Uchaguzi 2020 Wachangiaji wa DW wanasema Tundu Lissu atatoa changamoto kali kwa Rais Magufuli

Labda hukumsikiliza vizuri Luqman Maloto aliyoyataja kuwa ni madhila na mateso aliyopitia TL! Mimi nitaendelea kuwasamehe na kuwapuuzia mbali watesi na/au maadui wangu kadri nitakavyojaaliwa kuishi. Hakuna mwisho wa kusamehe, kuridhiana na kupatana maana watu hatuachi kukosea na kukosana!
Mkuu Wangu nilimsikiliza vyema Luqman Maloto na kutosikia Mateso ya Lissu Nje ya taaluma yake ya uwakili,Katika siasa na ya Kushambuliwa na maharamia anyway kusamehe ni Jambo la mwisho Lililo bora kwa kila mja duniani kwa Maana safari Yetu indefu mno.

Lissu anapowasamehe WATESI wake waliomshambulia kikatili Haina Maana ya kuwa anawajua kuweza KUWAOMBA appointment ya kukutana nao wakaongee hata yasiyohusu shambulio lile.

Lissu hawafahamu WATESI wake hao Kama ambavyo umekiri huwafahamu sambamba na sisi maamuma huku mitaani tusivyowafahamu.

Kitabaki kuwa ni kitendawili mpaka hapo kitakapoteguliwa KITAALUMA nje ya HISIA hasi ama chanya.
 
Wanachotakiwa wajue suala la shambulio la lissu sio kitu cha ajabu duniani ndio maana hata wazungu hawashikii kidedea sababu dunia ilishawahi kushuhudia shambulio dhidi ya rais wa dunia John Kennedy.

Nchi zilizoendelea zinajua fika dunia inaongozwa na kanuni zake.
Kwa maana yako wewe, likitokea shambulio ni sawa tu, hata Rais wko akishambuliwa ni sawa?
 
Hawajielewi mfano sisi CCM tulimptisha si kuwa akampe changamoto mgombea yeyote wa Cham a chochote Bali tunayeamini ataisimia na kuitekeleza ilani ya CCM

Lisu kumtuma eti akampa changamoto Magufuli mumeshindwa siasa tayari

Kwa Chadema anayeonyesha wazi kuelewa akiteuliwa atasimamia Nini Ni Nyalandu tu yuko organized, focused na ana hadhi ya muonekano wa kiraisi kuanzia lugha yaki staarabu na Wasifu wake umejaa barabara maeneo yote kuanzia kiuchumi ,kisiasa ,kimaadili,kidini na uwezo wa kumchukulia a na watu wote ndani na nje ya Chadema.Ni rafiki wa kila mtu Hana adui yeyote ndani na nje ya Chadema.Ana siasa za kushindanana kwa hoja Sio matusi na kejeli kwa yeyote au chama chochote

Ana pesa za kuendesha kampeni bila kubebesha mzigo chama au wanachama tofauti na Lisu ambaye alianza Kuomba kuchangiwa pesa Hadi za kuchukua fomu
Kwani umeambiwa Chadema ndo imemtuma Lissu kumpa changamoto magufuli? Kumbuka Chadema bado haijateua mgombea wake
 
Idhaa ya Sauti ya Ujerumani(DW) unaendelea LIVE. Wachangiaji wanasema Tundu Lissu atatoa changamoto Kali kwa Rais Magufuli.
Mbali na sifa ya SHAMBULIO LA JARIBIO LA MAUAJI ambalo limemjenga Tundu Lissu bado ana sifa nyingine lukuki za kumbeba ikiwemo umahiri wake KISHERIA kama Wakili na mchango wake katika kutetea MADINI YA WATANZANIA yasikwapuliwe na Wawekezaji Uchwara...!!

http://dw.audiostream.io/dw/1002/mp3/64/dw-radio-english

Hiyo link ya audio sijui ni lugha gani hiyo; sijui Kichina, sijui Kinyarwanda...

Kwa kifupi ni lugha gongana. Weka ya kiswahili au kiinglishi...
 
Nimebonyeza hio link naskia tu watu wanabonga sijui ni kisudani au kiwapi😅
 
Mimi sitishiki na yeyote na sihatarishi yeyote! Kama ulivyosema, namwogopa Mungu tu. Ukinipa email inbox (PM) au kwa namba ya simu 0754887348 utapata audio clip ya mahojiano yetu.
Haa haa :oops: :oops::oops::(:oops:Gwappo Mwakatobe, HAPANA, sikujui na hunijui mkubwa...

Kama haiwezekani kuiweka hapa kwa manufaa ya wote, basi acha ipite...

Hizi ni nyakati za hatari. Usimwamini yeyote. Mwamini Mungu muumba peke yake...!
 
Akili za bavicha na bawacha wanazijua wenyewe eti wanajipa matumanini kabisa ya kushinda uchaguzi ??? .

Haya sisi CCM tunasema hivi tunaingia kwenye uchaguzi tayati tukiwa tuneshinda uchaguzi ngazi ya Urais hakuna namna tutashindwa uchaguzi asimamishwe Lissu, Mbowe, Nyalandu, sijui Membe hakuna ambaye anaweza kufikisha angalau thelusi moja ya kura zote atakazozipata Mh Magufuli.

TUNAENDA KWENYE UCHAGUZI KUTAFUTA NINJ?
Tunaenda kwenye uchaguzi kuhakikisha tunashinda majimbo yote Tanzania bara na visiwani na kuhakikisha tunaongoza Halmashauri zote 184 Tanzania bara.


Sasa Kama kuna mtu anafikiri tunafanya mashala naomba tukutanae tarehe 28/10/2020 tuwafundishe hawa jamaa kwanini mtoto hakui kwa baba ba mama.
Inawezekana hilo likatokea.
Najiuliza tu!!
Gadaffi aliwalipa watu mishahara,watu walijengewa majumba na mengine mengi sana.
Lakini hakupata upendo kiasi cha kukubalika kwa kiasi kikubwa kama unachokisema wewe.
Why unaamini utapata matokeo makubwa kama unavoamini?
 
Back
Top Bottom