Wachina wabadilisha mwelekeo na kufuatilia zaidi lugha za Afrika kikiwemo Kiswahili

ldleo

Senior Member
Jan 9, 2010
165
250
微信图片_20210512154723.png

Hivi karibuni chuo kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing BEWAI kilifanya mashindano makubwa yaliyowashirikisha wanafunzi wanaosomea lugha mbambali za Afrika katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China, zikiwemo Kiswahili, Kihausa na Kiamhara. Lengo la mashindano haya ni kukuza uelewa wa Wachina juu ya utamaduni, Jiografia, siasa na hata mambo ya kijamii kwa ujumla ya watu wa Afrika.

Mashindano haya yanatupa funzo moja, kwamba hakuna lugha au utamaduni wowote ulio bora kuliko mwingine.

Kwenye mashindano hayo wanafunzi wengi wachina walikuwa ni wale wanaosomea lugha ya Kiswahili. Hivi sasa nchini China lugha ya Kiswahili imekuwa ikifundishwa katika vyuo vikuu zaidi ya saba vilivyopo katika mikoa mitano ambapo nikivitaja kwa uchache kuna chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing, chuo kikuu cha lugha cha Shanghai, Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, na chuo kikuu cha lugha cha Tianjin.

Kiswahili ikiwa ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na watu zaidi ya milioni 100 duniani, imejijengea umaarufu wake nchini China. Mbali na kufundishwa vyuoni, hivi sasa lugha hii imekuwa ikitumika kwenye makampuni mbalimbali yanayojihusisha na lugha ya Kiswahili, yakiwemo Redio China Kimataifa, kampuni ya Startimes, pia kazi za Kiswahili zimekuwa zikitafsiriwa kwa Kichina na za Kichina kutafsiriwa kwa Kiswahili.Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya lugha wakiwa kwenye mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika

Kutokana na maendeleo ya kijamii ya hali ya juu, wanafunzi wengi wa China huwa wanaelekeza macho yao zaidi kwenye vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya kwa ajili ya masomo yao ya elimu ya juu, lakini baadhi ya wanafunzi Wachina wamebadilisha mwelekeo huo na sasa kupata mafunzo yao katika nchi za Afrika.

Katika siku za hivi karibuni idadi ya wanafunzi Wachina wanaokwenda kupata elimu yao ya juu katika nchi za Afrika inazidi kukua siku hadi siku. Ingawa ongezeko hilo sio kubwa sana, lakini kitendo cha kuongezeka kinaashiria kwamba wanafunzi wengi zaidi wa China wanatambua lugha mbalimbali za Afrika.

Kutokana na ushirikiano kati ya China na Afrika, hususan katika masuala ya biashara na kiutamaduni, China imekuwa ikikaribisha lugha za Afrika hasa Kiswahili. Hivi sasa kuna wachina wengi waliopo katika nchi za Afrika zinazozungumza Kiswahili, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia kaskazini, Msumbiji, Mashariki mwa DRC, Rwanda, Burundi, Somalia na visiwa vya Comoro. Ndio maana lugha hii imepewa uzito mkubwa kwasababu inachangia maendeleo ya pande mbili.

微信图片_20210512154802.png

Washiriki wa mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika wakifurahia baada ya mashindano kumalizika na kupata washindi

Katika mwaka 2012, mwanafunzi mmoja wa China aliyejifunza Kiswahili, Shen Yuning, alipotangaza kwamba ana mpango wa kukusanya maneno kwa ajili ya kamusi ya Kiswahili-Kichina, marafiki zake wengi walidhani kwamba labda anatania. Na tokea atoe tangazo hilo Disemba mwaka huo, Shen alikuwa amekusanya karibu maneno 5,000, ambapo hatimaye alipata maneno 25,000 huku akifanya kazi kwa saa 15 kwa siku nchini Kenya na Tanzania akisaidiwa na Waafrika. Shen Yuning pia alishirikiana na wanafunzi wa chuo cha Habari cha Zanzibar.

Mbali na Kiswahili kufuatiliwa kwa karibu nchini China, lakini hata Kichina pia kimekuwa na soko kubwa sasa katika nchi za Afrika. Taasisi za Confucius ambazo zinatoa mafunzo ya lugha ya Kichina na kufunza utamaduni wa China, zimewasaidia sana wanafunzi wa Afrika kuwa karibu na utamaduni wa China pamoja na kujifunza Kichina sanifu “Mandarin”. Taasisi zaidi ya 20 za ina hii zipo katika Afrika, zikitoa kozi za lugha na mihadhara, maonesho n.k.

Lugha ni muhimu kwa mawasiliano, na kutokana na urafiki kati ya China na Afrika Mashariki, tunatarajia kupitia lugha ya Kiswahili ambayo ndio kubwa zaidi katika Afrika pamoja na Kichina, pande mbili zitaongeza ushirikiano na kuwasiliana kwa urahisi zaidi katika masuala ya kidiplomasia, kibiashara, kiutamaduni na kijamii. Pia kama ilivyo kwa wazungumzaji wa Kiswahili wanavyofuatilia kazi za Sanaa za China kupitia lugha, tunatarajia na wazungumzaji wa Kichina pia watafuatilia kazi za Sanaa za Kiswahili baada ya kutafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kichina.
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
6,137
2,000
Waafrika sijui ni lini tutakuwa na akili, anachokifanya mchina ni marketing strategy. Kiufupi mchina anataka kumiliki masoko ya maeneo hayo, na hatua ya kuanzia ni kuwa na watu unaoweza kuelewana nao katika mazungumzo. Baada ya muda kidogo utawakuta hawa wachina wapo maeneo husika wanafanya biashara bila kuhitaji tena wakalimani wa maeneo husika.
Lugha kama lugha haina mchango pasipokuwa na uchumi imara na teknolojia nzuri.
Wakati wachina wanajipanua kujifunza lugha ngeni, sisi tunataka tujifungie kwenye Kiswahili na kuachana na lugha nyingine.
Lugha ina mchango mdogo sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
2,956

wana strategies kali sana
 
Ausar

JF-Expert Member
Mar 19, 2021
308
500
Wachina wa kko wanapiga kiswahili kama vile wamezaliwa humuhumu nchini....wanakielewa kiswahili fasta kuliko wazungu
 
Pine Valley

JF-Expert Member
Nov 30, 2020
963
1,000
Hivi karibuni chuo kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing BEWAI kilifanya mashindano makubwa yaliyowashirikisha wanafunzi wanaosomea lugha mbambali za Afrika katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China, zikiwemo Kiswahili, Kihausa na Kiamhara. Lengo la mashindano haya ni kukuza uelewa wa Wachina juu ya utamaduni, Jiografia, siasa na hata mambo ya kijamii kwa ujumla ya watu wa Afrika.

Mashindano haya yanatupa funzo moja, kwamba hakuna lugha au utamaduni wowote ulio bora kuliko mwingine.

Kwenye mashindano hayo wanafunzi wengi wachina walikuwa ni wale wanaosomea lugha ya Kiswahili. Hivi sasa nchini China lugha ya Kiswahili imekuwa ikifundishwa katika vyuo vikuu zaidi ya saba vilivyopo katika mikoa mitano ambapo nikivitaja kwa uchache kuna chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing, chuo kikuu cha lugha cha Shanghai, Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, na chuo kikuu cha lugha cha Tianjin.

Kiswahili ikiwa ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na watu zaidi ya milioni 100 duniani, imejijengea umaarufu wake nchini China. Mbali na kufundishwa vyuoni, hivi sasa lugha hii imekuwa ikitumika kwenye makampuni mbalimbali yanayojihusisha na lugha ya Kiswahili, yakiwemo Redio China Kimataifa, kampuni ya Startimes, pia kazi za Kiswahili zimekuwa zikitafsiriwa kwa Kichina na za Kichina kutafsiriwa kwa Kiswahili.

View attachment 1781763
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya lugha wakiwa kwenye mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika

Kutokana na maendeleo ya kijamii ya hali ya juu, wanafunzi wengi wa China huwa wanaelekeza macho yao zaidi kwenye vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya kwa ajili ya masomo yao ya elimu ya juu, lakini baadhi ya wanafunzi Wachina wamebadilisha mwelekeo huo na sasa kupata mafunzo yao katika nchi za Afrika.

Katika siku za hivi karibuni idadi ya wanafunzi Wachina wanaokwenda kupata elimu yao ya juu katika nchi za Afrika inazidi kukua siku hadi siku. Ingawa ongezeko hilo sio kubwa sana, lakini kitendo cha kuongezeka kinaashiria kwamba wanafunzi wengi zaidi wa China wanatambua lugha mbalimbali za Afrika.

Kutokana na ushirikiano kati ya China na Afrika, hususan katika masuala ya biashara na kiutamaduni, China imekuwa ikikaribisha lugha za Afrika hasa Kiswahili. Hivi sasa kuna wachina wengi waliopo katika nchi za Afrika zinazozungumza Kiswahili, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia kaskazini, Msumbiji, Mashariki mwa DRC, Rwanda, Burundi, Somalia na visiwa vya Comoro. Ndio maana lugha hii imepewa uzito mkubwa kwasababu inachangia maendeleo ya pande mbili.

View attachment 1781766
Washiriki wa mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika wakifurahia baada ya mashindano kumalizika na kupata washindi

Katika mwaka 2012, mwanafunzi mmoja wa China aliyejifunza Kiswahili, Shen Yuning, alipotangaza kwamba ana mpango wa kukusanya maneno kwa ajili ya kamusi ya Kiswahili-Kichina, marafiki zake wengi walidhani kwamba labda anatania. Na tokea atoe tangazo hilo Disemba mwaka huo, Shen alikuwa amekusanya karibu maneno 5,000, ambapo hatimaye alipata maneno 25,000 huku akifanya kazi kwa saa 15 kwa siku nchini Kenya na Tanzania akisaidiwa na Waafrika. Shen Yuning pia alishirikiana na wanafunzi wa chuo cha Habari cha Zanzibar.

Mbali na Kiswahili kufuatiliwa kwa karibu nchini China, lakini hata Kichina pia kimekuwa na soko kubwa sasa katika nchi za Afrika. Taasisi za Confucius ambazo zinatoa mafunzo ya lugha ya Kichina na kufunza utamaduni wa China, zimewasaidia sana wanafunzi wa Afrika kuwa karibu na utamaduni wa China pamoja na kujifunza Kichina sanifu “Mandarin”. Taasisi zaidi ya 20 za ina hii zipo katika Afrika, zikitoa kozi za lugha na mihadhara, maonesho n.k.

