Wachawi wanaweza kuzika vitu vya mtu aliye hai?

MGOGO27

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
459
217
Nimesikia kwamba uwezekano wa wachawi /washirikina kuzika vitu mfano wa nguo aina zote za aliye hai na wakamfanya aishi maisha magumu mpaka kifo?

Huku uswahilini tunaibiwa sana nguo tena mpaka za ndani sasa sijui kama zinapelekwa huko au ndo njaa sasa naomba nifahamu ukweli na kama ni kweli, utatuzi wake ni nini?

Karibuni sana wakuu mnisaidie
 
Nishatoa challenge anayeweza uchawi aniloge hapa.

Mpaka leo sijaona mtu yeyote kuniloga.

Tena nataka aniloge in a very specific way nisiwe na shaka kwamba nimelogwa.

Hahahaaaaaaa utasubiri sana!

Kuna mtu [ gfsonwin ] niliwahi kumpa hiyo changamoto nadhani karibu miaka miwili iliyopita lakini mpaka leo bado nipo napeta.

Kwa hiyo hamna kitu kabisa hapo. Utaishia kupewa vitisho hewa tu.

Hebu fikiria tu kidogo...hivi kweli kabisa unadhani kama ingekuwa inawezekana usingekuwa usharogwa mpaka hivi sasa?

Hususan ukizingatia kwa miaka yote hii ambayo umekuwa ukisema wazi kabisa kuwa uchawi haupo?
 
Jamani naomba mniweke sawa kuhusu ndondocha.

Kwa nilivyosikia ni kwamba eti mtu (aliefanywa ndondocha/msukule) anakuwa bado yupo hai labda mfano yupo kila siku nyuma ya mlango, ila mnakuwa hamMuoni ila mpo nae kila siku bila nyinyi kujua.

Ila sijui kuna mafuta/maji sijui ukipakwa usoni na wataalam/waganga/wanaoyajua hayo mambo, eti wanasema unamuona huyo ndondocha, ila anakuwa haongei.

Kwa anaefahamu, au aliewahi pakwa hayo maji sijui mafuta wanayosema, hebu njooni mje kunipa Elimu
 
Na kingine nimesikia Wahindi wana kawaida ya kutoa sadaka moja ya ndugu katika familia zao, eti wanasema wanafanya hivyo ili wafanikiwe kimaisha,

Na sadaka yenyewe huyo alietolewa sadaka anatiwa uchizi/wendawazimu/utahahira.

Eti ndio maana nyumba nyingi za Wahindi ukienda hukosi kukuta Tahira.

Hili la kukuta matahira nimeshaliona nyumba za Wahindi tena sana, ila ninachokitaka hapa, mniambie kama ni kweli.

Eti kweli Wahindi wana kawaida ya kutoa sadaka ndugu zao?
 
Nimesikia kwamba uwezekano wa wachawi /washirikina kuzika vitu mfano wa nguo aina zote za aliye hai na wakamfanya aishi maisha magumu mpaka kifo?

Huku uswahilini tunaibiwa sana nguo tena mpaka za ndani sasa sijui kama zinapelekwa huko au ndo njaa sasa naomba nifahamu ukweli na kama ni kweli, utatuzi wake ni nini?

Karibuni sana wakuu mnisaidie
Cc mlonzi mkuu wa Jf mashana jr
 
Halafu nimesikia kuna watu wataalam wa ndumba kiasi kwamba ukiwa na kesi Mahakamani, wanachotaka kutoka kwako nguo, kitu kama shati hivi, hilo shati wanaenda kulifanyia mambo yao kisha wakishamaliza, hilo shati unapewa wewe muhusika mwenye kesi, na siku ya kupanda Mahakamani wewe vaa lile shati lilofanyiwa mambo basi ukipanda Mahakamani, ujue kesi imekwisha, lazime umwage.

Manaoyajua haya mambo au mliowahi kushuhudia.

Eti kweli?

Au uzushi!
 
Back
Top Bottom