Wachezaji wa Tanzania wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Ngasa

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
WACHEZAJI WA TANZANIA MNA MENGI YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA NGASA.

Na Abbas Jiriwa
Linapotajwa jina la Mrisho Khalfan Ngasa lazima liguse wadau wanaopenda mpira wa miguu. Kwani ni jina ambalo lilitikisa upande wa mpira wa miguu ukanda huu wa Africa ya mashariki. Hakuna shabiki ambae timu yake inacheza na timu ya ngasa angefurahi kumuona Mrisho ngasa akiwa yupo kwenye list ya wachezaji wanaoanza tena akiwa fiti. Nakumbuka Mrisho ngasa alishawahi kuahidi kwenye mechi moja ya watani wa jadi kwamba nisipofunga goli nachoma nyumba yangu moto na kweli ngasa alifunga goli tena la kwanza tu. Huyo ndio ngasa tuliokuwa tunamjua.

NGASA KAKOSEA WAPI?
Ukweli lazima usemwe japo utaumiza baadhi ya watu. Kilichomrudisha nyuma na kumchelewesha ngasa ni mapenzi yake kwa yanga yaliyopitiliza. Ilikuwa mpaka umtoe ngasa yanga umpeleke timu nyingine lazima utumie mbinu za kimafia kama walivyofanya azam na simba nafikiri wengi mnakumbuka.
Sehemu ya kwanza kukosea kwa ngasa ni kuipenda yanga kupitiliza na sehemu ya pili ni pale alipokataa ofa ya AL Mareik ya Sudan na kuwazimia simu pindi alipokuwa simba lengo lilikuwa arudi yanga na alienda yanga na nakumbuka alicheza kwa hasara kuliko kipindi chote alichocheza ligi kuu.
Nakumbuka mbwana samata aliwahi kuigomea simba kwenda mazoezi kisa hajapewa hela yake ya mkataba. Hiyo ilikuwa ni sahihi kwa mbwana samata kwani alithamini mpira kama kazi yake na alikuwa hataki aone inachezwa japo alikuwa na mapenzi na simba lakini hayakupitiliza kama ngasa na yanga.

KWA NINI WACHEZAJI WENGINE WAJIFUNZE KUTOKA KWA NGASA
Leo Mrisho ngasa anadhalilika kwa kutupiwa virago tena na mbeya city ambayo hata ligi kuu haiko nafasi nzuri.
Hivi kama angeenda Sudan na angejituma je leo hii angekuwa na haja ya kurudi tena bongo?
Wachezaji wengine kama mna mapenzi na timu nyingine tofauti na timu mnazochezea jaribuni kuyaficha na mfanye mpira kama kazi..
Kumbukeni Maisha ya mpira ni mafupi na hayana pensheni hivyo mkipata nafasi zitumieni.

Mimi sio mwandishi wa habari za michezo ila nimeguswa na hili.

ABBAS JIRIWA
 
Madege walimkataza asiende Lovam ya Sweden kwamba asubiri watampeleka Uingereza matokeo yake akapotea ht km alienda West ham ulikuwa ushauri mby kwenye career ya mpira wake
 
Kama kuna waliomsababishia hayo yote na wao mafanikio kwenye soka watayasikia kwenye vyombo vya habar kama Ngasa anavyoyasikia.
Kina Madega na wenzake walishindwa kumsaidia huyu kijana na kama alivyopotea ndio kama kina Madega walivyopotea pia.
 
alikosa akili...kamaaliendahadi westham akashindwa hakuna ambapo angeweza
 
Alipata timu Norway lakini Yanga wakagoma kumuuza eti dau la 50million lilikuwa dogo. Jamaa wakagoma kuongeza dau Ngasa akabaki nchini
 
Aisee...kipaji kilichopotea kwa kukosa ushauri mzuri.Yangu mrudisheni nyumbani, kwani ana mapenzi na Yebo fc..
 
Nakumbuka alifanyiwa majaribio na timu Moja ya marekani kwa bahati nzr ilikuwa ni kipindi cha MANCHESTER PRE SEASON TOUR,,, wakakutana na Manchester MAREKANI ,,, NGASA aliingia kipindi cha pili,,,, basi MAGAAZETI yote ya michezo ya bongo yalimpamba,,,, NGASA amtoa KAMASI Rio Ferdinand,,, NGASA afanya KUFURU,,, duh,, pole yake NGASA,,,
 
Jamaa Kila siku anaoa mke mpya, mpira utakuwa saa ngapi?
 
Sasa ni muda muafaka Mrisho Ngassa kuanza kujifunza ujasiliamali Na ikiwezekana aende kusoma ufundi veta, mpira Na umri vimempa kisogo
 
Hizo zote zinaweza kuwa ni sababu lakini yule Bwana Mdogo alikuwa anapenda sana wanawake nafikiri ndio sababu hasa ya kiwango chake kuporomoka kwa haraka .
 
Back
Top Bottom