Lugha ni muhimu kwa mawasiliano, na kutokana na urafiki kati ya China na Afrika Mashariki, tunatarajia kupitia lugha ya Kiswahili ambayo ndio kubwa zaidi katika Afrika pamoja na Kichina, pande mbili zitaongeza ushirikiano na kuwasiliana kwa urahisi zaidi katika masuala ya kidiplomasia, kibiashara, kiutamaduni na kijamii. Pia kama ilivyo kwa wazungumzaji wa Kiswahili wanavyofuatilia kazi za Sanaa za China kupitia lugha, tunatarajia na wazungumzaji wa Kichina pia watafuatilia kazi za Sanaa za Kiswahili baada ya kutafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kichina.
Mlivyo mafala mnakenua Tu , idiots
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,745
2,000
Utafikiri kwa kutupenda la hii ni mbinu ya kuteka soko na kuepuka usumbufu wa lugha
Milioni kadhaa wakijua lugha zetu na Soko wanalo
Sisi tunapigana na ukabila na hatuna bidii hata ya kujua lugha zao
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,774
2,000
Utafikiri kwa kutupenda la hii ni mbinu ya kuteka soko na kuepuka usumbufu wa lugha
Milioni kadhaa wakijua lugha zetu na Soko wanalo
Sisi tunapigana na ukabila na hatuna bidii hata ya kujua lugha zao
Baada ya miaka 5-10 ijayo ukalimani wa kichina utakuwa hauna dili tena Africa
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,602
2,000
Hawa ni wakoloni uchwara wapya wanaotafuta kujiend
Hivi karibuni chuo kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing BEWAI kilifanya mashindano makubwa yaliyowashirikisha wanafunzi wanaosomea lugha mbambali za Afrika katika vyuo vikuu mbalimbali nchini China, zikiwemo Kiswahili, Kihausa na Kiamhara. Lengo la mashindano haya ni kukuza uelewa wa Wachina juu ya utamaduni, Jiografia, siasa na hata mambo ya kijamii kwa ujumla ya watu wa Afrika.

Mashindano haya yanatupa funzo moja, kwamba hakuna lugha au utamaduni wowote ulio bora kuliko mwingine.

Kwenye mashindano hayo wanafunzi wengi wachina walikuwa ni wale wanaosomea lugha ya Kiswahili. Hivi sasa nchini China lugha ya Kiswahili imekuwa ikifundishwa katika vyuo vikuu zaidi ya saba vilivyopo katika mikoa mitano ambapo nikivitaja kwa uchache kuna chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing, chuo kikuu cha lugha cha Shanghai, Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Beijing, na chuo kikuu cha lugha cha Tianjin.

Kiswahili ikiwa ni lugha inayokadiriwa kuzungumzwa na watu zaidi ya milioni 100 duniani, imejijengea umaarufu wake nchini China. Mbali na kufundishwa vyuoni, hivi sasa lugha hii imekuwa ikitumika kwenye makampuni mbalimbali yanayojihusisha na lugha ya Kiswahili, yakiwemo Redio China Kimataifa, kampuni ya Startimes, pia kazi za Kiswahili zimekuwa zikitafsiriwa kwa Kichina na za Kichina kutafsiriwa kwa Kiswahili.

View attachment 1781763
Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya lugha wakiwa kwenye mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika

Kutokana na maendeleo ya kijamii ya hali ya juu, wanafunzi wengi wa China huwa wanaelekeza macho yao zaidi kwenye vyuo vikuu vya Marekani na Ulaya kwa ajili ya masomo yao ya elimu ya juu, lakini baadhi ya wanafunzi Wachina wamebadilisha mwelekeo huo na sasa kupata mafunzo yao katika nchi za Afrika.

Katika siku za hivi karibuni idadi ya wanafunzi Wachina wanaokwenda kupata elimu yao ya juu katika nchi za Afrika inazidi kukua siku hadi siku. Ingawa ongezeko hilo sio kubwa sana, lakini kitendo cha kuongezeka kinaashiria kwamba wanafunzi wengi zaidi wa China wanatambua lugha mbalimbali za Afrika.

Kutokana na ushirikiano kati ya China na Afrika, hususan katika masuala ya biashara na kiutamaduni, China imekuwa ikikaribisha lugha za Afrika hasa Kiswahili. Hivi sasa kuna wachina wengi waliopo katika nchi za Afrika zinazozungumza Kiswahili, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia kaskazini, Msumbiji, Mashariki mwa DRC, Rwanda, Burundi, Somalia na visiwa vya Comoro. Ndio maana lugha hii imepewa uzito mkubwa kwasababu inachangia maendeleo ya pande mbili.

