Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Pale Mtibwa Sugar, kuna nahodha kiongozi Shaban Nditi. Amecheza soka la kiwango cha juu kwa muda mrefu bila kuchuja. Amedumu sana kwenye soka la ushindani hapa Bongo.

Ukifika kwenye kikosi cha Kagera Sugar wanankurukumbi, utakutana na George Kavila Master. Ni karibia miaka 20 sasa anacheza ligi kuu ya Tanzania. Ni moja kati ya wachezaji wakongwe na wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja.

Lakini habari ni tofauti kwa baadhi ya wachezaji wengine. Kuna wachezaji wa kibongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kabisa katika ramani ya soka.

Leo, tujikumbushe list ya wachezaji hao.

Mimi naanza na hawa wafuatao...
Rashid Gumbo

Said Bahanuzi

Jerry Tegete

Endelea na wewe...

Sent using Jamii Forums mobile app
Jery Tegete mbona bado yupo anacheza ligi kuu
 
Kuna Moris waliwika Tz prison, Yanga akafail
Huyo ni Harry Morris, kaka yake alikua anaitwa Oswald Morris. Oswald alichezea tz prisons kwa mafanikio mpaka akapewa cheo cha captain na jeshi la magereza, japo Simba na Yanga walimtaka sana lakini aliwagomea. Harry yeye alipohama basi na nyota yake ikafa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni Harry Morris, kaka yake alikua anaitwa Oswald Morris. Oswald alichezea tz prisons kwa mafanikio mpaka akapewa cheo cha captain na jeshi la magereza, japo Simba na Yanga walimtaka sana lakini aliwagomea. Harry yeye alipohama basi na nyota yake ikafa

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu kwa kumbukumbu, ilinipotea kidogo
 
Back
Top Bottom