Wachagga wa Rombo, hii sasa laana! Mwaua mama wa mtoto kisa mtoto kakomba msosi wa jirani?

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,881
13,165
Inachekesha na kuhuzunisha hapo hapo.

Huko Rombo kwa kina bwashee, kijana wa darasa la sita karudi toka shule. Nyumbani hakukuta msosi, lakini kwa jirani akasikia harufu nzuri ya ngararimo, chakula mahususi na maarufu cha kichagga.

Kijana akakinyatia chakula kile, akala na kukimaliza. Lakini akila fundo la mwisho....hamadi mwenyewe huyu hapa.

Kijana katika nduki, moja kwa moja kwao na kukwea darini. Wafukuzaji aliowaacha nyuma wakafika pale nyumbani kwa kijana na kumkuta mama wa kijana.

Kwa hasira wananchi hao wakaanza kuuliza kwanini hamlishi kijana wake na wamechoka kuibiwa misosi na kijana ambaye amekuwa kama mbwa koko.

Kwa kutopata majibu kikaanza kisago cha mbwa koko, tena kama cha afande Moroto wa Dodoma! Mama masikini akaugulia siku ya kwanza ya pili akaaga dunia.

Hapo ndo nawashangaa wachagga wa Rombo.

Ref. pg 30 ,Mwananchi, 14/2/2019.
 
Back
Top Bottom