View attachment 1781766
Washiriki wa mashindano ya kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bara la Afrika wakifurahia baada ya mashindano kumalizika na kupata washindi

Katika mwaka 2012, mwanafunzi mmoja wa China aliyejifunza Kiswahili, Shen Yuning, alipotangaza kwamba ana mpango wa kukusanya maneno kwa ajili ya kamusi ya Kiswahili-Kichina, marafiki zake wengi walidhani kwamba labda anatania. Na tokea atoe tangazo hilo Disemba mwaka huo, Shen alikuwa amekusanya karibu maneno 5,000, ambapo hatimaye alipata maneno 25,000 huku akifanya kazi kwa saa 15 kwa siku nchini Kenya na Tanzania akisaidiwa na Waafrika. Shen Yuning pia alishirikiana na wanafunzi wa chuo cha Habari cha Zanzibar.

Mbali na Kiswahili kufuatiliwa kwa karibu nchini China, lakini hata Kichina pia kimekuwa na soko kubwa sasa katika nchi za Afrika. Taasisi za Confucius ambazo zinatoa mafunzo ya lugha ya Kichina na kufunza utamaduni wa China, zimewasaidia sana wanafunzi wa Afrika kuwa karibu na utamaduni wa China pamoja na kujifunza Kichina sanifu “Mandarin”. Taasisi zaidi ya 20 za ina hii zipo katika Afrika, zikitoa kozi za lugha na mihadhara, maonesho n.k.

Lugha ni muhimu kwa mawasiliano, na kutokana na urafiki kati ya China na Afrika Mashariki, tunatarajia kupitia lugha ya Kiswahili ambayo ndio kubwa zaidi katika Afrika pamoja na Kichina, pande mbili zitaongeza ushirikiano na kuwasiliana kwa urahisi zaidi katika masuala ya kidiplomasia, kibiashara, kiutamaduni na kijamii. Pia kama ilivyo kwa wazungumzaji wa Kiswahili wanavyofuatilia kazi za Sanaa za China kupitia lugha, tunatarajia na wazungumzaji wa Kichina pia watafuatilia kazi za Sanaa za Kiswahili baada ya kutafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kichina.
Mlivyo mafala mnakenua Tu , idiots
Hawa ni wakoloni uchwara wanaotafuta kujinufaisha kwa ujinga wetu.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
9,458
2,000
Mlivyo mafala mnakenua Tu , idiots
Ha ha ha ha ha. Huwa nadhani nipo pekee yangu kustaajabu watu kufurahia kuona mataifa ya kigeni wanajifunza lugha yao kwa bidii sana bila kuhoji wana malengo gani na sisi siku zijazo.

Ukiona taifa tajiri linaleta urafiki kwa kasi sana na taifa masikini, heads up..... Something fishy is about to happen.
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,299
2,000
Haha, mchina for everybody! (tumia sauti ya konde boy) 😂😂😂

Mchina ni mjanja kupindukia, sijui ni Zambia kule washahamia tangu zamani. Kuna dogo wa kichina ana ranch dadeq, anaishi na familia yake na wazazi wake kule. Ni mkulima pia. Yaani anakwambia harudi kwao, Afrika ndio home sasa. Duh, tutaisha tukiwaamini sana hawa jamaa. Akili zao sio mchezo. Alafu wanatoka kwao na target flani, either yao binafsi au kapewa na serikali na ni lazma wa accomplish kabla hawajarudi kwao.
 
Mac Bully 001

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
6,299
2,000
Soon n very soon wanachokitafuta watakipata
Africa kuwa koloni la mchina
Utumwa unarudi
Hawa viumbe walipashwa kuishi kwao kama wao ambavyo hawataki watu weusi kwenye nchi yao
Washajazana kwao, nchi ishakuwa ndogo, sahi wanataka kuijaza Africa yetu hii, wale na vyakula vyetu vya nguvu, hahaha. Mchina hana haya kabisa! 🤣
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom