Wachezaji Yanga waisoma namba, hawajalipwa mishahara miezi minne

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
yanga.JPG

Bundi wa maisha magumu ameendelea kuzunguka katika mitaa ya Jangwani baada ya wachezaji wake kuanza kulalama chinichini kwamba mshahara sasa umefikia miezi minne.

Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi minne sasa, jambo ambalo limewafanya waanze kulalamika.

"Kabla ya kwisha kwa ligi, tuliambiwa tupambane kubeba ubingwa. Mambo yatakuwa safi, lakini naona hali si nzuri hadi sasa.

"Mwisho wa mwezi huu (Mei), itakuwa miezi minne. Mmekuwa mkisema hatujitumi, hatuvumilii. Basi sasa mtutetee, maana miezi minne mingi ndugu zangu na sisi tuna familia," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wakikubali kwamba mishahara imekuwa tabu na baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji, mambo yamezidi kuwa mabaya zaidi.

Wachezaji hao walipambana mwishoni bila ya mishahara hadi kufanikiwa kufikisha pointi 68 zilizowapa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.

Chanzo: Salehe Jembe
 
Tatizo Wanayanga wanapenda pepo bila ya kufa..zimetolewa namba za kuchangia...watu hawachangi..timu yetu wote
 
Hahaaaaa adui muombee njaa atanyoosha mikono juu tu wa kimataifa hao hatimae sa hizi wanakula nyasi,
Poleni sana watani.
 
Ukisoma tu habari hii huku ukiwa unapima credibility yake kuna chembe ya shaka inayokuingia akilini haraka haraka.

Msalimie Saleh Jembe, ila mkumbushe kuwa tumekwisha Utawala hauna ukata wa kutowalipa salary players ukizingatia Klabu ipikusanya takribani Mil 351 Kwenye mchango uliofanyika last month.

Pia wachezaji wamelipwa pesa za pongezi za kubeba Ubingwa.....

Wengi wako likizo wanakula bata hivi sasa!
 
Tatizo Wanayanga wanapenda pepo bila ya kufa..zimetolewa namba za kuchangia...watu hawachangi..timu yetu wote
Zimepatikana Mil 351.

Haya sema lingine kuwa hazitotosha kulipa mishahara ya wachezaji wa Yanga SC.
 
Bundi wa maisha magumu ameendelea kuzunguka katika mitaa ya Jangwani baada ya wachezaji wake kuanza kulalama chinichini kwamba mshahara sasa umefikia miezi minne.

Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi minne sasa, jambo ambalo limewafanya waanze kulalamika.

"Kabla ya kwisha kwa ligi, tuliambiwa tupambane kubeba ubingwa. Mambo yatakuwa safi, lakini naona hali si nzuri hadi sasa.

"Mwisho wa mwezi huu (Mei), itakuwa miezi minne. Mmekuwa mkisema hatujitumi, hatuvumilii. Basi sasa mtutetee, maana miezi minne mingi ndugu zangu na sisi tuna familia," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wakikubali kwamba mishahara imekuwa tabu na baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji, mambo yamezidi kuwa mabaya zaidi.

Wachezaji hao walipambana mwishoni bila ya mishahara hadi kufanikiwa kufikisha pointi 68 zilizowapa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.

Chanzo: Salehe Jembe
Yanga gani, hii bingwa wa ligi kuu? Na ile check ya voda unadhan iliandikwa tuu zile namba?

Au hii post ya mwaka gani jaman
 
Ukisoma tu habari hii huku ukiwa unapima credibility yake kuna chembe ya shaka inayokuingia akilini haraka haraka.

Msalimie Saleh Jembe, ila mkumbushe kuwa tumekwisha Utawala hauna ukata wa kutowalipa salary players ukizingatia Klabu ipikusanya takribani Mil 351 Kwenye mchango uliofanyika last month.

Pia wachezaji wamelipwa pesa za pongezi za kubeba Ubingwa.....

Wengi wako likizo wanakula bata hivi sasa!
mkuu hongera kuwakata ulimi
 
Asante sana
 
Back
Top Bottom