Wachezaji Waliopata Kuharibikiwa Wakiwa Simba SC

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Habari wana jamvi.

Kuna orodha ya baadhi ya wachezaji ambao wanatarijiwa kuacha a Simba SC. Miongoni mwa wachezaji hao ni wale ambao waliokuwa wakifanya vyema katika timu zao za hapo awali.

Simba SC imeetendeleza Tamaduni yake ya kuharibu Vipaji vya Vijana wa Kitazania, haswa kwa kuwahadaa kwa pesa pasi na kuzingatia future yao. Leo tupate nafasi ya kuwajua baadha ya wachezaji waliokuwa Moto wakiwa Yanga SC na baada ya kuhamia upade wa pili wakaharibikiwa mazima.

1. Haruna Niyonzima
Huyu mwamba alikuwa akitengeneza pacha nzuri sana na Ajibu ezi zile Makambovic anakiwasha. Mikia FC ikaonamuda muafaka umefika wa kumuharibu kijana huyu wa kiyarwanda, wakamchukua na mwisho wa siku wakafanikiwa kumuharibu hata kwenye timu yao ikafika wakati akawa hawezi kupata nafasi. Kwa bahati nzuri Yanga wakaamua kumrudisha huyu kijana ili wamuweke sawa, ikashindikaa kwa kuwa Uchawi ulikuwa umeshaota mizizi kweye kipaji cha kijana huyu wa Gisenyi kule Rwanda.

2. Gadiel Miachael
Kijana hakuwa wamoto kivile alivyokuwa Azam FC, Yaga wakaona potential yake wakaamua kumvuta. Ndani ya Msimu mmoja wa VPL dogo kaanza ku-click hadi akawa anatupia magoli. Timu ya Taifa bandika bandua ni yeye ktk ile nafasi. Simba SC wkaona ni tishio kwa kijana wao aitwaye Siphiwe. Wakakaa kikao wakaona njia pekee ni kumharibu. Kijaa bila kujua hili wala lile akaamua kujiunga nao 2019. Matokeo yake ktk muda wake wote Gadiel akiwa kwa Mikia FC amefanikiwa kucheza mechi 4 tu kati ya mechi 68 za misimu miwili ya Ligi Kuu.

3. Beo Kakolaya
Hakuna mwenye chembe ya shaka kuhusu uwezo wa Beno alipokuwa chini ya Zahera. Alikiwasha na saves za hatari hata akawa Kipa wa Kuaminika katika Yanga SC. Walimu wa Taifa Stars waliweza kuiona potential yake hadi akaitwa kama kipa namba 2 nyuma ya Manula pale Taifa Stars. Licha ya kuwa kulikuwapo na mgogoro wa kimaslahi baina yake yeye na Klabu ya Yanga SC, haikuhalalisha kitendo cha Simba kuchukua mwanya huo wa mapungufu ya kipesa ii kulenga kuharibu kipaji cha aina hii.

Beno aliondoka akiwa kwenye Ubora wake, baada ya muda mfupi akiwa pale Simba SC walifanikiwa kutimiza mpango wao na sasa wana mpango wa kumuacha Beno ili wamchukue Jeremiah Kisubi.

4. Ibrahim Ame
Mnaikumbuka ile partnership ya Coast Unio kati ya Ame & Mwamnyeto? Ndio , ni ile partneship ambao wachambuzi wengi wa soka la bongo walisema kuwa ni partnership ya backline ya Taifa Stars hapo baadaye. Basi bwana, Wale jamaa wakaona hapa ndio mahala pa kupaharibu tena, wakaweka mpango wa kuwavuta wote wawili. Kwa bahati nzuri Yanga SC wakajitokeza kuokoa kipaji kimojawapo,yaani Bakari Mwamnyeto.

Ame kwa sasa yuko katika mpango wa kuachiwa kwa mkopo kwa kuwa tangu ajiunge Simba hakuwahi kucheza mechi zaidi ya 2 ambazo amemaliza dakika 90.

5. Naona nachoka tu kuendelea kuandika hebu ongezea hapo chini jina la mchezaji ambaye alienda simba akiwa mota lakini aliachwa akiwa hatamaniki na yeyote yule.
 
6. Ibrahim Ajib
7. Miraji Athumani
8. Saidi Ndemla
9. Perfect Chikwende
10. Charles Ilanfya
Etc...
 
Kwa Beno Kakolanya ni kosa la Zahera, huwezi kumnunia mchezaji mwaka mzima utafikiri mke mwenzio. Kati ya makocha wa ajabu wa kigeni Zahera ni nambari wani.
 
Kwahiyo mnaona wameharibikiwa au wamejiunga na timu yenye wachezaji wenye viwango bora zaidi yao?.

ukweli ni kwamba mchezaji anaekaa benchi Simba akienda Yanga anaingia kikosi cha kwanza.
 
