Wachawi loliondo waenda kumjaribu "babu" mwaisapile!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachawi loliondo waenda kumjaribu "babu" mwaisapile!!!!!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Alberto De, Mar 16, 2011.

 1. Alberto De

  Alberto De New Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Machi 16 mwaka 2011.
  wachawi.jpg
  Mchungaji mwenye miujiza mingi, Ambilikile Mwasapile ‘Babu‘ (pichani)yupo kwenye majaribu mazito baada ya kubainika kwamba kuna wachawi wanapima uwezo wake wa miujiza.

  Habari zinasema kuwa, Babu amekuwa akipata misukosuko mingi hasa nyakati za usiku kutokana na kujaribiwa na wachawi yeye binafsi na dawa zake.
  The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lilinong’onezwa na mmoja wa wasaidizi wa Babu (jina tunalo) kwamba mauzauza ni mengi, hasa eneo la dawa.

  “Sisi wasaidizi ndiyo tunaopata misukosuko lakini neno la Babu lina nguvu na tupo salama,” alisema msaidizi huyo kufuatia swali la mwandishi wetu lililolenga kujua changamoto za nguvu za giza zinazowakabili.

  clip_image001.jpg
  Msaidizi huyo wa Babu aliendelea: “Wakati mwingine unaenda sehemu ya dawa unakuta mtu ambaye anatoweka ghafla. Hilo ni tatizo ambalo tumeliona na Babu huwa anafanya maombi kila baada ya saa sita.

  “Hayo maombi huwa yanalenga kudhibiti nguvu za wachawi ambao wanajitahidi sana kuharibu dawa na kupima nguvu za Babu. Tunachoamini ni kwamba hawawezi kushinda kwa sababu kila kinachofanywa na Babu kinatokana na Mungu.

  “Wachawi hawawezi kushindana na Mungu. Kupambana na nguvu za Babu ambaye ni mteule wa Mungu kwa ajili ya kuokoa kizazi kinachoteseka na maradhi mbalimbali ni sawa na kudhibiti nguvu ya Mungu.”

  Msaidizi huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe kwa sababu yeye na wenzake wamekatazwa na Babu wasizungumze, alisema: “Kimsingi Babu anajua njama za wachawi lakini anazidharau.

  clip_image001.jpg
  “Anajua haziwezi kumbabaisha lakini kikubwa ambacho naweza kukithibitisha hapa ni kwamba wachawi ni wengi wanaokuja hapa.
  “Wakati mwingine tunaona hata hizo ajali zinazotokea kwenye njia ya kuja hapa (Loliondo) ni sehemu ya hila za wachawi.”

  Kwa upande mwingine, mwanamuziki maarufu nchini, Baby Madaha aliliambia gazeti hili juzi (Jumatatu) kwamba alikwenda Loliondo na alishuhudia miujiza ya wachawi.

  Babu alisema, alipofika sehemu ya kunywa dawa, alishangaa kuona mtu amekakamaa, alipomuomba msaada amshikie kikombe alitoweka.

  “Nilishtuka sana kuona mtu anatoweka lakini nilipouliza kwa wasaidizi wa Babu, walinijibu huyo huwa anakuja na kutoweka,” alisema Baby aliyedai kwenda Loliondo kumsindikiza mkwe wake (mama wa boyfriend wake).

  Aliongeza: “Wale wasaidizi waliniambia hayo ni mambo ya wachawi, nilishtuka sana. Namshukuru Mungu nimerejea Dar salama na hali ya mama mkwe inaendelea vizuri.

  “Nilirudi tangu Ijumaa iliyopita, kimsingi yule Babu anatisha, uwezo wake ni mkubwa kwa maana watu niliowashuhudia kule si mchezo.”

  “Nilirudi tangu Ijumaa iliyopita, kimsingi yule Babu anatisha, uwezo wake ni mkubwa kwa maana watu niliowashuhudia kule si mchezo.”​

  [​IMG]
   
 2. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nakushauri uitume hii mada kwenye jukwaa stahili. Otherwise, asante kwa kutujulisha!
   
 3. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sawa, naona sasa imeletwa mahala inapostahili. Thanks Mod for your effectivity!
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Inatakiwa hao wachawi wakamatwe hadharani
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280

  Kwenye red unataka kutuambia nini au umeona ukiandika ni gazeti la Risasi hutapata wachangiaji.
  Kajifunze upya kudanganya umejiunga juzi leo tu unachanganya madesa

  Alberto De
  Join Date : 14th March 2011
  Posts : 2
  Thanks 0Rep Power : 0
   
Loading...