Wachawi ni balaa: Jamaa asahaulishwa siku ya kufunga ndoa apelekwa kanisani hivyo hivyo kilazima

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,413
Atakayekuambia uchawi haupo muone kama punguani sana.

Kijana mmoja mkazi wa Kilosa Morogoro amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya wataalamu wa mambo ya jadi kumsahaulisha siku yake ya kufunga ndoa.

Kijana huyo ambaye alimchumbia binti mmoja mkazi wa Mkata anayeitwa Grace alijikuta anasahau kila kitu ilipofika siku ya ndoa yake na kuchukua jembe na kuelekea shamba.

Ndoa hiyo iliyopangwa kufungwa juzi tarehe 17 mwezi huu iliingiwa na changamoto baada ya bwana harusi ambaye alikuwa amejiandaa kwa kila kitu kuamka asubuhi ya siku hiyo ya ndoa yake na kuwa amesahau kama siku hiyo anatakiwa afunge ndoa.

Alipoamka asubuhi siku ya ndoa yake akaanza kuwauliza wazazi wake kuna nini pale nyumbani kwao mbona watu wengi na kuna mishemishe nyingi?
Swali hilo liliwaacha hoi wazazi wake na baadhi ya ndugu zake.

Mwanzo walimpuuza ila baadaye wakaona kumbe yupo serious hajui kinachoendelea wakaanza kushangaa na wasijue cha kufanya.

Walipomuambia kuwa ilikuwa ni siku yake ya kuoa alishangaa sana na kusema:
"Mimi naona?
" Namuoa Mani?
"Mbona mmenishitukiza hamkuniambia mapema?
"Namuoa Grace? Kwani Grace ndio nano? Mbona mimi simjui?
"Siwezi kuoa ghafla hivyo na sipo tayari kufunga ndoa ya staili hii.

Mama yake mzazi baada ya kusikia hivyo aliangua kilio kikubwa sana mpaka akapoteza fahamu. Ndugu wakaitama kikao cha dharura ili wajadili cha kufanya.

Ndugu ikabidi wajifanye kama kweli wamemshitukiza na wakamuomba msamaha ili tu waweze kumteka ili aende kanisani ili waepuke na aibu ambayo ingewakumba.

Taarifa zikaenea kwa watu wote waliowasili pale harusini kuwa bwana harusi amesahaulishwa ndoa yake mpaka bibi harusi hamjui wakati yeye mwenyewe ndiye aliyemtambulisha nyumbani na mahali alitoa yeye mwenyewe.

Wazee wa busara walitumia hekima inayoonekana na isiyoonekana bwana Aloyce akafanikiwa kwenda kanisani na akafunga ndoa kiugumu sana na Grace bila kiongozi wa dini kujua kilichotokea.

Dunia inamambo sana na utajua hivyo mpaka yakukute.
 
Baada ya kumpa ushauri kuwa kuoa ni utumwa akili zikamrudi, ilikuwa ishafika point of no return ameshindwa kujiokoa.... avumilie tu maumivu hadi kifo kimtenganishe.

Usiku utapokwisha.
 
Back
Top Bottom