Tangu mshinde mnaandika pumba sana. Hakuna klabu isiyokuwa na wachezaji walioflop. Msimu uliopita utopolo ilisajili wachezaji zaidi ya 20 halafu ikaja kuwatema dirisha dogo zaidi ya 15. Kwa hapa bongo utopolo ndio inaongoza kukwamisha ndoto za wachezaji na shahidi ni Ngasa na Tegete.
 
Simba inaua vipi vipaji vyao....
Haina makocha wazuri?
Haina uwanja wa mazoezi, inapelekea wachezaji kutonoa vipaji vyao?
Ili mchezaji apate namba ni lazima ajitume mazoezini, hakuna kocha atakupa namba eti kwa kuwa wewe ni ajibu, na hujitumi mazoezini.
 
Gadiel Miachael

Huu uharibifu wanaoufanya mikia sio wa kuvumiliwa kabisa
Hivi shamte, junior lokosa wako wapi?,deo kanda, sharaf shiboub,
Mikia ni waharibifu sana kwa nchi
 
Kwahiyo mnaona wameharibikiwa au wamejiunga na timu yenye wachezaji wenye viwango bora zaidi yao?.

ukweli ni kwamba mchezaji anaekaa benchi Simba akienda Yanga anaingia kikosi cha kwanza.
Naona mimba imeanza kukupa kichefu chefu..
Vumilia utajifungua soon
 
...
6. Ibrahim Ajib
7. Miraji Athumani
8. Saidi Ndemla
9. Perfect Chikwende
10. Charles Ilanfya
Etc...
Huyu dogo Charles Ilanfya alikuwa moto sana pale KMC. Uchawi umemuharibia Career yake.
Tangu mshinde mnaandika pumba sana. Hakuna klabu isiyokuwa na wachezaji walioflop. Msimu uliopita utopolo ilisajili wachezaji zaidi ya 20 halafu ikaja kuwatema dirisha dogo zaidi ya 15. Kwa hapa bongo utopolo ndio inaongoza kukwamisha ndoto za wachezaji na shahidi ni Ngasa na Tegete.
Kunatofauti kati ya kusajili flop na ukashindwa kumkuza akawa bora & Kusajili mchezaji aliye kwenye form yake na ukashindwa kumfaya awe bora zaidi.
 
Simba wana usajili wa aina tatu.

Wa kwanza ni kwa ajili ya mahitaji yao halisi kama timu (Chama nk.)

Wa pili nk kuikomoa Yanga ili mchezaji asiende au wamtoe Yanga (Gadiel nk)

Wa tatu ni ule wajanja kula hela ya Kanjibhai (Lukosa nk)
 
Huyu dogo Charles Ilanfya alikuwa moto sana pale KMC. Uchawi umemuharibia Career yake.

Kunatofauti kati ya kusajili flop na ukashindwa kumkuza akawa bora & Kusajili mchezaji aliye kwenye form yake na ukashindwa kumfaya awe bora zaidi.
Sarpong alikotoka hakuwa bora? Waziri junior je hakuwa bora au uchawi ushammaliza hapo utopoloni.
 
Huyu dogo Charles Ilanfya alikuwa moto sana pale KMC. Uchawi umemuharibia Career yake.

Kunatofauti kati ya kusajili flop na ukashindwa kumkuza akawa bora & Kusajili mchezaji aliye kwenye form yake na ukashindwa kumfaya awe bora zaidi.
Kuna dogo alikuwa anaitwa Yusuf Mlipili, day huyu Mimi nilikuwa namkubali Sana tangu akiwa Toto Africa, lakini sasa hata kusikika simsikii tena, Mikia washafanya yao. Nasikia na Metacha mambo yoote aliyotufanyia kiburi anakipata kwa hao Mikia. Nasikia washamsainisha contract.
 
David Kaseke na Peter Mwalyanzi waliondoka Mbeya city siku moja! Kaseke akajiunga Yanga na Mwalyanzi akajiunga Simba! Leo hii Mwalyanzi alishasahau kama aliwahi kucheza simba huku Kaseke anaendelea kukipiga katika kiwango cha juu Yanga!

Kuna mtu anaitwa Salimu Mbonde alikuwa fundi kwelikweli (simba walishampoteza) bila kusahau kipaji cha ajabu kilichopotezwa na simba Mo Ibrahimu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo mnaona wameharibikiwa au wamejiunga na timu yenye wachezaji wenye viwango bora zaidi yao?.

ukweli ni kwamba mchezaji anaekaa benchi Simba akienda Yanga anaingia kikosi cha kwanza.
Hebu tuombe radhi wananchi nakwambia omba radhi timu ya nchi pumbavu viwango hivyo vipo wapi?
 
Back
Top Bottom