Wachimba dawa kituo cha Makambako

Magane

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
202
57
Niko ndani ya moja ya mabasi yaendayo Dar kutoka Mbeya mara basi linasimama na konda anawaambia abiria " jamani mkachimbe dawa , msichelewe ni kwa muda wa dakika tano tu" basi kila abiria anatoka haraka kwenda nje ya basi kuelekea uchochoroni. Utararibu ni kwamba akina baba wana mwelekeo wao na kina mama hivyo hivyo na ni marufuku kwenda kinyume. Sasa wana jf nilichojionea kule uchochoro ni kwamba kumechimbwa mashimo kina na diameter ni kama ft moja halafu kumefagiliwa wacha tu.Baada ya hapo unasikia tena konda akiwahimiza abiria wangie ndani ya basi.Ninachotaka kupoint out ni kwamba watu wakiamua wanaweza wakajiongoza wenyewe bila hata katibu kata au mwenyekiti wa mtaa kuwasimamia katika jambo lao la maendeleo.Kumbuka pale kituoni pana biashara za bites na vinywaji baridi.Kweli wanawajali wateja wao.
 
Ni uchafu tu na kudhaliisha abiria wengine hasa akina mama. mahali pale huwa hapana maji wala privacy ya kutosha.
 
Kwani hawawezi kusimama shm ambayo ina vyoo kwa ajili yakutunza mazingira?
 
Mabasi mengine bwana,Dar-Mbeya,kuchimba dawa mara nne,panda Happynation,tunachimba dawa Aljazeera tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom