Wachina, utu na Tanzania

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
21,033
64,844
Wasalaam ndugu zangu,

Mimi namshukuru Mungu aliye juu kwa kunipa uzima na kila pumzi ninayoivuta nampa utukufu yeye. Naandika haya leo kwasababu nimeumia vibaya sana na kwa neema za Mungu tu nimepona.Katika pilika pilika zangu za kutafuta maisha kuna siku nikasafiri nikaenda sehemu fulani kutafuta maisha, huko sikuwa na mtu nayefahamiana naye sana.

Japo sikuwa na ndugu hata moja Watanzania sisi ni watu wenye Ukarimu sana na namshukuru Mungu sana kwa upendo wao; kiukweli niliishi kwa amani na furaha nikajihisi kama nipo nyumbani.Sasa kinachonfanya niandike haya ni siku ambayo naondoka kurudi nyumbani, nilikuwa natembea niwahi usafiri na unajua vijijini usafiri ni adimu.

Kipindi hiki ni cha mvua na kuna matope na utelezi mwingi barabarani. Kwa bahati mbaya nlikuwa natembea halafu nimevaa raba mtoni ambazo zinaleteza, mara nikajikuta niko chini sielewai nimefikaje.Hapo chini pana korongo kubwa nimtumbukia na matope yamenijaa mwili mzima, kwa mbali nikasikia watu wanafanya oooh!Ile kuangalia vizuri nikakuta wachina fulani nadhani ni wahandisi wanafanya ujenzi wa barabara.

Kweli nilijaribu kuinuka kumbe nikajikuta siwezi hata kidogo ili kusema nijaribu kuinua mguu nashindwa. Nikapandisha mguu wa suruali nione nini kinaendela, nikakuta mguu wa kulia umepasuka na donda kubwa na damu zinatoka na sehemu nyingine zimevilia damu.Kilichonishangaza sana ni pale ambapo nipo katika hali ile wale Wachina wakaniangali tu na kuendelea na maisha yao kama vile hakuna kilichotokea.

Nawaza nafanya nini hata kusimama siwezi na kuangalia mfukoni kucheki simu kumbe niliikalia na display imevunjika basi kimoyo moyo nikasema Mungu nitie nguvu tu.Wale majamaa Wachina wakaingia ndani ilhali mimi nipo pale chini wakaniangalia tu na mguu wangu na matope yale basi wakaondoka.

Niwe muwazi moyo waku ulizimia sana kuona wamefanya vile nikawaza je ni tamaduni tofauti au pesa mbele utu baadae?Nikaja kukumbuka kuna tukio lilitokea pale Iringa vijijini Pawaga, kuna jamaa moja alikuwa na mkandarasi wa hapahapa Tanzania.

Gari lake lilipata ajali poroni basi akamfuata mchina moja alikuwa anafanya ujenzi wa barabara amsaidia kuvuta gari lake kwasababu alikuwa na Gari kubwa lenye WINCH CARRIER.Yule Mchina alikubali akamsaidia ila katika kuendela kufanya hivyo wale wenzake wakamfuata na kuanza kumpiga hadi wakamuumiza. Wakatoa ilegari yao basi yule Mtanzania akabaki stranded porini hadi asubuhi.

Nikiwa nimelala pale chini baada ya muda kuna msamalia mwema alikuja akanibeba, alishangaa sana kile wale wachina wamefanya. Hapo sijiwezi hata kidogo jamaa kanitafutia pikipiki wakati huo hata sijiwezi, Mungu ndiye atamlipa yule ndugu kwa Utu wema wake.

Nina mikwaruzo mwilini sana na mwili umevimba maana pale chini palikuwa na mawe ya chuma na kokoto na vyuma vya ujenzi hivyo unaweza kuelewa mtu kaumiaje. Nlilala hadi nimesafiri nimerudi nyumbani asubuhi hii nimepumzishwa na nimepata madawa namshukuru Mungu kwa Uzima.

Japo, kuna somo nimejifunza kubwa sana wiki hili. Sipendi kuongea siasa ila waswahili husema mcheza kwao hutuzwa. Baba wa taifa Nyerere pamoja na baadhi ya sera zake za kiuchumi kushindwa lakini alituacha sisi Watanzania wamoja.Nimejua nifanye mambo yote niende duniani kote lakini hakuna ndugu kama Mtanzania, hii bila kujali dini, mkoa au kabila.

Waafrika hasa Watanzania ni lazima tujifunze hili somo. CHARITY BEGINS AT HOME.Mlio makazini mfanye kazi, wanasiasa muache unafiki na wasomi elimu yenu iwakomboe ile mwisho wa siki Taifa hili lifike mbali.

Nasema hivi kwasababu, huenda wale Wachina hawakutaka kunisaidia kwasababu ya Weusi wangu, Uafrika wangu au Utanzania wangu. Hayo yote yanawezekana.Kinachoumiza zaidi ni pale ambapo hawa Wachina ndiyo wanakuwa marafiki wakubwa wa CCM na Watawala wetu.

Naomba nieleweke kwamba dhumuni si kueneza chuki dhidi ya Wachina na Uchina lakini nataka tukumbuke hata kwenye ngazi za kitaifa wanatusaidia sana kwasababu tuna vitu vya kuwapa. Hasa hasa madini na tenda mbali mbali.

Ndugu zangu mpaka sasa mtu anayeitwa Mtanzania huyo ndiye ndugu yako.
Fanya ufanyalo usimbague, usimdharau, usimtenge wala ukafanya jambo lolote baya la kuhatarisha maisha yae au maslahi yake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom