Wachina ni NOMA kwa Kukopi - Wavumbua Goojle Badala ya Google


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,381
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,381 280

Google ya Kichina - "Goojle" Saturday, January 30, 2010 1:01 AM
Wachina wamedhihirisha kwa mara nyingine kuwa wao ni wakali wa kukopi kwa kuikopi tovuti ya google na kutoa tovuti yao inayoitwa Goojle na pia kwa kuikopi YouTube na kutoa YouTubecn. Wachina katika kuendeleza mpambano na tovuti za kampuni ya Google ya Marekani wameziigiza tovuti za Google na YouTube.com na kutoa tovuti zao za Goojle na YouTubecn.com.

Hivi karibuni Google walitishia kusimamisha shughuli zao nchini China kutokana na mashambulizi toka kwa hackers wa nchini China.

Katika kuendeleza vita hivyo, Wachina wametoa tovuti ya Goojle ambayo imetengenezwa kwa kuigiza kila kitu kutoka kwenye Google. Kuanzia rangi mpaka mpangilio wa ukurasa wa Google.

Herufi "jle" katika Goojle zinamaanisha dada kwa lugha ya taifa ya China, Mandarin wakati herufi "gle" katika Google zinamaanisha kaka katika lugha ya Kichina.

Tovuti ya Goojle imeambatanisha meseji ambayo inasema "Dada alikuwa na furaha sana baada ya kaka kuutupilia mbali uamuzi wake wa kuondoka na kuamua kukaa na dada yake". Meseji hiyo ilikuwa ni kijembe kwa Google ambao wanatishia kusimamisha shughuli zao nchini China.

Nayo YouTube ya Kichina YouTubecn.com video zake zote zinatoka kwenye YouTube original inayomilikiwa na Google ambayo imepigwa marufuku nchini China.

Tovuti hizo mbili ziliwekwa online kuanzia katikati ya mwezi huu punde baada ya google kutishia kusimamisha shughuli zake nchini China.

Kampuni ya Google yenye makazi yake mjini California ilifungua matawi yake nchini China mwaka 2006 na ilisema kuwa itaendelea kuwepo nchini China iwapo serikali ya China itasaidia kukomesha mashambulizi ya hackers wa China.

Wachina ni maarufu kwa kutoa bidhaa feki kuanzia kwenye magari mpaka kwenye madawa. Tovuti ya Goojle ni kithibitisho kuwa Wachina wanatisha kwa kutoa vitu vya kukopi.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3996746&&Cat=2
 
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Una uhakika wameiga ? hebu weka kichwa kamili cha habari kama kilivyo kwenye habari yenyewe unapofanya hivyo pia umevunja sheria za miliki
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,376
Likes
1,302
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,376 1,302 280
MChina balaaa, wazungu watajijuuu
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
39,002
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 39,002 280
Kwani google wameshindwa kuweka security zao wenyewe ili kulinda maslahi yao?
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Messages
2,596
Likes
1,863
Points
280
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2007
2,596 1,863 280
Inawezekana wameiba hizo herufi tatu za domain yao "g, o, o na e" na siyo architecture ya SERP yao.
 
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2007
Messages
2,596
Likes
1,863
Points
280
Chamoto

Chamoto

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2007
2,596 1,863 280
Kwani google wameshindwa kuweka security zao wenyewe ili kulinda maslahi yao?
Kama una army ya watu ambao wamelengesha bunduki kwenye kichwa chako ukiambiwa unabidi "u-hack big G" au la unakuwa baridi unafikiri akili ya ku-overcome hizo security haita kuja?

Trust me everyday I simulate http requests...there is always a way out when it comes to survival...
 

Forum statistics

Threads 1,251,234
Members 481,615
Posts 29,763,493