Wachina wafumwa wakichimba madini katavi national park | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina wafumwa wakichimba madini katavi national park

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  Sunday, July 22, 2012  MKUU wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe amewataka wawekezaji wanaokwenda kuwekeza katika sekta ya madini katika mkoa wa Katavi wawasiliane na ofisi za serikali mkoani humo kabla ya kuingia katika mikataba ya uendeshaji wa shughuli za uzalishaji katika maeneo husika.

  [​IMG]

  Mwandishi wa habari hii kutoka Katavi Willy Sumia anaripoti kuwa wito huo umetolewa na mkuu kufuatia utapeli waliofanyiwa wawekezaji wa kutoka nchi ya China na kampuni yao ya Red Ore Mining Co. Ltd ya DSM na kupelekwa eneo la pori la akiba la Luafi mpakani na hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma na shaba.

  [​IMG]

  Taarifa zinasema kuwa kampuni hiyo yenye makao yake jijini DSM inayoendeshwa na Raia wa nchi ya China ilianza shughuli katika eneo hilo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita hadi jana walipofika askari wa wanyamapori wa Pori la akiba la Rukwa / Lukwati/ Luafi na hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwaamuru waondoke katika eneo hilo kwakuwa ni eneo lilitengwa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na ustawi wa wanyama pori.

  Askari hao walipozungumza na waandishi wa habari walisema kuwa awali walipowakuta raia hao wa China waliweza kuwahoji na kubaini kuwa walikuwa wameingizwa eneo hilo kimakosa na ofisi ya hifadhi hiyo iliwaandikia barua yenye Kumb Namba RLLGR/LGR.1/72/14 ya tarehe 06/06/2012 iliyokuwa akiwapa amri ya kuondoka eneo ndani ya siku saba tangu tarehe ya barua hiyo lakini hawakuweza kutekeleza agizo hilo

  Askari hao wa wanyamapori walisema kutokana na kushindwa kutii agizo hilo waliamua kufika eneo husika kuwachukua viongozi wa kampuni hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa kwa maamuzi zaidi kwani walibaini kuwa walipewa taarifa za uongo na mtu aliyewauzia hilo eneo kwani hilo eneo na eneo lisilotakiwa kufanyiwa shughuli yoyote ile

  Walisema hata barua walizojibiwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii yenye kumbukumbu namba HB 178/286/01/102 iliyosainiwa na ndugu J. Muya kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo ya tarehe 20/06/2012 pamoja na ile iliyotoka kwa wakala wa misitu Tanzania (TFS) yenye kumbukumbu namba TFSC.166/286/01/29 ya tarehe 25 Juni, 2012 ikieleza kuwa eneo hilo waliloomba kwa barua siyo eneo linaloruhusiwa kwa kufanya shughli yoyote ya kibinadamu isipokuwa kwa utafiti wa mafuta, gesi au madini ya uraniamu tu

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao na Wachina wamiliki wa Kampuni ya RedOre Mining Co. Ltd, mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe alisema kuwa katika mazungumzo na wawekezaji hao alibaini kuwa walitapeliwa na mtu aliyewauzia eneo hilo baada ya kuona kuwa eneo hilo haliruhusiwi kwa shuguli yoyote.

  Alisema kutokana na hali iliyojitokeza inabidi sheria ichukue mkondo wake na huku wawekezaji hao wakiwa nje ya hifadhi kwani tayari eneo hilo limeshaharibiwa na kuingiza hasara kubwa Taifa hivyo ili kuepusha malalamiko ya kuwa wageni hao wameonewa na Watanzania hivyo mahakama ndiyo itakayoamua nani kakosea, wapi na namna gani kakosea ili kulinda utawala bora.

