Uchaguzi 2020 Wachangiaji wa DW wanasema Tundu Lissu atatoa changamoto kali kwa Rais Magufuli

Luqman Malotto, Khalifa Said, Gwandumi Mwakatobe na Godlisten Malisa wanachambua vizuri matukio ya kisiasa yaliyojitokeza baada ya kushambuliwa kwa Tundu Lisu lakini nadhani wangechanganya watoa maoni/wachambuzi wenye mitazamo tofauti kidogo kwani katika wote hao angalau Mwakatobe ndio unawez kumuita yupo neutral katika itikadi za vyama

Jambo la kufurahisha ni kwamba wote wamelaani kitendo cha kushambuliwa Lisu na kuwalaani wote waliohusika kupanga, kutekeleza na hata kuunga mkono ukatili huo

Hawa DW mfumo wao wa mijadala ni mzuri sana sio kama BBC. Wanamuacha mchangiaji aongee na kujenga hoja yake bila kumkatisha. Mwenyekiti Mohamed Khelefu anaendesha mjadala kwa weledi sana
Mmenikumbusha watu wasiojulikana wa awamu ya 5
 
Nimependa mawazo ya mchangiaji anasema Kwa miaka mi 5 serikali imezuia wapinzani kufanya siasa wakati huo vyombo vyote vya habari vinaripoti yale mazuri tuu yanayofanywa na serikali. Hivyo kipindi cha kampeni ndio muda muafaka kwa wapinzani kuibua na kuonesha changamoto zinazotukumba na jinsi gani serikali imeshindwa tatua changamoto kibao. LISSU FOR PRESIDENCY
Mje na takwimu maana hizi si zama za uropokaji..mkishushwa kwenye majukwaa msimlaumu mtu
 
Hiyo heading yako pekee kwa mtu asiyejua kabisa chochote kuhusu siasa za Tz tayari anajua mshindi ni nani.
 
Akili za bavicha na bawacha wanazijua wenyewe eti wanajipa matumanini kabisa ya kushinda uchaguzi ??? .

Haya sisi CCM tunasema hivi tunaingia kwenye uchaguzi tayati tukiwa tuneshinda uchaguzi ngazi ya Urais hakuna namna tutashindwa uchaguzi asimamishwe Lissu, Mbowe, Nyalandu, sijui Membe hakuna ambaye anaweza kufikisha angalau thelusi moja ya kura zote atakazozipata Mh Magufuli.

TUNAENDA KWENYE UCHAGUZI KUTAFUTA NINJ?
Tunaenda kwenye uchaguzi kuhakikisha tunashinda majimbo yote Tanzania bara na visiwani na kuhakikisha tunaongoza Halmashauri zote 184 Tanzania bara.

Sasa Kama kuna mtu anafikiri tunafanya mashala naomba tukutanae tarehe 28/10/2020 tuwafundishe hawa jamaa kwanini mtoto hakui kwa baba ba mama.
Jecha,jecha,jecha,jecha,jecha,jechaaaaaaaaaaaaa.
Tume,tume,tume,tume,tume,tumeeeeeeeeeee.
 
Chadema wasipompitisha Lissu watakuwa wamejichimbia kaburi wanachama, wapenzi na washabiki wao wengi WATANYUTI. Nyalandu siyo kabisa wa kupeperusha bendera ya Chadema.

Idhaa ya Sauti ya Ujerumani(DW) unaendelea LIVE. Wachangiaji wanasema Tundu Lissu atatoa changamoto Kali kwa Rais Magufuli.
Mbali na sifa ya SHAMBULIO LA JARIBIO LA MAUAJI ambalo limemjenga Tundu Lissu bado ana sifa nyingine lukuki za kumbeba ikiwemo umahiri wake KISHERIA kama Wakili na mchango wake katika kutetea MADINI YA WATANZANIA yasikwapuliwe na Wawekezaji Uchwara...!!

http://dw.audiostream.io/dw/1002/mp3/64/dw-radio-english
 
Kuna kitu hujui kuhusu ku analyise budget naomba nipe data za bajeti ya maendeleo imetimizwa kwa kiasi gani?

Pesa nyingi walikuwa wakijaza kwenye miposho ya vikao , seminar na makongamano .Kazipunguzav pesa zimerudi serikalini kufanya mambo mengine ya maendeleo usisome budget Kama bwege fanya analyisis nineneo lipi katika hiyo asimia 50 limechangia bajeti isi perform asilimia 100 utagundua sababu kuj Ni hizo pesa zisizo za miradi ya maendeleo.Go back to school
Hivi hapa umeandika nini,? Kwani hizo budget zilikuwa zinaandaliwa na serikali gani na huyo magu alikuwa anaongoza serikali gani? Wewe kweli ni utopolo
 
Sisi hatumtaki rais mwenye pesa za w
Hawajielewi mfano sisi CCM tulimptisha si kuwa akampe changamoto mgombea yeyote wa Cham a chochote Bali tunayeamini ataisimia na kuitekeleza ilani ya CCM

Lisu kumtuma eti akampa changamoto Magufuli mumeshindwa siasa tayari

Kwa Chadema anayeonyesha wazi kuelewa akiteuliwa atasimamia Nini Ni Nyalandu tu yuko organized, focused na ana hadhi ya muonekano wa kiraisi kuanzia lugha yaki staarabu na Wasifu wake umejaa barabara maeneo yote kuanzia kiuchumi ,kisiasa ,kimaadili,kidini na uwezo wa kumchukulia a na watu wote ndani na nje ya Chadema.Ni rafiki wa kila mtu Hana adui yeyote ndani na nje ya Chadema.Ana siasa za kushindanana kwa hoja Sio matusi na kejeli kwa yeyote au chama chochote

Ana pesa za kuendesha kampeni bila kubebesha mzigo chama au wanachama tofauti na Lisu ambaye alianza Kuomba kuchangiwa pesa Hadi za kuchukua fomu
Hatumtaki Rais mwenye pesa zilizopatikana kwa njia yenye kutia shaka.
Tunamtaka mgombea maskini mwenye uwezo wa kutuongoza hata kama tutamchangia kwa wiki zote za kampeni. Tunamtaka LISSU.
 
Nimekupata ndugu yangu, nashukuru mno kwa maoni na ushauri wako mzuri. Umekomaa sana kiutu na kifikra. Ubarikiwe sana!
Luqman Malotto, Khalifa Said, Gwandumi Mwakatobe na Godlisten Malisa wanachambua vizuri matukio ya kisiasa yaliyojitokeza baada ya kushambuliwa kwa Tundu Lisu lakini nadhani wangechanganya watoa maoni/wachambuzi wenye mitazamo tofauti kidogo kwani katika wote hao angalau Mwakatobe ndio unawez kumuita yupo neutral katika itikadi za vyama

Jambo la kufurahisha ni kwamba wote wamelaani kitendo cha kushambuliwa Lisu na kuwalaani wote waliohusika kupanga, kutekeleza na hata kuunga mkono ukatili huo

Hawa DW mfumo wao wa mijadala ni mzuri sana sio kama BBC. Wanamuacha mchangiaji aongee na kujenga hoja yake bila kumkatisha. Mwenyekiti Mohamed Khelefu anaendesha mjadala kwa weledi sana
 
Anacho takiwa Lssu kufanya ni kwenda kansani na kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu. Pia auachie moyo wake. Asamehe yote yaliyo mkuta Mungu ata mlipizia.
Aache kulaumu ajfanye kama hajatokewa na lolote. Asimtaje JPM kwenye mdomo wake kila wakati. Maana wateule wake Jpm wanamtafuta asigombee urais. Wanajua ni moto kwa baba yao. Ila Watanzania wana akili na moyo wa huruma. Lissu nenda kanisani na sadaka yako kwa Mungu utaona miujiza inayo kwenda kutokea kwa maadui zako.
 
Ndagha fijo kikolo! Kwa faida ya wengine ninamaanisha "ahsante sana ndugu yangu". Tuendelee kuombeana heri na ustaaratibu wa kiutu. Aidha, tuzidi kuwasiliana na kupeana mawazo ya kujengana kifikra
Ninakushukuru sana Kaka yangu Gwapo Mwakatobhe kwa ushauri ulioutoa kwa Tundu Lissu leo wakati ukichambua kupitia DW.

