Wachina wakamatwa na Shehena ya Meno ya Tembo Bandarini Dar

Thanks Invisible

Kuna baadhi ya watu ndani ya serikali hii na nchi bado wanadhani Tanzania ya sasa bado kama ile ya miaka ya 1990's ambapo Wachina na Wasia walikuwa wanavuna Meno ya Tembo na vipusa vingine kama mchicha shambani.

Hawataki kujifunza na kubadilika kulingana na mazingira kama baadhi ya watu ninaowafahamu walioosha biashara zao na kuwa ndani ya sheria.

Kuna umuhimu mkubwa wa kupitisha sheria ya kunyongwa pindi mtu yeyote atapatikana na hatia ya kuwa na nyara za serikali bila idhini kisheria, otherwise, tutaendelea kuwa na habari kama hizi ambazo hata zikipatikana haziwezi kuwarudishia Tembo uzima tena.

Bora kuzuia kuliko kukamata nyara za serikali.

Na hao waliowashika walikuwa wa Serikali ya chadema?
 
Mi nahisi sasa wanachi inapaswa tuchukue hatua mkononi popote tunapowaona wachina maana this is too much sasa,na hii demokrasia yetu tunayoingamgania inatuponza kila kitu kutaka kufanya kwa misngi ya sheria. Na ushahidi

Kwanza mchukuwe akilini zenu mikononi. Hao wachina wameshikwa hawajashikwa? uliwashika wewe?
 
Kwani kunaubaya gani Serikali kuuza kiasi cha shehena ili zipatikane fedha za kulinda Tembo waliosalia?...Maslahi ya nchi Muhimu Jamani...
 
Watanzania ni wazuri kulalamika kwenye mitandao tu yataishia apa apa
China hao wangenyongwa ndani ya wiki moja
 
Ajuza kama ungekuwa na akili timamu ungetambua kuwa ukamataji ungeanzia mbugani na sio bandarini. Mtu kaua tembo, kasafirisha hadi bandarini na serikali yenu sikivu ya mazezeta ipo??

Jitambue bibi kizee

Kinana Strikes Once Again

Kwa hiyo kama hawakushikwa mbugani na bandarini wasishikwe? wewe punguani kweli kweli.
 
Mkuu ficha upumba.vu wako usifiche hekima. Unajua lvory Coast tembo walikuwa wengi sana kule leo hii wajukuu wanaona tembo kwenye picha.

Na kwa mara ya kwanza kipindi cha Kikwete tunaona mikakati thabiti na endelevu ya kuzuia huu ujangili, wa kabla yake walikuwa wapi? wamelala.
 
Na yule jangili mwingine mwenye lijumba likubwa arusha lenye maandaki, ambaye amekuwa akilia lia sana kuwa boss wake hampangii kazi (baada ya kumgundua ni jangili) ndo juzi kaitisha press conference kujifanya yupo concerned tembo wameawa wengi kumbe yote ilikuwa kutuzuga tu na kuwaonyesha wachina kuwa mzigo upo powa kuchukuliwa !!
 
Watanzania ni wazuri kulalamika kwenye mitandao tu yataishia apa apa
China hao wangenyongwa ndani ya wiki moja

Tanzania hatuna sheria ya kunyonga wanaouwa tembo na wanaosafirisha meno ya tembo, labda upeleke mswaada bungeni ipitishwe sheria mpya.
 
Wanyongwe hadharani,

Hii operesheni tokomeza irudi tu tena kwa nguvu zaidi

Mimi mwenyewe nimesikia hii habari kutoka vyanzo ninavyoviamini sana
Kazi kupiga siasa tu. Sasa mbona wengi mmenyamaza wakati hila imetumika kusitisha operation tokomeza na kagasheki kutupwa nje wakati alisimama kishujaa kupambana na majangili.
 
Back
Top Bottom