Wachaga No.1, Wasambaa No.2, Wanyakyusa vuta mkia.

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Ukitaka kujenga kiwanda cha Pombe nenda Moshi, utaokoa gharama kubwa za usambazaji.

Jafari Shekanabo Shekifu na Mrindoko Mchome Senkoro walijitolea kukusanya damu nchini kusaidia vitengo vya dharura vya taasisi za tiba. Kwenye fomu ya kuchukuwa taarifa za mchangiaji damu waliweka sehemu ya kujaza kabila la mchangiaji. Mbali na ukusanyaji damu, lengo la msingi la zoezi hili pia lilikuwa ni kutumia damu hizo kama sampuli ya kutafiti kabila lenye alcohol nyingi kwenye damu. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kwamba Wachaga wanaongoza kitaifa na kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kaskazini kwa kiwango kikubwa cha alcohol kwenye damu zao, wakifuatiwa kwa karibu na Wasambaa. Wanyakyusa licha ya kuwa kwenye ukanda wa baridi kama Wachaga na Wasambaa; walishika nafasi ya mwisho kwa makabila yenye alcohol nyingi kwenye damu nchini. Walibaini sababu za Wachaga kuongoza kitaifa na kikanda kuwa ni:-

1. Baridi.
2. Masharti ya matambiko.
3. Kukosekana hofu ya Mungu.
4.Biashara ya Bar.

Katika hatua nyingine iliyoshangaza wengi, baadhi ya Wachaga waliohojiwa walilalamika na kuomba kwamba Katiba ibadilishwe ili gongo isiitwe Pombe-ya-Moshi badala yake ipewe jina jingine mfano Pombe-ya-Lushoto au hata Pombe-ya-Same.

NB: Namba 2, 3 na 4 havikuwa na nguvu kubwa kwa Wanyakyusa. Aidha, ripoti ya utafiti huu ilitunukiwa ela nyingi na vitengo vya masoko na utafiti vya makampuni ya vilevi kwa kuwa inawasaidia kujuwa wapi kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa zao. Kisa siyo halisi.

Na, Douglas Majwala.
 
Back
Top Bottom