Umeshauri vizuri sana, lakini najiuliza ni namna gani ushauri huu utamfikia Lissu huko alipo.
Umesema
1. Asirudie kuwasema wale waliotaka kumuua kwa sababu atawapa umaarufu, ni sahihi kabisa atakuwa kama anawatukuza kwa uovu wao
2. Aende akawashukuru watu waliokuwa wanakesha kumuombea ili mungu amponye na pia akawashukuru wale wote waliodiriki kumtembelea kwenda kumjulia hali huko haspitali akiwemo makamu wa Raisi Samia Suluhu Hassan na Mzee Mwinyi
3. Aweke mkakati wa kuwepo maridhiano atakapokuwa ameapishwa kuwa raisi maana hili halikwepeki. Tutampigia kura na atashinda tu (tumechoka na maigizo ya kitapeli)

Umeongea mengi kama ulikuwa umeandika naomba uyaposti hapa yatatusaidia sana huko tuendako. Posti huku JF maana ukimpelekea live utatengeneza maadui kutoka kile chama cha wenye visasi. Nasema hivyo home boy hawa wa kijani tunaishi nao kinafiki. Ukweli hatuwependi hata kuwaona tu. Wengine tunatamani itokee mapinduzi ili hicho kikundi kipigwe marufuku kama ilivyopigwa marufuku NAZI ya Ujerumani enzi Hitler.

Tunashukuru sana. Na nimefurahi mno.

Hongera poti
 
Ndagha fijo kikolo! Kwa faida ya wengine ninamaanisha "ahsante sana ndugu yangu". Tuendelee kuombeana heri na ustaaratibu wa kiutu. Aidha, tuzidi kuwasiliana na kupeana mawazo ya kujengana kifikra
Nimekuelewa kikolo, muda mrefu nimekuwa nafuatilia mijadala yenu na huwa nafurahi sana unapokuwa miongoni mwa wachangiaji. Big up and keep it up.
 
Anacho takiwa Kisdu kufanya ni kwenda kansani na kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu. Pia auachie moyo wake. Asamehe yote yaliyo mkuta Mungu ata mlipizia.
Aache kulaumu ajfanye kama hajatokewa na lolote. Asimtaje JPM kwenye mdomo wake kila wakati. Maana wateule wake Jpm wanamtafuta asigombee urais. Wanajua ni moto kwa baba yao. Ila Watanzania wana akili na moyo wa huruma. Lissu nenda kanisani na sadaka yako kwa Mungu utaona miujiza inayo kwenda kutokea kwa masdai zako.

Sina imani sana na makanisa haya. Nafikiri sadaka nzuri ni kumpelekea mgonjwa asiyejiweza. Na kuna watu wengi sana wana matatizo makubwa wanaitaji misaada ya hali na mali. Kuna wagonjwa wamekosa pesa ya matibabu, fuatilia vipindi vya ushauri wako kila jumapili saa mbili ahsubuhi RFA kinachoendeshwa na Rebecca Molesi au saa nane mchana jumapili clouds FM kinachoendeshwa na doctor Isaac Marlow.

Makanisani kule ni ofisi za watu na wamewekeza huko. Sishauri sana sadaka za makanisani.
 
Umenena ukweli mtupu!

Labda kwa Gwajima. Ila nenda Catholic, nenda Lutheran, nenda Anglucan, nenda SDA, NK. Usikie nguvu za Mungu. Wacha maneno mzee. Nimeshauri maana nimeona nguvu za Mungu kupitia sadaka ya madhabahuni mwa Bwana
 
Sawa, lakini TL hatakuwa mgombea wa CDM, labda CUF ya lipumba. CHADEMA game ishasukwa zamani, na watakaompigoa kura Nyalandu weshatatarishwa na team mbowe. TL ameambiwa nyote mnatokea Singida, mshindane kwenye Box la Kura. Waafrika wote wezi wa kura
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom