Wachambuzi wa Mpira katika Redio za Tanzania tutaanza Kuwadharau sasa, Goli la Yanga SC lilikuwa halali kwa Uzembe wa Kipa

Baada ya Golikipa "kuutema" ule mpira, ulianguka kwa Yannick Bangala.
Bangala alimpa pasi (assist) Fiston Mayele ambaye alikua kwenye eneo la kuotea.

Hivyo incidence ile ni offside.

Kwa sababu binadamu tumeumbiwa kusahau, teknolojia ina tabia ya kutukumbusha.

Tazama hapa...

Rudia tena kuangalia uone nani alikuwa offside position

Ni moloko ww

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli ni kiri tu kuwa hili nilikuwa silijui. Nilijua kipa anapotoka anakuwa anahesabiwa kama mmoja wapo wa timu inayozuia. Hivyo beki na kipa kufanya idadi ya wawili. Ila nashukuru umenifanya nilifatilie hili na nimejiridhisha pasi na shaka kuwa ni clear offside. Jamani tusiojua hili tupitie hii kuna hadi mifano ya hili sheria ya offside kipa anapokuwa katoka.
Usijali mkuu. Ndio maana ya platforms kama JF, tunajuzana hili na lile. Uwe na wakati mwema.
 
Rudia tena kuangalia uone nani alikuwa offside position

Ni moloko ww

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Achana na watu wote ambao hawajahusika na mchezo, (those who were not involved in a play).
Watazame watu waliohusika moja kwa moja na mchezo kwa kuugusa mpira.

Saido, Aucho, Ssettuba, Bangala na hatimaye Mayele. Hao watano tu.

Unayemtaja wewe hajahusika na mchezo (wasn't part of build up of that goal).

Wakati Bangala anapiga pasi ya mwisho kwenda kwa Mayele, Mayele tayari alikua kwenye eneo la kuotea.
Kwanini alikua ameotea, ni kwa sababu mbele yake kulikua na mchezaji mmoja pekee wa biashara (beki aliyepo golini), ili isiwe offside ni lazima mbele kuwe na wachezaji angalau wawili.

Mkuu, hili bado tu halieleweki ?
Jesus Moloko anatokea wapi hapa ?
 
Wachambuzi wa hovyo kabisa, Mimi walinishangaza wachambuzi wa Azam Sports 1, kipindi Cha mapumziko, kutokuongelea utata uliopo dhidi ya zile offside za dhulma, yaani sijui wanaogopa Nini! Wajifunze basi ata kwa wenzao wa ulaya, utata Kama ule uwa unaongelewa kwa kwa undani zaidi ikiongozwa na utoaji wa Elimu.

Ila wa huku bongo sijui ni nini yaani, maoga mno ata kuongelea, wakati Ile ni tasnia yao, yawapasa kuongea kwa uwazi zaidi na hata kurumbana kwa hoja, ila mioga mno michambuzi ya huku, wanaboa!!

Yanga jana ilishinda kwa kutumia ubabe tu. Ila waamuzi wa Bongo sijui wapewe semina ya aina gani! Maana wana mapungufu mengi sana ya kiuchezeshaji.
 
Achana na watu wote ambao hawajahusika na mchezo, (those who were not involved in a play).
Watazame watu waliohusika moja kwa moja na mchezo kwa kuugusa mpira.

Saido, Aucho, Ssettuba, Bangala na hatimaye Mayele. Hao watano tu.

Unayemtaja wewe hajahusika na mchezo (wasn't part of build up of that goal).

Wakati Bangala anapiga pasi ya mwisho kwenda kwa Mayele, Mayele tayari alikua kwenye eneo la kuotea.
Kwanini alikua ameotea, ni kwa sababu mbele yake kulikua na mchezaji mmoja pekee wa biashara (beki aliyepo golini), ili isiwe offside ni lazima mbele kuwe na wachezaji angalau wawili.

Mkuu, hili bado tu halieleweki ?
Jesus Moloko anatokea wapi hapa ?
Wewe naye ni mchambuzi ?!. Hovyo kabisa

Tanganyika uswahili wa kipuuzi
 
Ile ni clear offside. Mchezaji wa mwisho sio lazima awe golikipa.

Hii sheria nishawahi kumsikia Amri Kiemba akiielezea vizuri sana clouds, na leo incidence hiyo imetokea.

Hongera kwa mwamuzi kwa kuichanganua vyema hiyo sheria ya offside.
 
Asee! Kumbe ndio maana hii nchi imejaa watu wajinga wengi.

Umesoma sheria ya offside kweli au ni uswahili tu kujifanya mnajua na kumbe ukiazi tu
Mkuu acha kutudanganya, wakati Bangala anapiga pasi kwenda kwa Mayele, haumuoni beki wa biashara akiwa yupo golini? Mayele kapokea pasi akiwa onside position. Rudia hiyo video kutazama halafu angalia position aliyosima mayele vs position aliyokuwepo beki wa Biashara halafu niambie nani alikuwa mbele ya mwenzie
 
Asee! Kumbe ndio maana hii nchi imejaa watu wajinga wengi.

Umesoma sheria ya offside kweli au ni uswahili tu kujifanya mnajua na kumbe ukiazi tu
Sawa mkuu nashukuru mimi ni mjinga na ndio maana niliyem quote alinipa ufafanuzi kisha nikaenda kujiridhisha na kukiri kuwa sikuwa nalifahamu hilo hapo kabla. hakuna anayejua kila kitu, wewe kama una uelewa wa kila kitu basi utakuwa miongoni mwa waliopo kwenye kundi la malaika sio binadamu. Endelea na kashfa nyingine zaidi ya hilo la kuniita mjinga kwasababu nilishakiri ni mjinga, heri yako wewe ambaye sio mjinga kisa tu unajua sheria ya offside.
 
N off side nawew Hawa wachambuz na waamuz wana mapungufu yao ila ukiangalia apo n offside clear kabisa ilianzia Kwa aliyetoa pasi kwa mayele
 
Mkuu acha kutudanganya, wakati Bangala anapiga pasi kwenda kwa Mayele, haumuoni beki wa biashara akiwa yupo golini? Mayele kapokea pasi akiwa onside position. Rudia hiyo video kutazama halafu angalia position aliyosima mayele vs position aliyokuwepo beki wa Biashara halafu niambie nani alikuwa mbele ya mwenzie
We kwel sheria huzijua kbsa...embu kazipitie then uje...
 
Back
Top Bottom