Wachezaji timu ya Yanga wagoma kufanya mazoezi

Wapi Frank Chacha?
Wapi Mzee Akilimali?
Yani hawa watu hapa ndo huwa nawapuuza.
Mi niko tayari tumpe timu Manji bure kabisa
 
WAMUONYESHA LWANDAMINA NGUVU YAO




Kocha George Lwandamina alipigwa na bumbuazi leo asubuhi baada ya wachezaji wake kugoma kuingia na kufanya mazoezi.

Wachezaji wa Yanga hawakufanya mazoezi kwa kuwa inaelezwa wanadai mishahara yao ya mwezi Novemba.

Mara baada ya wachezaji kutua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, walishindwa kuanza mazoezi.

Baada ya uchunguzi, iligundulika kwamba wachezaji hao walitaka kulipwa mishahara yao ya Novemba.
“Wachezaji hawajalipwa mishahara yao ya Novemba, hawataki kufanya mazoezi na kocha ameshindwa la kufanya,” alisema mmoja wa viongozi waliokuwa eneo hilo akithibitisha hilo na kusisitiza yeye si msemaji.

Juhudi za kumpata Katibu Mkuu, Barala Deusdedit ziligonga mwamba, kama ada simu yake huita bila ya kupokelewa hata pale anapotumiwa ujumbe kuelezwa kusaidia kutoa ufafanuzi wa jambo, huwa hajibu.

Wachezaji Yanga wamefanya hivyo ikiwa ni siku moja tokea waanze Ligi Kuu Bara hatua ya mzunguko wa pili kwa kishindo wakiitwanga JKT Ruvu kwa mabao 3-0.
Shauri zao si ajira zao, wapuuzi!
 
Hiyo ndiyo inaitwa ' collective bargain' ina nguvu kuliko bomu la nuklia, na ndiyo iliyo mkimbiza super coach morinho pale darajan
 
Wapi Akilimavi njo ulipe stahiki za wachezaji wa yanga afrika mkataba wa na TBL Umeisha Yanga Yetu Imewasaidia kambi na usajili njo umlipe hata oscar jushua tu peke yake...si uliwahi kusema una 500 million za usajili
 
Hapo wameshikwa pabaya maana wasipowalipa tu wanauza mechi na hapo ndipo mnyama anapowaacha... mwakani mchangani panawahusu Kufa kufaana
 
eml
Tumeshamlipa. Umeshakwenda kupiga magoti.? Wenzako wameshakusanyika klabu unangojewa wewe tu.Mazoezi ya kupiga magoti karibu yataanza. Mzee Rashid Matunda alichangangisha maharage na unga wachezaji wale. Sijui safari hii mtachangisha nini?Bora mpige magoti.
Mmemlipa lini yule mama hadi Leo anawalani kwa pesa yake ya chapatu kama familia ya marehemu Mafisango pesa ya rambirambi na ndio maana amfanikiwi kwa kudhurumu watu
 
DUNIANI KOTE MPIRA NI BIASHARA HAYA WEWE AKILIMALI LETE MAJINI YAKO TULIPE MSHAHARA
Mimi ni Simba lakini kwa hili nashauri Yanga wavamie kwa Akilimali wakidai awalipe wachezaji ili liwe funzo kwa watu kama Kilomoni. Mi najua Manji kafanya makusudi ili Yanga wajue umuhimu wake
 
eml

Mmemlipa lini yule mama hadi Leo anawalani kwa pesa yake ya chapatu kama familia ya marehemu Mafisango pesa ya rambirambi na ndio maana amfanikiwi kwa kudhurumu watu
Jifunze kuandika kiswahili
Chapatu
Anawalani
Kudhurumu
Halafu rudi ujaribu tena kuandika unachokusudia. Sio wote wanaelewa kilugha.
 
Jifunze kuandika kiswahili
Chapatu
Anawalani
Kudhurumu
Halafu rudi ujaribu tena kuandika unachokusudia. Sio wote wanaelewa kilugha.
Heri yako wewe mswahili ila nashangaa mswahili gani anaipenda Simba au ulikuwa mfanyakazi wa Ramesh Patel
 
Back
Top Bottom