Wachezaji wa Kibongo na kauli za tunamshukuru Mwenyezi Mungu nini tafsiri yake?

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu Habari zenu?

Baada ya korona naona tumerudi tena kwenye mchezo wetu pendwa wa mpira wa miguu ili tumalizie mechi zilizo baki.


Wakuu nimekuwa nikifatilia mpira wa miguu kwa muda mrefu sana kwenye ligi mbali mbali sasa kuna kitu nimekiona kwenye ligi yetu ya hapa Tanzania Kwa wachezaji wetu wa kibongo Baada ya mpira kuisha wakiwa wanahojiwa kuhusu mtazamo wao/ au chochote kile kwenye mechi usika Baada ya hiyo mechi kumalizika.

Lazima ajibu kwanza haya maneno “ tunamshukuru mwenyezi mungu au tunamshukuru mungu” kitu ambacho ajaulizwa.kwanini mungu wao wanamuingiza kwenye mpira(mchezo unachezwa hadharani kila mtu anaona)?
hiyo kauli anaweza kuitaja hata mara 3 kwenye hiyo swali aliloulizwa aijalishi kaulizwa swali gani.

Hivi kwanini wachezaji wa kibongo hawawezi kujibu maswali ya waandishi wa habari bila ya kusema Hiyo kauli ambayo ajaulizwa au ndio utamaduni wetu kwamba tu naamini sana kwenye mungu kwamba tunaimani sana? Naomba kujua kwenye hili.

Ligi zote duniani sijawahi kuona wala kusikia kila mchezaji wazawa wakiojiwa Baada ya mechi kila mechezaji lazima aseme “tunamshukuru mwenyezi mungu “

Hivi kuna nini nyuma ya kauli hii kwangu nimeona sio kawaida kwenye mchezo wa mpira kwenye ligi ya bongo ,Baada ya mechi mchezaji wa kibongo swali lolote akiulizwa lazima aseme hiyo kauli “tunamshukuru mwenyezi mungu au tunashukuru mungu” mbona ni wao wote tu lazima waseme hivyo mbona kwenye ligi zilizo endelea wachezaji wazawa wakiojiwa awasemi kauli hizo kila mchezaji hata kama wachezaji hao wakiwa walokole au watu wa swala tano?



Wakuu Baada ya kuwaambia hapa muanze kufatilia
Kuanzia leo mtajionea.

Unakuta mchezaji kwenye mechi yeye ndio alikuwa analeta Fujo kabisa mpaka unakuta mechi inataka kualibika kisa fujo zake na hata kufungiwa lakini akihojiwa utasikia “tunamshukuru mungu au tunamshukuru mwenyezi mungu”

Hapo ndio nashindwa kuwaelewa mungu gani huyo wanao mwambia hayo maneno?


Sijaona ulazima wakusema Hiyo kauli ukinzingatia hawataji ni mungu yupi ana mshukuru.au wachezaji wa kibongo wanaamini kwenye ushirikina ndio maana hawafiki kokote wanaishia hapa hapa tu bongo ? Au ndio mawazo ya kimaskini hayo? Mungu akusaidie bila ya kufanya Kazi?


Mimi na amini kwenye mungu alieumba mbingu na nchi.

Ni hayo tu wakuu.
 
lazima aseme hiyo kauli “tunamshukuru mwenyezi mungu au tunashukuru mungu” mbona ni wao wote tu lazima waseme hivyo mbona kwenye ligi zilizo endelea wachezaji wazawa wakiojiwa awasemi kauli hizo

Sio lazima tucopy magharibi kila kitu.. Hata sisi tunaweza kuwa na vitu vyetu, hata namna ya uzungumzaji pia.
 
Tanzania ni nchi huru, wote tuna uhuru wa kuabudu na uhuru wa kutoa maoni.

Kama wewe huamini katika Mungu or whatever huwezi kuwapangia watu wanaoamini kuwa hata uhai wao hadi kucheza mpira, utimamu wao mwili ni neema za Mungu wasimshukuru Mungu wao kwenye interview.

Kama umekasirika sana fanya mazoezi ukasajiliwe kwenye timu za Bongo halafu uwe unamshukuru Shetani tuone kama kuna mtu atakuingilia uhuru wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani wewe ni jinga la mwisho.. gazeti lote hilo uliloandika ndio upuuzi kama huu! Kutokutajwa kwa mungu kwa wachezaji wa ulaya kwa mujibu wako wewe ingawa sina uhakika juu hili kama ni kweli, hii haizuii wachezaji wa nyumbani kumtaja mungu... sasa wewe ulikuwa unataka iweje labda!
 
Mbona hata Kagere anasemaga "first of all i thank God"


Usipomshukuru Mungu utamshukuru nani sasa ,we unadhani dk 90 ni rahisi uwanjani,wengine wanakufa uwanjani,wengine wanaumizwa na kupata majeraha.

Sasa hata goli afunge asishukuru ?

Wachezaji gani wa nje hawashukuru mechi ikiisha hapa tukianza kusearch google evidence zipo.

Cha kukushauri umrudie Mungu
 
Mbona hata Kagere anasemaga "first of all i thank God"


Usipomshukuru Mungu utamshukuru nani sasa ,we unadhani dk 90 ni rahisi uwanjani,wengine wanakufa uwanjani,wengine wanaumizwa na kupata majeraha.

Sasa hata goli afunge asishukuru ?

Wachezaji gani wa nje hawashukuru mechi ikiisha hapa tukianza kusearch google evidence zipo.

Cha kukushauri umrudie Mungu
Mbona Messi , Ronaldo sijawahi kusikia wakitamka huo upuuzi.
 
Hahaha naona watu wamepanic kweli.. Watu weusi wanafiki sana.

Utasikia "kwanza napenda kumshukuru Mungu", wakati kabla ya mechi wameamkia makaburini au kwa mganga.

Bongo kuna mpira hapa..?? Upuuz tu
 
Nimejilipua ila imegoma...aluta continua...
20200621_182903.jpg
20200621_182410.jpg
 
Eheeee.
Sasa wakimshukuru MUNGU wewe haupendi?.
Haya wataanza kukushukuru wewe.
Mpira ni vita kuanza kucheza na kumaliza salama ni jambo la kumshukuru MUNGU
 
Back
Top Bottom