Wachezaji waomba msamaha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachezaji waomba msamaha

Discussion in 'Sports' started by Mkora, Mar 13, 2009.

 1. M

  Mkora JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wachezaji wa taifa stars wavunja ukimya kupitia globu ya jamii
  KILICHOTOKEA IVORY COAST KATI YETU (HARUNA, ATHUMAN, KEVIN, BONI, AMIR, NURDIN) NA KOCHA MARCIO MAXIMO
  UTANGULIZI

  Kwanza kabisa tunatoa pongezi kwa mtandao huu wa jamii na Tunaomba balozi utufikishie haya tulionayo kwa jamii ya watanzania wote.

  Katika maelezo yetu haya tutaeleza kila mmoja ya walioandikwa hapo juu kilichomtokea kwa kituo kabla hatujaondoka na baada ya kuwa kwenye mashindano, tunafanya hivi kwa kuwa hatuna uwezo wa kuongea na waandishi wa habari ana na pia tunaogopa kama binadamu tusije tukatereza kitu ambacho kinaweza kikatuletea madhara katika shughuli zetu za kila siku (Kucheza Mpira).
  Hivyo kwa ushauri wa ndugu na jamaa zetu tukaona ni bora tutumie tovuti yetu hii ya jamii kuwaomba msamaha watanzania wote na pia kuwapa haki ya kujua nini hasa kilichotokea na pia tunaomba wanahabari watumie ujumbe wetu huu kuwafikishia habari wananchi wote wa Tanzania ili waweze kuelewa undani wa sakata zima hili na tunaomba endapo tutakacho kieleza hapa kitakuwa sio kweli atoke mbele ya jamii na kutukosoa tuko tayari kwa hilo.

  ATHUMAN IDD (Chuji)
  Itakumbukwa kuwa wakati nikiwa na timu yangu ya Yanga niliumia nyama za paja kitu ambacho kilisababisha Dakitari wa timu kushauri kuwa nipumzike wakati nikiendelea na matibabu ili niweze kupona vizuri kitu ambacho nilikifanya na nikaamua kwenda kwa mama yangu Tanga kupumzika wakati nikiendelea na matibabu.
  Siku chache baadae niliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambapo niliripoti lakini sikuweza kufanya mazoezi na timu kwa sababu ya tatizo langu la paja na hata Dakitari wa timu alithibitisha hilo, lakini baada ya muda mfupi nikaanza mazoezi mepesi pamoja na timu na mwisho nikawa sawasawa japo sio 100%.
  Muda mfupi kabla ya kwenda kwenye mashindano Kocha mkuu akaniita na kuniambia kuwa ananichukua mimi kwenda Ivory Coast kwa kuogopa kelele za watu lakini sitocheza kitu ambacho sikukielewa lakini pia sikutaka kukubali kwani niliamini naendelea vizuri na baada ya siku chache nitakuwa sawasawa 100% kwahiyo kocha ataweza kunipanga.
  Tulipofika kwenye mashindano niliongeza bidii ya mazoezi ili kumshawishi kocha kuwa niko sawasawa 100% lakini hilo halikueleweka nikaendelea kubaki benchi bila maelezo ya kujitosheleza kwanini niko benchi hasa mechi ya pili tuliocheza na Ivory coast nilikuwa niko tayari kimwili na hata kiakili kwa aslimia 100 kucheza mchezo ule lakini sikupangwa.

  HARUNA MOSHI (Boban)
  Kucheza kwenye mashindano makubwa kama yale imekuwa ni ndoto ya kila mchezaji duniani kwahiyo kupata nafasi kama ile huwa ni bahati na kila mtu huwa anajitahidi kuonyesha kiwango chake chote ili ikiwezekana apate nafasi ya kwenda kucheza mpira wa kulipwa popote duniani kwani kunakuwa na wawakilishi wa vilabu mbalimbali vya nje kuja kuangalia wachezaji wanaoweza kuwafaa.
  Siku ya mechi ambayo tulicheza na Ivory Coast nilipangwa lakini nakiri nilicheza chini ya kiwango ila tu naomba watu waelewe kuwa haikuwa hivyo kwa makusudi kwani ilikuwa ni nafasi yangu ya kuonekana hivyo ilitokea kwa bahati mbaya sana na ninasikitika kwa hilo.

  Baada ya mechi tukiwa kwenye mkutano wa wacheza kocha alinisema sana kupita kiasi (kwa karibu dk15 hivi) kitu ambacho hakikunifurahisha na kama hivyo haitoshi kwa muda wote toka siku hiyo nikawa hata nikimsalimia haitikii wala hataki kuniangalia machoni kwa kweli ni kitu ambacho kiliniumiza sana katika muda wote niliokuwa mashindanoni.

  KEVIN YONDANI
  Na mimi pia nakiri kuwa katika mechi ya kwanza nilicheza chini ya kiwango lakini kama alivyosema Boban kuwa ile ilikuwa ni jukwaa la sisi kuonekana duniani kwamba tunaweza endapo tukipewa nafasi.
  Kwa hiyo kutokana na presha ambayo kwa kweli ilinizidi nikajikuta kuwa nimepania sana mpaka nashindwa kucheza kwa kiwango kile ambacho ninakifiria kichwani kwangu.

  Baada ya mechi kwenye mkutano wa wachezaji kwa kweli hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa kocha wetu kiasi cha kushindwa hata kuvumilia na kunipa nafasi nyingi na hata kuongea au kusalimiana na mimi ilikuwa haiwezekani kitu ambacho nadhani haikuwa sawa nilistahili kupewa nafasi nyingine niweze kufanya kile ambacho kila mtu alikitarajia kutoka kwangu.

  AMIR MAFTAH
  Kwa upande wangu mimi kosa langu kubwa ni kuwa karibu na Athuman kwa hiyo na mimi nikajikuta nimeingizwa kwenye mkumbo huo, lakini ikumbukwe kuwa mimi na Athuman tumekuwa tukila na kulala pamoja toka wakati wa Serengeti Boys. Kwa hiyo n iwatu ambao yeye anapokuwa na matatizo kama haya mimi najisia angalau kumwambia neno hata moja ambalo litamfariji kwasababu ndie mtu ninemjua vizuri kuliko mtu mwingine kambini na siwezi kumtelekeza leo hasa wakati ambapo anahitaji kuwa na mtu wa karibu.
  Kwangu mimi hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana kiasi cha kutopangwa na hata kuwekwa kwenye list ya wachezaji wa akiba.

  NURDIN BAKAR
  Kama ilivyokuwa kwa Amir na mimi kosa langu kubwa ni hilohilo la kuwa karibu na Athuman na mimi pia nikaingizwa kwenye mkumbo huo, lakini Mimi, Amir na Athuman tulikuwa kulala pamoja Serengeti Boys, Simba na hata sasa Yanga kwahiyo niwatu ambao mmoja wetu anapokuwa na matatizo tunakaa kama kitu kimoja kuongea na pia ifahamike kuwa hata wazazi wetu wanafahamiana kwahiyo tunapoongea ni kama watoto wa familia moja, lakini baada ya kuona kuwa kocha hafurahii uhusiano huo nikaona wacha nijitoe kwa muda na ndio angalau nikapata nafasi ya kucheza.

  MWINGINE
  Haya yaliyotokea pia yamumuhusisha Godfrey Boni ambaye sijui ni kwanini Kocha aliamua kumuingiza kwenye sakata hili labda anaweza kueleza vizuri (Kocha) endapo akiulizwa.

  MATUKIO YA IVORY COAST
  Sisi wachezaji ambao tulikuwa katikati ya sakata hili yalitukuta yafuatayo:
  Tulitolewa kabisa kwenye Program ya mazoezi ya timu tukawa tunafanya mazoezi wenyewe pembeni (kwa wale waliokuwepo wanaweza kuwa mashahidi wa hili).

  Tulitolewa kwenye mazungumzo ya timu kwa sababu kocha alisema anataka kuzungumza na wachezaji wake tu, ikabidi sie tutoke waongee.

  Kocha alimwambia Katibu kuwa sisi asiotutaka turudshwe nyumbani ndege ya kwanza itakayopatikana kitu ambacho katibu hakukubali na hata Waziri alipoambiwa kasema yeye ndio kiongozi wa msafara kwahiyo ndie anaeamua ni nani anarudi na nani anabaki kwahiyo hakuna mtu atakae rudi nyumbani kabla ya mashindano kuisha.

  UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM
  Baada ya kufika uwanja wa ndege waziri Mkuchika alituita (Boban na Chuji) na kutuuliza kilichotokea tukamueleza yote bila kubakiza.
  Baada ya hapo tukaamua kuondoka kurudi makwetu kitu ambacho watu wengi waliona kuwa sio sawa kwa hiyo kwa ajili yao tunawaomba radhi kwa hilo lakini ikumbukwe kuwa sisi ni binadamu na yote yaliyotokea Ivory Coast yalitutesa kwa kipindi chote tulichokuwa huko tukaona hatuna hata haja ya kuwa na watu ambao hawakutaka kuwa na sisi, kifupi ni kwamba hatukutaka kuwa wanafiki na kuvaa tabasamu la plastiki.

  MWISHO
  Tunatoa shukurani zetu za dhati kwa Katibu wa TFF Frederick Makalebela na Mkuu wa msafara Mh. Muhammad Seif Khatibu wa kutumia busara ya hali ya juu wakati wote wa mtafaruku huu na tunawaambia kuwa huo ndio moyo wa kimichezo na kizalendo.
  Tunaimani endapo wakiendelea hivi basi Nchi yetu itafika mbali kwa Tanzania ni Kubwa kuliko mtu binafsi awae yeyote Yule.

  Hayo ndio yaliyotokea Ivory Coast na tunaomba mzee wa tovuti ya jamii uwasilishe kilio chetu kwa watanzania na tumeamua tutoe leo kabla ya wenzetu kuondoka kwenda mashindanoni Misri na kama kuna mtu yeyote anasema kuwa haya tuliyoandika sio kweli basi awasilishe maoni yake ili watanzania wajue mbivu na mbichi.

  Unaweza kuwasiliana na sisi kuhusu hili kwa email (KAPUNI) Ila tunaomba usiichapishe hii email address kwenye mtandao wa jamii.

  Asanteni sana
  Haruna;
  Athuman;
  Kevin;
  Amir;
  Nurdin;
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mbona sioni kama wameomba msamaha? Naona kama vile wanaelezea story kwa upande wao ili public iamue.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,477
  Likes Received: 81,763
  Trophy Points: 280
  Hli la kutoelewana na Wachezaji ni sababu nyingine ya kutomuongezea Maximo mkataba mwingine. Kuna haja ya kutafuta kocha mwingine wa timu ya Taifa. Kazi aliyoifanya Maximo inatosha na sidhani kama ana uwezo wa kuongeza lolote zaidi ya kiwango tulichofikia.
   
 4. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nionavyo mie wameomba msamaha kwa lile walilokubali kuwa ni kosa yaani kujitenga na wenzao uwanja wa ndege ama kwa kilichotokea Ivory Coast wameeleza hali ilivyokuwa ili kama wana makosa basi wahukumiwe kwa haki badala ya kusikia ya upande mmoja. Hawa wamekuja ukumbini ili wapate ushauri na maonyo kama yapo na sio kuja kulumbana.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  This is most unprofessional.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  how? b specific plz
   
 7. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuuu mbona kichwa cha habari na habari ulitoa ni tofauti kabisa??Au hiyo habari hujaisoma umecopy na kupaste tu?
   
 8. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ana uwezo mqubwa yla zengwe letu ndio linaturudisha nyuma,hawa wachezaji hapo watakapokuja gundua hii yote ni kwa faida yao itakuwa too late.wanatakiwa walearn the system kwa sababu wakati wao ukifika wao watakuwa makocha.Maximo amewasoma akagundua hawa hawaambiwi mara moja na yeye anataka kubadilisha hiyo tabia.wachezaji wetu wanataka kujifanya celebrities hadi mazoezini Maximo hana time ya kuwabembeleza wamezoea makocha wa kwetu wanavyowatreat the wrong way.Mchezaji wa ulaya celebrity akiwa mitaani anapoingia mazoezini ama uwanjani yupo kazini.
  Think Twice.