  Akizungumzia juu ya aliyewatapeli wawekezaji hao mkuu wa mkoa alisema wao ndio wanamfahamu aliyewauzia na wanafahamu watampata wapi hivyo ni jukumu la wawekezaji kumtafuta wamuawajibishe kwa kuwatapeli ambapo mkuu huyo wa mkoa alitoa ushauri kwa wawekezaji wengine wasiingie mkataba na mmiliki yeyote wa ardhi katika mkoa wa Katavi bila kuwasiliana na Halmashauri au ofisi ya madini ya kanda ya Magharibi iliyoko mjini Mpanda kwa ushauri na msaada wa taarifa za eneo husika.


  SOURCE: KATAVI YETU


   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mlitegemea wafanye nini kwenye shamba la bibi tena linalosimamiwa na mataahira na mafisi? Kimsingi uwekezaji unaoendelea nchini utaleta maafa na vita baadaye. Ingawa wachache kati yetu wananufaika kwa kupata cha juu kama tulivyosikia hivi karibuni kuwepo zaidi ya dola 300 milioni huko kwenye mabenki ya Uswisi. Hata hivyo huko tuendako nchi haitakalika kutokana na dhuluma hii ya wazi wazi. Hii ni aibu kubwa kwa utawala unaojidai ungeleta maisha bora kwa wote wakati ni maafa na balaa kwa wote.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Unaona hawa Wachina... Wameona Madini; na wakpo Katavi National Park na Pia Vijidudu Vyetu pia Wanavila

  Kama Jongoo, Ndege, Faru, Nyoka, Vyura, Paka, Mbwa, Snails n.k

  Ni watu wa kuogopa - Mzindakaya huyo - lazima CCM ianguke 2015
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ndio wawekezaji wetu hao tulioamua kuwafungulia mipaka.
  Hapo wanatafuta mtaji ili wajaze yeboyebo kariakoo.
   
 5. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tanzania my motherland,what do they do to you? A few of Your sons and daughters have turned into selfish demons,money matters more to them than the life of their kins. God bless my motherland...
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ina utajiri wa kutisha w amadini na mali asili ila wananchi tumelala na viongozi ndio wanatuburuza na kutuingiza mikataba ya aibu na ya ajabu kabisa!sijui nani atatuamsha jamani!watu wanatoka maili 100,000 kuja kuchimba madini sisi hapa maili 2 hatuyaoni au hatuwezeshwi au hatujaamka!!majirani zetu wangekuwa na madini haya sijui tungewashikia wapi!!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Ndio Tanzania hiyi inayoendeshwa na DHAIFU na Serikali yake DHAIFU, wenyewe hujiita Serikali sikivu!!!! sijui kwa usikivu upi waliokuwa nao.
   
 8. v

  vngenge JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ingekuwa ngozi nyeusi ashapigwa shaba
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hawatochukuliwa hatua yoyote zaidi ya kulipa ushuru wa 10% wa Mafisadi CCM. Nchi yetu mnaiharibu Magamba
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  ...Hata Watanzania wangekutwa wanafanya haya kule China basi hukumu yao ni kifo tu.

   
 11. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hao siyo wa kwanza,kuna wengine kule Chunya walikuwa na PROSPECTING LICENCE lakini walikuwa wanachimba,huku wananchi wakibaki na ngonjera ya kidumu chama cha ...!
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mwisho wa ssiku wataachiwa na no kesi hapa...
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
 14. MD24

  MD24 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hao ndio wawekezaji wa ccm...
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  china imeahidi kuipa afrika ma trilion,kikwete unavyopenda misaada thubutu kuwa gusa wachina..tanzania tumefavywa shamba la bibi
   
 16. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ukiwachunguza sana hawana hata work Permit
   
 17. m

  massai JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inamaana waliuziwa hilo eneo wakiwa daresalama?hawakufanya survey?mamlaka ya hifadhi hawakua na taarifa?mkuu wa mkoa na wilaya pia?wenyeji vipi au ndio wale kidumu chama ambao wengi wao jua wanaita mwezi na bahari wanaita ziwa basi tu kwakua huwa wepesi kuoteshwa chuki na ujinga?kweli shamba la bibi.
   
Loading...