Wachezaji wa KiTanzania UK

Ok,
Kama wiki 2 au 3 hivi zimepita, kuna mshikaji aliniambia kuna mchezaji mwenye asili ya bongo yuko Leicester City, ila hakukumbuka jina. Aliniambia jamaa ni teenager na striker mzuri.

Juzi nasoma BBC sport sehemu ya transfer rumors etc, nikaona jina la Eric Odhiambo, nikasema interesting, ngoja nione waKenya wanafanya vipi. Huko zamani, wachezaji wa Kenya walifanikiwa/jitahidi sana sana Belgium au Scandinavia.

Katika curiosity, nikaanza ku-google, na nikakuta huyu yuko linked na Tanzania (na sio Kenya). Infact wakasema ana kaka yake anaitwa Eddie. Sasa surname ni tofauti, ila kuna sehemu inasema huyu Eddie katokea Arusha. Na ukiwaangalia, wamefanana kwakweli.

Sasa, kuhusu Odhiambo, mjue kwamba kuna wajaluo waKitanzania. Musoma wapo wengi tu, hata Mwanza kuna wajaluo wanaongea kisukuma utafikiri hawana breki. Ishu sio jina. Pia kuna sababu nyingi ya mtu kucheza na majina.....hiyo topic naomba niikwepe.

Kuna hii link, ingawa ni wikepedia, but i believe this is the guy;

http://en.wikipedia.org/wiki/Eric_Odhiambo

Eddie Anaclet;
http://sw.wikipedia.org/wiki/Eddie_Anaclet

Ok, hapa sources zinasema ni m-south-Africa;
http://news.bbc.co.uk/sport1/shared/bsp/hi/football/statistics/players/a/anaclet_301005.stm
Je kuna wa-South Africa wanaitwa Odhiambo??

Hapa chini, wanasema kazaliwa Tanzania.

http://www.4thegame.com/club/chester-city-fc/player-profile/29756/eddieanaclet.html
hapa wanasema mtanzania.
http://www.soccerpedia.net/db/index.php/Eddie_Anaclet

Pia, nakumbuka wakati Kali Ongala anafanya trials Bradford, walikuwa wanasema ni mJamaica (official website yao).

In either case, kuna mshikaji alinihakikishia kuna mchezaji mwenye asili ya KiTanzania pale Leicester City.
 
interesting haya Maximo asikie na kufungua macho sasa sio azidi kutuyeyusha tuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom