Wachezaji wa Simba Wazuiwa Uwanja wa Ndege Nigeria

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,254
2,000
Huu ni mfano wa ubabaishaji katika mpira wa Bongo!

Simaba wanatarajia kucheza na Enyimba huko Aba keshokutwa katika mechi ya klabu bingwa barani Afrika.

Kuna taarifa kwamba wachezaji wawili wa klabu ya Simba; Ramazani Waso na Moses Odhiambo wamekataliwa viza kuingia Nigeria kwa sababu hawakuwa na vibali vya kufanya kazi Tanzania.

Inasemekana wote wana vibali vya zamani ambapo Odhiambo ana kibali cha timu ya Moro United na Waso ana kibali cha kuchezea Yanga ambavyo havikukubaliwa na maafisa uhamiaji wa Lagos kwa vile timu waliyokuwa wanaitegemea ni Simba.

Inasemekana wamepakiwa katika ndege inayofuata kurejea nyumbani.

Alipoulizwa kiongozi mmoja wa "fwati" kuhusu hilo, alisema Simba walikwenda kuomba vibali siku mbili kabla ya safari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom