Wachezaji 13 wa Eritrea Waomba Hifadhi ya Ukimbizi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachezaji 13 wa Eritrea Waomba Hifadhi ya Ukimbizi Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jul 13, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Wachezaji 13 wa Eritrea Waomba Hifadhi ya Ukimbizi Tanzania

  Wachezaji 13 kati ya 26 wa timu ya kandanda ya Red Sea ya Eritrea walitokomea kusikojulikana baada ya kushiriki kombe la Kagame Castle Cup, wamejisalimisha katika Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam na kuomba hifadhi ya ukimbizi.

  Msemaji wa Wizara Isaac Nantanga ameeleza kwamba hivi sasa wachezaji hao wanafanyiwa mahojiano na Idara ya Wakimbizi Wizarani humo kabla uamuzi wa nini cha kuwafanya haujatolewa, "Mahojiano haya ya awali yanafanywa ili kujua sababu zilizowafanya wachezaji hao kutorejea kwao na kama sababu hizo zinaweza kuwapa sifa ya kupewa hadhi ya ukimbizi kufuatana na sheria za kitaifa na kimataifa... "Wakati wakiwa hapa nchini wechezaji hao wanahifadhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na hati zao za kusafiria zinashikiliwa na Idara ya Uhamiaji", alisema Bw. Nantanga.

  Wachezaji hao hawakujulikana walipo tangu juzi wakati timu yao ilipokuwa inajiandaa kuondoka kurejea makwao, baada ya kutolewa na timu ya Yanga katika robo fainali ya mashindano hayo.

  Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, liligundua kukosekana kwa vijana hao baada ya kujikuta wakiwa na hati za kusafiria 13 wakati msafara wa kuelekea uwanja wa ndege ulipoanza, ndipo wakatoa taarifa kunakohusika na msako ukaanza.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa wajanja sana wanatafuta nafasi ya kwenda ulaya tena safari yao inaweza kuanzia hapa Tanzania kuelekea South Africa kufika huko ulaya , hizi ndio uwa njia zao hawa jamaa
   
 3. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Haya tena ,
  Ooooh bongo shida , bongo hapakaliki!!!
  Leo wenzenu wanapaona bongo fresh.
   
 4. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  duu, wanazamia bongo. aiseee
   
Loading...