Wachezaji timu ya Yanga wagoma kufanya mazoezi

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,126
2,000
WAMUONYESHA LWANDAMINA NGUVU YAO
Kocha George Lwandamina alipigwa na bumbuazi leo asubuhi baada ya wachezaji wake kugoma kuingia na kufanya mazoezi.

Wachezaji wa Yanga hawakufanya mazoezi kwa kuwa inaelezwa wanadai mishahara yao ya mwezi Novemba.

Mara baada ya wachezaji kutua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, walishindwa kuanza mazoezi.

Baada ya uchunguzi, iligundulika kwamba wachezaji hao walitaka kulipwa mishahara yao ya Novemba.
“Wachezaji hawajalipwa mishahara yao ya Novemba, hawataki kufanya mazoezi na kocha ameshindwa la kufanya,” alisema mmoja wa viongozi waliokuwa eneo hilo akithibitisha hilo na kusisitiza yeye si msemaji.

Juhudi za kumpata Katibu Mkuu, Barala Deusdedit ziligonga mwamba, kama ada simu yake huita bila ya kupokelewa hata pale anapotumiwa ujumbe kuelezwa kusaidia kutoa ufafanuzi wa jambo, huwa hajibu.

Wachezaji Yanga wamefanya hivyo ikiwa ni siku moja tokea waanze Ligi Kuu Bara hatua ya mzunguko wa pili kwa kishindo wakiitwanga JKT Ruvu kwa mabao 3-0.
 
kabotis

Member
Jul 21, 2016
38
95

Acheni kuandika taarifa ambazo una uhakikaas.chezeaYanga baba lao
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Pitisheni kikapu cha mchango. Mlichanga maharage enzi za Rashid Matunda mtashindwa mishahara. Desemba nayo hiyo inamalizika.
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Pigeni magoti kama kawaida yenu. Bila hivyo mtaadhirika. Kila goti litapigwa mishahara ilipwe.
 
Ngarna

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,969
1,500
Habari ya mujini ni mishahara. Kipindi cha sikukuu hiki. Unafikiri nani anataka ujinga. Lipeni wachezaji mishahara yao.
 
7ve

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
907
1,000
Nipo pamoja nao bora waendelee kugoma tu mpaka ligi iishe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom