Jamaa tuwe wakweli hivi wanaotutesa ni wachina au ujinga wetu? Hawa kina mama kutumia madawa ya kunenepesha *^#@ na kujichubua ni matokeo ya sisi wandume kupenda lumbesa na ving'aravyo na ndiyo kina dada wanafanya hivyo.
Cha msingi ni sisi kubadilika katika mitazamo yetu kwenye nyanja hizo kwani imefika wakati hivi sasa [hasa mijini] ni vigumu kukuta mwanamke mwenye rangi halisia na mkitaka kujua athari ya urembo huu hebu nendeni ocean road mtaona ongezeko la cancer ya ngozi,figo kwa kina mama.
Wanatulete ukiangalia wenyewe vibody structure vyao poa tu hata makalio hawana. ni ujinga wa wanaoyatumia kwanini usirithike na umbile alilokupa mwenyezi Mungu.
jamani wadada turidhike na jinsi mungu alivyotuumba,kama mtu unalo unalo tu na kama mtu huna huna tu hata utumie madawa haisaidii sana sana kujitafutia maradhi ya ajabu ajabu tu.kwanza uzuri wa mwanamke ni tabia,mwanamke ukiwa na tabia njema utamvutia kila mtu.halafu hawa wachina wanataka kutumaliza,mbona wao migongo kama meza ya kupigia pasi lkn hawaangaiki kutumia wanatuletea sisi.
wakilizika na umbile waliopewa na mwenyezi MUNGU hawatapata wanachokitafuta, huo ulimbukeni ndo unaosumbua watu, maana ilikuwa mikorogo na sasa tena hips!!!!!!!, mbona wao hawatumiiii???
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.