ndani ya nchi yetu wenyewe,manake sisi tunawapa heshima ya miungu watu.Acha wanaswe vidbao sisi yetu macho.
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu keli ni mambo ya ajabu Daktari aidi ya miaka sita sule na mingine anayofanya kwa ajili ya specialisation anakwenda kusukumiwa mlango na yeye anachekacheka tuu,nashangaa na nitaendela kushangaa,nani ametupumbaza kiasi cha kwamba mtu unaruhusu mhamiaji haramu akunyanyase kwente nchi yako na taaluma yako mmh
   
 13. P

  Percival JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,568
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hao watendaji unaozungumiza wanakwenda kukagua ili wapate rushwa tu. Inawezekana wamewaandama hawa jamaa kwa kutaka rushwa ndio maana wanawafukuza , Afya ya wananchi ni kitu cha mwisho kwa hao watendaji.

  Je babu wa Lolionda nani alimkagua ? au dawa yake ilipimwa kuwa haina madhara ?
   
Loading...