  SAHIBA>
   
 9. C

  Chuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kocha Maximo anajua Kizungu na wachezaji wetu wanaelewana nae kilugha?,,,,isije ikawa moja ya tatizo ni Hilo,,,,inabakia watu kusomana Usoni,,,,

  Bahati Mbaya ktk Timu ya Taifa pia hakuna Mtu anaeweza tibu matatizo ya Kisaikolojia,sina hakika na wenzetu wa Ulaya wanafanyaje,,,/
   
 10. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa ni nani apewe hiyo tiba ya kisaikolojia, hao wachezaji au Maximo? Wachezaji hata kama wangepewa hiyo tiba bado wasingecheza, kwa kuwa anayepanga timu ni kocha. Labda Maximo angepewa hiyo tiba ingesaidia, kwani huenda angebadilika na kuanza kuwatumia.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Of course I am taking a leap of faith in accepting that this is something bona fide, although the stupidity it takes to self incriminate in this way is way beyond the level any adult should have the misfortune to have, I would not be surpised given our collective level of education and communication skills.  -Professional soccer player anaogopa kuongea na waandishi wa habari? Huyu jabali anayeshindana na mijibaba kwenye Akifanikiwa kwenda kwenye nchi za watu ambako kuna mikataba mikubwa na sponsors itakayomtaka afanye press conferences atafanyaje? Mbona wanakuwa kama watoto na sio wachezaji wa timu ya taifa? Kuna kitu gani wanaficha?

  This is most unprofessional

  So this is about kuomba msamaha, vizuri,


  Mchezaji amekubali hayuko 100% Kocha kashamwambia kwamba anaenda lakini takaa benchi, bado mchezaji anang'ang'ania kutaka kucheza kwa tamaa yake binafsi na ego huku anajua kwamba hayuko 100% fit, hataki kumsikiliza kocha na ana nerve ya kuiambia dunia kupitia JF kwamba hakukubaliana na kocha. Timu kufanikiwa ni lazima iwe na nidhamu, kama mchezaji hawezi kumsikiliza kocha sijui kama timu inaweza kuwa na nidhamu inayotakiwa kuleta ushindi.

  Halafu watu wengine wataona kuwa hawa wachezaji wame wa snob waandishi wa habari.

  This is most unprofessional


  Huyu paragraph ya kwanza kaanza vizuri sana, na angeachia hapo ningeona kwamba kwanza yuko humble na pili ameumwa sana na kukosa ushindi mpaka ameelezea kile kisichohitaji maelezo mengi, kushindwa kutokana na kucheza chini ya form, hii inajulikana hata kina Tiger Woods wana siku zao wanachemsha.

  Lakini akaendelea kujionyesha asivyo na uzoefu.Wachezaji wetu hawana elimu ya saikolojia ya kutosha.Kwanza niseme kumsema huyu mchezaji hivi haina maana kwamba kocha hana makosa, inawezekana kocha ana makosa, lakini mchezaji kuanza kulalamika kwa sababu amesemwa na kocha kunaonyesha mchezaji huyu asivyo tayari kukosolewa. Kila kocha ana style tofauti za kufundisha, wengine wanakuwa waangalifu kuhusu sensibilities za wachezaji wao, wengine wanakuwa wanaamini katika kuwa toughen wachezaji wao "Full Metal Jacket" style.Sasa kama mtu huwezi kuchukua criticism and a little beating from the coach sijui utawezaje kupambana na mijanaume uwanjani, kama uko overly sensitive na una whine na ku bytch kama mtu ambaye hajapewa nafasi ya kuonyesha vitu vyake utakuwa unajidanganya, kocha kama amefundisha halafu mnachemsha ana haki ya kuwasema na kuwa scold.Hapa inawezekana kuna complex ya kusemwa na mtu mweupe ina play part.

  This is most unprofessional


  Either hawa wachezaji wame coordinate kumfanyia huyu kocha conspiracy (knowingly or unknowingly) or huyu kocha naye ana matatizo. Lakini kwa watu pro wanachofanya wana move on na kufanya vitu vyao uwanjani.Haya mambo ya kuanza kusemana kwenye magazeti na JF, especially is such a cowardly manner, is the height of unprofessionalism.Sasa kocha naye atajibu, waandishi wataspin, itakuwa bonge la circus.

  Hata kama wanachosema ni kweli, presentation yao mbovu.

  This is most unprofessional


  Huyu kaamua kumtosa mwenzake moja kwa moja, hivi teammate ambaye unasema umekuwa ukila na kulala naye pamoja tangu Serengeti Boys unamtosa hivi hivi? Team spirit iko wapi? Halafu kwanza unamtosa then unasema "siwezi kumtelekeza" inaonyesha upeo mdogo, saikolojia ndogo, uwezo wa kujieleza mdogo, then you wonder why we lose? Halafu visingizio tu "nimejikuta nimeingizwa katika mkumbo huo huo" mkumbo gani? Usiache vitu vina hang, unaonyesha usivyo na upeo.

  Kwa hiyo wewe unamtetea kwa sababu ni rafiki yako, not on the merit of his case, au siyo?

  This is most unprofessional


  Huyu maskini kashindwa hata kuja na kitu original, ka copy paste cha mwenzake tu na basically kasema sisi tuna vote kama block, sisi ni NATO, you attack one of us you attack all of us. Kwa hiyo naye anajitoa timu ya taifa kwa sababu ya drama zilizomkuta mshikaji wake? Hii ndiyo professionalism? Vipi kama yeye angeamua kubaki kwenye timu na kutumia ushawishi wake kumshawi wake ku broker some sort of understanding between the coach na rafiki yake?

  Naona tatizo kubwa ni ukosefu wa ukomavu na tatizo la saikolojia ndogo.


  OK, tunajua kwamba wachezaji are not necessarily the most scholastic of people, kwa hiyo sitegemei kwamba wajue kuandika sana, lakini wameshindwa hata kumpelekea counselor wao aangalie kitu walichoandika? Hii sehemu ya matukio ya Ivory Coast ilitakiwa kuja mwanzo kabisa kabla ya visingizio vyao ili tujue wakilalamika wanalalamikia nini, walichofanya wao wametanguliza ego zao ku pour malalamiko bila hata ya kueleza environment ilivyokuwa halafu baadaye wanaeleza kilichotokea.This is simply lack of judgement.

  Kuna mambo matatu nayaona.

  1. Wachezaji hawajapevuka kisaikolojia na hawawezi kuiweka timu mbele yao, hawawezi kuwa tayari kukosolewa.Mara nyingine mtu anakukosoa kwa sababu anakupenda, hata mzazi wako anaweza kukusema sana, siyo kwa sababu hakupendi au vipi, bali kwa sababu anataka ufanye vizuri zaidi.

  2. Kocha hajaijua vizuri culture ya watanzania, ili kuwasema hawa vijana inabidi awaandae, jamani mimi style yangu ni hii na hii, mara nyingine nasema sana, kwa hiyo ukiona nakusema sana, au nakupa the silent treatment (although if this is true it is not in line with the spirit of sportsmanship and most unconventional of the coach) for a min, it is not nothing personal, ni katika mambo ya kuwekana sawa.

  3. Kocha anaingiliwa sana katika kupanga timu, kiasi cha kumwambia mchezaji kuwa "mimi nakuchukua kutokana na kelele za watu tu" watu hao ni watu gani? siamini kama ni watu wa kawaida tu, inaonekana katika uongozi wa juu kuna pressure anayowekewa kocha katika kupanga timu.Pressure hii inaleta tension na inamfanya kocha asiwe na uhuru, kitu kinachosababisha zengwe na kukosa ushindi.

  4, Kuna vitu havijasemwa

  Bongo tunafungwa kwa mengi tu.
   
  Last edited: Mar 14, 2009
 12. M

  Mkora JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu sasa naomba unitafsilie kiluga chenu
  Hivyo kwa ushauri wa ndugu na jamaa zetu tukaona ni bora tutumie tovuti yetu hii ya jamii kuwaomba msamaha watanzania wote na pia kuwapa haki ya kujua nini hasa kilichotokea na pia tunaomba wanahabari watumie ujumbe wetu huu kuwafikishia habari wananchi wote wa Tanzania ili waweze kuelewa undani wa sakata zima hili na tunaomba endapo tutakacho kieleza hapa kitakuwa sio kweli atoke mbele ya jamii na kutukosoa tuko tayari kwa hilo.
   
 13. P

  PWIDA Member

  #13
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 20, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 25
  Watuelezee vizuri makosa yao, maana huku uswahili sisi tumesikia habari zenu za mibange tu.

  We umekatazwa kuvuta bange, unabeba ya kwenda kuwauzia wenzio hebu taabarisheni kama ni ya kweli hayo.

  Mashindano mchemsha period. Hizi hadithi hazitusaidii. Mnashindwa kubana kwa dakika tano tu.

  Achani mbwembwe fanyeni mazoezi mcheze mpira na hizo bange muache kabisa, kama hamuwezi ujue generation ijayo ukiwa mtazamaji ndio utaona wadogo zenu wakicheza ulaya.

  Kuvuta bange sio nidhamu, acheni bange. Mtu usipovuta bange mpira huuoni hii hatari, halafu tutegemee ushindi kutoka kwako. Acha bange wambie na wadogo zako waache kama wanataka kucheza mpira.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli! Jamaa anajaza bandwith hapa!! Habari haendani kabisa na kichwa
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mimi naelewa kwa nini Cynic anaona hawajaomba msamaha. Wachezaji wanaongea "out of both sides of the mouth" hapa wanaomba msamaha, hapa wanampiga madongo kocha, hapa wana ji excuse na mambo kibao, mradi vurugu.

  Msamaha wa kweli mtu ana acknowledge straight, no visingizio no majungu.
   
 16. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,263
  Likes Received: 4,237
  Trophy Points: 280
  Nani kaomba msamaha mbona sijaelewa?
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  NIMEWASAMEHE

  sijui wanabodi wenzangu mna maoni au hukumu gani dhidi yao?
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapo umeongea na kujaji wachezaji wetuwana viburi wanajiona amekuwama celebrity tayari wameshindwa hatakuomba msamaha kwa Kocha na kw Watanzania wote adala yake wanaandka maelezo yaliyojaa kiburi na majivuno hakuna hata point moja ndni a maelezo yao. Kumbua wakatiDavd Beckham alipoondolewa ndani ya firs 11 ya Real Madrd na mzee Capelo alikuwa mkimya na mwenye heshima baati mbaya au nzuri Capelo kawa kocha mkuu wa England na mpaka sasa anaendelea kmpnga Beckham nkwa sababu pamoja kna kutopagwa ndani ya 11 ya madrid aliendelea kumheshimu Capelo na hakujua kama Capelo atakuja kuwa kocha wa England National team. Je kama angemchukia Capelo kipindi kile angeendelea kumpanga kwenye national Team? Adabu na heshima michezoni ni kitu muhimu sana. Maximo angezewe muda ili amalizie Progam zake achana na vijana hao wasiokuwa na adabu kwa kocha wao hata kwa Watanzana kwa ujumla.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Degauche2008 hiki ndicho naongea hapo juu, inabidi wachezaji wawe na humility kidogo.
   
 20. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,263
  Likes Received: 4,237
  Trophy Points: 280
  Tatizo la hao wachezaji ni kuongea ovyo na waandishi wa habari,bora wangekaa kimya but walishalikoroga
  Mchezaji anamwabia kocha una wivu,chuki,gubu ni bora waeendelee kuchezea Simba na Yanga
   
Loading...