Wachangie CCM Wenzangu, CHADEMA haiwahusu.

leroy

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,589
2,140
Kidumu chama cha Mapinduzi.

Ndugu Makada wenzangu, kama mjuavyo siku zinazidi kupepea na mwaka 2015 ndio huo unatunyemelea kwa kwasi.

Hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu ni shwari licha ya changamoto za hapa na pale tunazokumbana nazo, mathalan kutokana na udhaifu wa baadhi ya wadau tuliowapa jukumu la kuendesha serikali.

Nadhani imefika wakati tuanze KUANDAA mazingira mazuri ya atakayepokea kijiti cha Urais 2015. Hii haimaanishi kwamba kuacha kuwatumikia wananchi na kutekeleza ilani ya chama la hasha, ni sehemu ya mchakato.

Kwa maoni yangu nadhani hakuna mtu tunayepaswa kumuachia kijiti zaidi Lowassa. Nchi yetu inahitaji mtendaji atakayesukuma gurudumu kwa ustadi na kasi pasipo kuhatarisha umoja wetu. Nadhani tumfariji na kumpa ushirikiano ktk kipindi hiki kigumu anachopitia ili kuitimiza azma hii.

Wenu,

Kada.
 
Haya ndiyo matatizo ya kunywa kimpumu mchana kama lunch. Hata hivyo nakushukuru kwa kukiri "Udhaifu" kwenye uendeshaji wa serikali
 
wananchi watatuuliza HUYU SI FISADI ALIYEIBA KUPITIA RICHMOND? tukiwambia HAPANA watatuuliza kwanini tulimvua uwaziri mkuu, tukijibu NDIYE watatupiga mawe

Hakuvuliwa uwaziri mkuu, alijiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji. Ndio maana anaitwa WAZIRI MKUU MSTAAFU. Nadhani kuna haja ya kuliweka wazi suala la richmond ili wananchi kiundani ni nani aliyehusika.
 
Haya ndiyo matatizo ya kunywa kimpumu mchana kama lunch. Hata hivyo nakushukuru kwa kukiri "Udhaifu" kwenye uendeshaji wa serikali

Ni vema ungebainisha mwelekeo wako kwanza...
 
Hakuvuliwa uwaziri mkuu, alijiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji. Ndio maana anaitwa WAZIRI MKUU MSTAAFU. Nadhani kuna haja ya kuliweka wazi suala la richmond ili wananchi kiundani ni nani aliyehusika.

Hivi wewe unajua kiswahili?! unasema kwamba ALIJIUZULU halafu unasema anaitwa waziri Mkuu MSTAAFU. Hivi huko kwenu neno KUJIUZULU lina maana sawa na KUSTAAFU? Kamusi yangu ya TUKI inaonesha maneno haya mawili yana maana tofauti.
 
Taifa linamtambua kama waziri mkuu mstaafu...tusishindane kiswahili.
 
Hakuvuliwa uwaziri mkuu, alijiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji. Ndio maana anaitwa WAZIRI MKUU MSTAAFU. Nadhani kuna haja ya kuliweka wazi suala la richmond ili wananchi kiundani ni nani aliyehusika.
tukiwambia hivi maswali yatazidi, watauliza kama yeye si mwizi na anawajua wezi kwanini alikubali kujiuzulu? Kwanini hajawataja wezi mpaka leo?
 
Huwezi kuendelea kukaa madarakani na tuhuma.
Hajawataja kwa sababu ya kulinda umoja wa chama na taifa. ​Hata hivyo tunao muda wa kutosha kusafisha hili mbele za wananchi.
 
Kidumu chama cha Mapinduzi.

Ndugu Makada wenzangu, kama mjuavyo siku zinazidi kupepea na mwaka 2015 ndio huo unatunyemelea kwa kwasi.

Hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu ni shwari licha ya changamoto za hapa na pale tunazokumbana nazo, mathalan kutokana na udhaifu wa baadhi ya wadau tuliowapa jukumu la kuendesha serikali.

Nadhani imefika wakati tuanze KUANDAA mazingira mazuri ya atakayepokea kijiti cha Urais 2015. Hii haimaanishi kwamba kuacha kuwatumikia wananchi na kutekeleza ilani ya chama la hasha, ni sehemu ya mchakato.

Kwa maoni yangu nadhani hakuna mtu tunayepaswa kumuachia kijiti zaidi Lowassa. Nchi yetu inahitaji mtendaji atakayesukuma gurudumu kwa ustadi na kasi pasipo kuhatarisha umoja wetu. Nadhani tumfariji na kumpa ushirikiano ktk kipindi hiki kigumu anachopitia ili kuitimiza azma hii.

Wenu,

Kada.

Nyie ni manyang,au tena yale mamakubwa. Tutakutana 2015. Safari hii hata kwa silaha tutapigana.
 
Kidumu chama cha Mapinduzi.

Ndugu
....Hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu ni shwari licha ya changamoto za hapa na pale tunazokumbana na
udhaifu
wa baadhi ya wadau tuliowapa jukumu la kuendesha serikali.

Wenu,

Kada.

Afadhali sana kama hilo neno dhaifu linawaingia akilini vizuri
 
Back
Top Bottom