Wachina wacharanga Watanzania mapanga ndani ya Tanzania

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
18,778
2,000
Halafu mbaya zaidi, walisaidiana na Watanzania wengine kukatakata wenzao kwa mapanga, ama kwa kweli Watanzania mumekua aibu ya Afrika.

======


POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu nane, wakiwemo raia watano wa China, kwa tuhuma za kujeruhi Watanzania wawili kwa kuwacharanga na sime, baada ya kutokea ugomvi kati ya Wachina wanaomiliki kampuni ya michezo ya kubahatisha, maarufu kama Bonanza na watu waliokuwa wanacheza mchezo huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei, Mei 25, mwaka huu saa 11 jioni maeneo ya Soweto Kata ya Ruanda jijini hapa, watu wawili Abison Hamis (36) na Gilbert Mwakanyema (32) wote wakazi wa Manga Veta, walijeruhiwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na raia wa China, kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ambao ni Watanzania.

Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka kati ya mfanyabiashara na raia wa China, Chen Yen (43) anayeishi Veta jijini hapa na Hamis maarufu kwa jina la Ndele, baada ya Mtanzania huyo kutamka neno la Kichina, lililomuudhi Yen na kusababisha ugomvi uliosababisha baadhi ya watu kujeruhiwa.

Akifafanua, alisema awali raia huyo wa China alifika eneo hilo kuchukua fedha kwenye mashine ya mchezo wa kubahatisha ya Kampuni ya Bonanza akiwa amefuatana na dereva wake, Gift Elia (23) maarufu kwa jina la Mwamelo anayeishi Airport, wakiwa na gari yenye namba za usajili T 252 DNL aina ya Toyota Kluger katika eneo lijulikanalo kwa jina la Sports Centre, linalomilikiwa na Salum Juma pia wa jijini Mbeya.

Alisema wakati huo, Hamis alifika eneo hilo kucheza “pool table” akiwa ameongozana na Gilbert Mwakanyemba, Kennedy Mwamlima na mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Yohana.

Alisema baada ya kuzuka kwa ugomvi huo, Yen alipiga simu kuomba msaada kwa wenzake, ambao walifika na kuanza kuwashambulia akina Abison na Gilbert kwa sime maeneo mbalimbali ya miili yao.

Alisema waliokamatwa ni Wachina Yen, Xiao Jing (30), Lin Hai (30), Lyu Qzing (36), Jiang Ze Dong (39) wote wakazi wa Meta jijini hapa na Watanzania Elia, dereva na mkazi wa Airport, Herman Elius maarufu Mwalwiba (20) dereva na mkazi wa Esso na Mwamlima (28) dereva na mkazi wa Ituha jijini hapa.

Chanzo: HabariLeo
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,621
2,000
Yule mfanyakazi wa hotel alicharazwa viboko na wachina nae alikua mtanzania? Si mkenya yule?

Huu upuuzi wa jambo kutokea unajumuisha jamii nzima utaisha lini?

Nikiona mtu wa Afrika Mashariki anajitutumua kuwa wako bora au wana unafuu kwenye ufukara hua natabasam tu.

Lakini kujipa moyo na kujifariji kwa maneno sio hatia.
 

The Book

JF-Expert Member
May 21, 2017
2,211
2,000
Huyu jamaa mleta mada ana uwezo mdogo wa kunyambua mambo,kiufupi ni kilaza!
 
  • Thanks
Reactions: Oii

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,292
2,000
Kiongozi maelezo yako ya Watanzania tumekuwa aibu ya Afrika yamekaa kinafiki zaidi... hujawaza nje ya box... Yanayotokea Kenya tena kati yenu unayajua.. na yanatia aibu zaidi
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
778
1,000
Sijawahi hata kumwona Mtanzania mmoja amekuwa na maisha bora kwa kuajiriwa na Mchina au Muhindi. Hao madereva wa Wachina walijiona kama raia wa Uchina kisa mishahara ya laki 2.5
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom