Wachambuzi wa soka kama edo kumwembe ni hatari kwa soka letu.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachambuzi wa soka kama edo kumwembe ni hatari kwa soka letu....................

Discussion in 'Sports' started by only83, Mar 9, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Katika hali ya kusikitisha kabisa,napenda kutoa dukuduku langu kuhusu anayejiita mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe....Kimsingi sijui huyu jamaa kasoma wapi taaluma ya michezo,tulikuwa na watu kama Said Mzirai aka super coach mwanangu..hawa walikuwa wamesomea kabisa masuala ya michezo.Leo hii watu kama Edo ni uizi mtupu,kazi yao ni kuchambua mambo kwa ushabiki na kuponda tu.wana fikra za kimagharibi wakati ni watu weusi.....Mimi siwezi kumsikiliza huyu jamaa maana naona ni mbabaishaji tu....................
   
 2. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mcklze hata na mwenzake Shafii Dauda. Tune clouds fm
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ngoja aje hapa Rutashubanyuma...atawameza nyie!
   
 4. S

  SURNAME Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi uchambuzi wa kitu sio lazima usome darasani,inawezekana edo anasoma kwenye mitandao na magazeti ya nje,na kuwa mchambuzi sio lazima ujue kila kitu.Ricky abdallah ameitwa DR.sio kwa kucheza wala kukaa darasani kusomea mpira ni mapenzi na uelewa wake wa soka.Mziray (late)huyu hajawahi kucheza mpira ni mtaaluma wa elimu ya viungo na hakuwahi kuwa mchambuzi wa soka bali mwalimu wa soka na vituo vya tv vilitumia elimu yake ya ukocha.Superspoti wachambuzi wao sio wasomi wa darasani ni wachezaji wa zamani.Labda kama unalililojificha.
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kaka pole nadhani wameiponda timu yako ndicho kinachokuuma tehe. usihalalishe maumivu yako ya kupondwa kwa timu yako iwe ticket ya kuwaharamisha hawa jamaa wabongo hatupendi kuambiwa ukweli.
   
 6. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  umejuaje kama ni mbabaishaji kama huwa humsikilizi. acha wivu wa kijinga. edo kumwembe is among the best football analysits in tanzania
   
 7. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa huyo mziray ndiye nilikuwa simfagilii kabisa! Pamoja na usomi wake. Kumbuka uchambuzi wake kuhusu yule refa aliyeboronga ktk fainali za mataifa ya Africa. Afadhali ya huyo Edo.
   
 8. p

  pires New Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani Edo ni mchambuzi bora zaidi wa soka nchini na huwa haongelei ushabiki anapochambua mpira. Lakini kumbuka kuwa uchambuzi hausomewi kama unavyosema...unajipambanua kutokana na hoja zako. Halafu pia Edo hajiiti mchambuzi hila sisi mashabiki na watu wanaomualika katika Televisheni na magazeti ndio tunamuona mchambuzi. Mara zote nimewahi kumuona akizisifia timu mbalimbali na pia akiziponda. ni vigumu kujua anapenda timu gani. Ana kipaji cha kipekee katika kuchambua mambo ya soka na akiandika Article utapenda jinsi anavyoitumia lugha yake. Kifupi, Article zake zinapendwa na kuaminiwa na wengi kuliko mwandishi mwingine yoyote yule wa michezo nchini.
   
 9. Lonestriker

  Lonestriker JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Edo ni mwandishi bora wa makala za michezo kwa hapa Tanzania na hili halina ubishi.Nahisi muanzisha thread alikerwa na makala ya Edo kuhusiana na mechi ya Simba na Yanga.Alichokiandika Edo ni ukweli mtupu kwani kila aliyeangalia mechi ile anatambua it was so boring especially on Tv.There was no meaningful attack,both keepers were at free holiday,in fact timu zote zingeweza kucheza bila golikipa na bado magoli yasingezidi mawili... Nway, Edo ni fan wa Arsenal though ana ficha sana.
   
 10. Prophet

  Prophet JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Usiumie bure, hawa jamaa hasa edo hana lolote,anajifanya kuchambua wakati watu tunaoshinda tukiperuzi tunafaham wanapodig hizo info na kuzitoa bila hata kuedit. Kwanza huo ni wizi nijuavyo mm, walitakiwa kutoa source. Anachojua ni kujisifia tu.. Mara nilipokuwa K'ro hotela, nilipoenda brazil, nilipopiga picha na nani... Wachambuzi gani wa kusema yale Wasemayo wa maandishi wa magharibi?
   
 11. K

  Kana Amuchi Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pires an lonestriker mmeongea ukweli. edo ni moja kati ya wachambuzi wa soka na waandishi wa makala za michezo ambao wana upeo na wanachokisema au kukiandika tofauti na watanzania wengine wengi tu wanaojitamblisha kama wachambuzi wa soka ama waandishi wa michezo na hata watangazaji wa kibongo wa redio na vituo vya television. wasomi wanasema "no data na right to talk:! hawa jamaa Edo na wenzie (shafii, luambano na maestro) wanafanya kazi zao kwa umakini kwa sababu wanatafuta data. moja kati ya sifa ya mtaalamu yeyote ni kujua wataalamu wengine wanajua nini juu ya kile anachokijua yeye, hawa huperuzi taarifa kwenye mitandao, majarida na magazeti ya sehemu mbalimbali za dunia. Na wanapotoa taarifa hizi husema wazi ni wapi wametoa taarifa hizo na hivyo siyo wizi kama anavyodai Prophet. na ndivyo wachambuzi na waandishi wa michezo hata wa Ulaya na vituo kama supersport hufanya. ni mara chache sana kukuta taarifa za kukurupuka kwenye maandishi na vipindi vyao. watanzania wengi hawasomi, wewe kama unabisha soma magazeti au sikiliza vipindi vya redio na TV zetu. Na ndio maana documentary za kibongo ni chache sana na pengine hakuna kabisa. watu hawataki kutafuta taarifa. Edo ni mkweli, mimi nilikuwa sijui anashabikia the gunners ingawa sikosi kipindi chake na sikosi makala yake kwenye gazeti, kwa sababu unapotakiwa ukweli husema kweli. nina imani anaipenda moja kati ya timu za simba na yanga lakini haachi kusema ukweli inapobidi. kuna siku aliisifia Azam akasema itazipiku simba na yanga kwa vile ina mipango na dira nzuri kiuendeshaji. leo hii siyo siri Azam inakuwa tishio na ndiyo timu inajenga uwanja wake na ina program nzuri ya yosso. tumchukie Edo kwa tathmini ile kwa vile tu mimi ni mpenzi wa Simba?
  mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. ukitaka kupata taarifa zinazoeleweka za mpira sikiliza au soma makala za edo na timu yake. hawababaishi ukilinganisha na wengine wengi kwenye hiyo fani.( na kwa clouds fm hicho ndio kipindi pekee kimebaki cha kusikilizana kuangalia !!).
   
 12. p

  pires New Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Edo mimi sijawahi kukutana naye moja kwa moja. Lakini ukweli ni kwamba jamaa ni bora na namuamini sana. leo anaiponda Arsenal kesho anaisfia, leo anaiponda manchester Kesho anaisifia, leo anaiponda Chelsea kesho anaisifia. Hata Yanga na Simba huwa anazitendea haki kwa kiwango cha juu sana. Anasema anachokiamini, ana uwezo mkubwa wa kukuelewesha, na kama akiandika makala ana uwezo mkubwa wa kupambanua kwa lugha tamu. Anapotoa mifano ya uwepo wake Brazil, Ulaya au wapi ni anawakumbusha tu watu umuhimu wa kusafiri kwa ajili ya kufungua upeo wa ubongo. Hayo si majivuno kwa sababu hata wa waandishi wa Ulaya ndivyo wanavyoandika na hata Mwalimu Nyerere alikuwa anatumia sana mifano ya anavyosafiri na kuona. tukumbuke Seeing is Believing!
   
 13. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni kweli. Vigumu kujua anashabikia timu ipi na hayuko biased.
   
 14. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kuna siku kulikuwa na michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2002 kama sikosei, kuna mchangiaji mmoja alisema wataalamu wa soka la Tanzania walitakiwa waende kwenye hizi michuano kwaajili ya kujifunza na kupata ujuzi wa kuinua soka la Tanzania.

  Edo alivyosikia hivyo, akadakia na kumwelewesha mtangazaji siku hiyo alikuwa Maulid Kitenge wa ITV alisema watu kama sisi (akiwa na maana ya yeye Edo) tulitakiwa tuende kwenye hayo mafunzo, Maulid alicheka sana maana Edo kama vile aliutaka huo ulaji wa kufika majuu.
   
 15. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ndo wale wale! Wivu wa kijinga kweli. Hivi hiyo huwezi kujua kama ilikuwa ni joke
   
 16. p

  pires New Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mopao, mbona as long as i know Edo amesafiri sana. Alikwenda Brazil na timu ya taifa, alikwenda Senegal, alikwenda Ghana katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2008, alikwenda Afrika Kusini katika michuano ya Confederations mwaka 2009..sina uhakika kama alikwenda kombe la dunia. Nadhani ilikuwa Jokes tu kwa sababu yeye, na hata yule mchambuzi mwenzake Shafii wamekuwa wakienda nje mara nyingi tu. Nadhani ulikuwa utani tu though sijui maisha yake kwa undani sana. Tuache wivu, Edo anajua sana, kama ilivyo kwa akina Shafii na wengineo
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Thats obvious....kazi yao ni kusema nilikuwa huku mara kule.................shiiiiiiiiiiiiittttttttttttttttttt
   
 18. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  teheteh wat about kibonde.?kwangu ndo commentator mzuri
   
 19. V

  Vas P Member

  #19
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli ni commentator mzuri wa masumbwi na kuponda wenzake.....
   
 20. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Katika watu ambao walikuwa hawajui kitu Mzirai ni mmoja wapo tena afadhali hata ya edo, mzirai alikuwa ni mtu wa majungu na fitna tu ya kuwahonga kina ngasa na mgosi wasifunge kwenye timu ya taifa ili maximo aonekane mbaya
   
Loading...