Wachina 150 katika mradi wa barabara ya km 65 je wote hawa ni wataalamu au ni siasa?

gayella

Member
Jun 23, 2011
11
2
Ndugu wana Jf, naomba niwasilishe hoja hii kwenu, nilfanikiwa kufika katika mradi huo nilichokiona, hata mhesabu trip za mchanga katoka china, wasimamizi wa vibarua ni wachina halafu waliowengi hawana elimu. Je, swali sasa wanaingiaje inchini hawa, kw vigezo gani. maana kazi wanazofanya watanzania wapo wengi sana naamini. Uhamiaji wanafanya nini au ni kugonga mihuri tu bila kujua kwa vile wachina hawa niliambiwa kwa rushwa wanaongoza, maana wamegundua sumu ya mtanzania ni rushwa. hawa wachina wapo mradi wa barabara tanga horohoro. naomba mulijadili hili la sivyo ajira zote zinaenda kwa wageni wakati wazawa wenye fani hizo wapo
 
Mkuu hata mimi nilishangaa mradi wa barabara toka Korogwe hadi Handeni kila baada ya kilometa moja unakumbana na wachina 4 mpaka 10 nikajiuliza hivi Tanzania tuna kwenda wapi ?.
 
Swali hilo elekeza wizara ya kazi na uhamiaji wao ndio watoa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Pia waweza kuuliza kupitia website ya serikali utajibiwa
 
Mkuu hata mimi nilishangaa mradi wa barabara toka Korogwe hadi Handeni kila baada ya kilometa moja unakumbana na wachina 4 mpaka 10 nikajiuliza hivi Tanzania tuna kwenda wapi ?.

tulijengewa reli, tukaiuwa wenyewe, wamekuja kutujengea uwanja wa mpira, sasa ni pay back time.
 
Swali hilo elekeza wizara ya kazi na uhamiaji wao ndio watoa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Pia waweza kuuliza kupitia website ya serikali utajibiwa

mkuu....kama face to face haupewi majibu, kwenye website/email ndo utajibiwa? Tanzania hii hii??
 
Ni kweli hii barabara imejaa wachina (sina uhakika kama wanafika au kuzidi idadi ya 150 iliyotajwa),kila hatua ni wao tu hata kuhesabu trip za mchanga ni wao,sehemu ambayo sijawaona ni katika kufagia barabara tu,ni tofauti na barabara ya mwenge-tegeta ambapo kuanzia mwenge hadi tegeta utakutana na wajapan wachache sana,ilifika sehemu nikawa na wasiwasi na barabara hii ya tegeta lakini kwa hatua waliyofikia nimeona kweli wanaweza,tatizo ni foleni inayokera kuanzia tegeta sokoni kutokana na ujenzi huu.
 
Hapo uhamiaji tuna maboga tu. Halafu mbona waziri wa mambo ya ndani alisema anataka kupitisha fagio kwa hayo maboga halafu kimya!
 
Nasema hivi, Laiti Serikali ingekuwa makini, nchi hii tatizo la ajira ingekuwa ni ndoto.
Ajira nyingi zimeshikiliwa na wageni ambao wengi wao sio wataalamu, kazi hufundishwa na wabongo.
 
Mkuu Ndibalema,

Ni kweli kabisa serekali imelala kabisa katika hili eneo.Utashangaa baada ya mradi kumalizika wachina wote watahamia sehemu mbali mbali kama hilo halitoshi tutawaita wawekezaji {wauza maua,makarai na plastic}.

Nasema hivi, Laiti Serikali ingekuwa makini, nchi hii tatizo la ajira ingekuwa ni ndoto.
Ajira nyingi zimeshikiliwa na wageni ambao wengi wao sio wataalamu, kazi hufundishwa na wabongo.
 
Waacheni Wachina wafanye kazi yao maana Watz wakipewa hata kuhesabu magari ya mchanga ataiba tu na pia kwenye diesel ndiyo balaa zaidi
 
Nani kakwambia waChina hawaibi kwa taarifa yako wanapiga nyoka diesel mtindo mmoja mradi ukimalizika wanakimbilia Kariako wanafungua maduka ya maua ha ha ha ha.

Waacheni Wachina wafanye kazi yao maana Watz wakipewa hata kuhesabu magari ya mchanga ataiba tu na pia kwenye diesel ndiyo balaa zaidi
 
hapa dodoma wanajenga barabara ya iringa - dodoma kila gari la maji,vifusi kuna mchina mmoja nenda dodoma- manyara hivyo hivyo baada ya miaka 20 tutegemee vijana wa kutosha wasio na baba
 
AMKENI WA BONGO NA MUANZE KUFANYA KAZI SIO BLA BLA , NI HAKI YAO WACHINA KULETA HAO WATU ,engineer wa kichina analala ndani ya container camp mshahara wake ni usd 500 mbongo anataka million plus GARI na weekend hayupo porini , wameshaajiri wabongo wamechoka ukiona hivyo , hivi kwanini ma engineer wakibongo wasijiunge na kuanzisha kampuni ya ujenzi wa barabara , WATASEMA HAKUNA PESA ZA VIFAA hivisasa dar kila kifaa kipo unakodi tuu na kuanza kazi TUACHE KUSEMA TUINGIE MBUGANI TUJENGE NCHI YETU
 
hapa dodoma wanajenga barabara ya iringa - dodoma kila gari la maji,vifusi kuna mchina mmoja nenda dodoma- manyara hivyo hivyo baada ya miaka 20 tutegemee vijana wa kutosha wasio na baba

TUWAFUNGE DADA ZETU GAVANA ??? wacha wabongo wachanganye damu labda tutapata wabunge wenye akili ya maendeleo kama china
 
Nani kakwambia waChina hawaibi kwa taarifa yako wanapiga nyoka diesel mtindo mmoja mradi ukimalizika wanakimbilia Kariako wanafungua maduka ya maua ha ha ha ha.

Sawa mkuu nimekupata, maana nilifikiri sababu ni kudhibiti uwizi kumbe na wao ni wezi
 
Wachina hawa wako more labour based hivyo wanaweka manyapala wengi kuwasimamia waTanzania ambao ni wavivu; hawawezi kufanya kazi vema mpaka wasimamiwe na wezi sana; waakipata upenyo kidogo wachina wanakuwa waameliwa.
Hili pengine siyo tatizo la uhamiaji tu bali la kitaifa zaidi kwa sasa.
Tunahitaji kiongozi wa kushika kiboko. nmjerumani alijua hilo. la sivyo tuendelee kulia lia tu.
 
Tuseme ukweli hawa wanaogopa gharama za ujenzi utakuwa juu vile tumezoea kuiba hata trip za mchanga. Tukubali kuwa patakuwepo na vibarua hewa.
 
Tunalo hilo na hii serikali legelege, muda si mrefu tutakuwa km Guanzhou, wachina wa kumwaga!!
 
Mkuu hata mimi nilishangaa mradi wa barabara toka Korogwe hadi Handeni kila baada ya kilometa moja unakumbana na wachina 4 mpaka 10 nikajiuliza hivi Tanzania tuna kwenda wapi ?.

Hatuaminiki!
 
Back
Top Bottom