Wachambuzi wa soka bongo na unazi maandazi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachambuzi wa soka bongo na unazi maandazi!!

Discussion in 'Sports' started by Mwanamageuko, Jul 11, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana, hawa makocha wetu walioalikwa kuchambua soka hususan STAR TV! Walikuwa wanaboa vibaya,hawakuwa wachambuzi wa soka bali UNAZI! walikuwa wanashabkia wachezaji na kuwazodoa waalimu wa timu husika. Wakiwasifia wachezaji wetu wa ndani bila kujua afya zao, kiasi kwamba wakapelekea wachezaji kuchezeshwa wakiwa wagonjwa kwa shinikizo!
  Hakuna cha maana kilichofanywa na wachezaji waliokuwa wakiwashabikia na kuwapigia debe zaidi ya kurudi kwenye maumivu yao....
  Huwezi kumzidi kujua mtu kuliko yule anaeishi nae....

  Makocha wetu wa Kizalendo, ikiwa ninyi mna uwezo si padisheni timu mlizonazo viwango!? Msiwalaumu wachezaji wetu na makocha wa nje, waacheni wafanye kazi zao ili muepuke aibu. Mnapopewa nafasi ya kuchambua soka CHAMBUENI SOKA na SI KUZODOA WACHEZAJI...
  LA ASAMOAH ni FUNZO KWENU.
   
 2. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli mimi jana nilisikitishwa sana na uchambuzi uliokuwa ukifanywa na huyo anayejiita Kanakamfumu. Mwanzo mwisho anamlaumu kocha wa Yanga, eti kwanini hawatoi Mwape na Taita wanaharibu! Lakini simshangai, maana huwa anaiandika vibaya Yanga kwenye makala zake kwenye gazeti la mwanaspoti, mara ooh, kwa usajili huu Yanga haifiki kokote, mara sijui wachezaji wa kigeni hawatusaidii chochote, n.k. Nilimshangaa zaidi alipokuwa anamlaumu Tegete kwa kurudi kati kutafuta mipira, eti yeye ni straika kwa nini asisubiri kule golini aletewe mipira (sina hakika kama huwa anajishughulisha kuangalia mipira ya nchi za wenzetu, ameshamuona Drogba au Rooney anapotafuta mpira na kufua baada ya kutoa pasi)! Halafu anjidai na yeye kocha, wakati timu zote alizofundisha zimeshuka daraja! Anyways, hizo ni chuki binafsi kwa kutoswa, taaluma yenye ndo hiyo, akili mgando! Shame on you Kanakamfumu!!!
   
Loading...